Na Lucas Myovela_Arusha

Serikali mkoani Arusha imeitaka kamati inayoshughulikia kuhamasisha upigajo vita wa mimea vamizi ,kutoa elimu kwa kushirikiana na wataalamu kwa taasisi mbalimbali za serikali, ikiwemo mifugo,Kilimo,Mazingira na wizara ya Afya, mashuleni na maeneo mbalimbali ya jamii juu ya mimea vamizi wa gugu karoti.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ,kwenye siku ya maadhimisho ya siku ya gugu karoti na visumbufu vamizi vya mazao mkoani Arusha ,kongamano lililofanyika wilayani Arumeru ,katika Taasisi ya Utafiti wa viwatilifu kwa ukanda wa kitropiki (TPRI)Mkoani hapa.

( Ikumbukwe kuwa Katika siku kadhaa mmea huo wa gugu karoti umekuwa sumbufu katika jamii zetu hasa katika wanyama na mimea hushambuliwa sana na gugu hili ambalo ni hatarishi katika jamii zetu.)


Kwitega ameeleza kuwa pasipo kuwa na ushirikiano wa pamoja kati ya wataalamu na wadau wa maendeleo   kazi hiyo haitakuwa na maana wala mafanikio ,hivyo kila mmoja analojukumu la kuhakikisha anafanyakazi kwa nafasi yake, ili elimu na uelewa iwafikie jamii kwa ujumla katika mapambano hayo.

"Natoa wito kwa kamati ya udhibiti wa visumbufu vamizi kushirikiana na wataalamu mbali mbali wa serikali ili kuweza kudhiti gugu karoti mkoa wa Arusha pia washirikiane na tasisi zabutafiti ili kuweza kuondoa visumbufu vamizi na kusaidia jamii ili kuondokana na vita ya umasikini inayosambishwa na visumbufu vamizi".alisema Kwitega.


"Kumekuwa na visumbufu vamizi mbali mbali hapa nchini mfano gugu maji kule kanda ya ziwa katika maeneo ya Musoma na Mwanza lakini pia niwapongeze wataalam mbali mbali wanao pambana kila siku kupambana na visumbufu vamizi hivi maana lengo ni kuondoa tatizo na kuleta tija katika jamii maana hili gugu karoti linaathiri mazingira yetu na wanyama wetu pamoja na sisi wenyewe." aliongeza kwitega.

Pia Ametoa wito kwa Waandishi wa habari ambao ni wadau muhimu na jeshi la mianvuli, kutumia vyema kalamu zao kuhabarisha jamii juu ya gugu hilo vamizi ,kwa kutoa elimu kwa umma juu ya madhara na namana ya kuliangamiza gugu hilo.

Nae kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati uhamasishaji wa kudhibiti gugu hilo Bw Ndelekwa Kaaya , alisema kuwa  dhumuni la  siku hiyo ni  kuwahamasisha na kutoa Elimu ya uelewa kwa  wadau wa kilimo,mifugo,mazingira,afya ya binadamu,viongozi wa dini,viongozi wa kimila taasisi za Elimu ,makundi maalum watafiti ,wanasayansi ,wafanyabiashara viongozi wa siasa wafahamu kuhusu madhara na udhibiti wa Gugu karoti na visumbufu vamizi katika mkoa wa Arusha, na mikoa mingine ambapo kuna visumbufu vamizi.

Alisema katika siku hiyo mada mbalimbali zinazohusiana na ueneaji usambaaji na mbinu,njia za kuzuia na kudhibiti visumbufu vamizi zitatolewa na wataalam mbalimbali toka taasisi za serikali na sekta binafsi ili kujenga uelewa kwa jamii ya watanzania.

"Japokuwa  jitihada zilizofanywa na kamati katika harakati za kudhibiti gugu hilo ni pamoja na kushirikiana na taasisi binafsi ,zimeweza kufanya utambuzi wa visumbufu vamizi ,na kuainisha maeneo yaliyo vamiwa na gugu hilo".

Pamoja na hatua nzuri tuliyo ifikia bado changamoto zinazo tukabili  katika kutekeleza majukumu yetu ni pamoja na ukosefu wa rasilimali fedha, kwaajili ya kuwezesha uhamasishaji wa kuzuia na kudhibiti visumbufu vamizi, ikiwemo kuwafikia wadau wengi katika maeneo yaliyovamiwa mkoani Arusha". Alisema Kaaya.

Aidha ukosefu wa vifaa vitendea kazi ,vifaa kinga vinavyotakiwa kutumika katika zoezi la ung’oaji wa visumbufu vamizi haswa katika maeneo mbalimbali katika barabara za jiji la Arusha, ambapo ushirikiano mdogo kutoka kwa wadau wenyewe katika maeneo yaliyovamiwa na visumbufu vamizi likiwemo gugu karoti". Aliendelea kusema Kaaya.

Ramadhani Kilewa ni Mtafiti kitengo cha kidhibiti visumbufu vya mimea kutoka (TPRI) amesema kuwa aina hiyo ya visumbufu vya wadudu na wanyama ni tatizo katika mikoa yote nchini Tanzania,ambapo maeneo mengi yaliyovamiwa ni mashamba ya mazao ,malisho ya wanyama,Hifadhi za taifa ya Arusha ,Ziwa manyara , Serengeti na Ngorongoro,maeneo ya makazi ya watu ,maeneo ya kutunza na kusambaza nishati ya umeme ,mabwawa ya maji kwaajili ya matumizi ya binadamu na  wanyama. 

Kilewa ameyataja  madhara yatokanayo na gugu hilo kuwa ni pamoja na magonjwa ya aleji ya ngozi kwa binadamu na wanyama,kifua kinachobana (pumu)kwa binadamu,umasikini  katika ngazi ya familia, kata ,wilaya na mkoa.(pumu)kwa binadamu.

 Kiuchumi gugu hilo linasababisha kupungua kwa mavuno ya mazao ya chakula na biashara,Athari katika biashara ya utalii na wanyama kushindwa kupita kwenye baadhi ya mimea vamizi,maziwa ya wanayama wanaofugwa kuwa na uchungu kwasababu ya sumu iliyomo katika mimea vamizi,upungufu wa malishio ya wanyama pamoja madahara kwa afya ya udongo na uoto wa asili na uharibifu wa mazingira 

Aidha asili ya gugu hilo kwamba ni Amerika ya Kusini,A.kati na A.Kaskazini maeneo ya Mexico, hapa nchini Tanzania liliingia mwaka 2010  limetokea nchini Ethiopia,ambapo mmea mmoja huweza kutoa mbegu 15,000 ,25,000-100,000 na zinauwezo wa kuzaa kila baada ya  miezi 4,mmea mmoja unaweza kutoa miche kwa mara tatu,unauwezo wa kukaa ardhini kwa miaka kumi.

"Zinaene kwa njia ya upepo,utengenezaji wa barabara,upepo binadamu wenyewe,asaia ,Afrika,visiwa ,Austaralia Afrika ya kusini,nchi zote za afrika ya nmashariki kwa afrika zaidi ya 13,kwa Tanzania taarifa iliyopo ni mikoa mitano,inaathiri uoto wa asili,inazuia mbegu za mazao zisiote ,inasaidia uzaliaji wa wadudu,vimelea vya magonjwa kwenda kwenye mazao mengine,inzi weupe.Alisema Kilewa.



Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: