Na Woinde Shizza,Arusha

Watanzania wametakiwa kuwatunza watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuwa watoto hao wengi wao Wana ndugu hapa nchini lakini pia baadhi wazazi wao wapo hai.


Akizungumza katika hafla ya kufungua kituo cha Amani Cha Makazi Salama na kuokoa watoto wa mitaani kilichopo kaloloni Jijini Arusha, Kamishna wa Ustawi wa Jamii,Dkt.Naftali Ng'ondi  amesema kuwa dhana ya kuliacha kundi hili kutunzwa tu na wageni kutoka nje  ya nchi haileti taswira nzuri.

Aidha Dkt.Ng'ondi alisema kuwa ni vyema watanzania wakajenga utaratibu wa kuchangia Kundi hili ili kupunguza baadhi ya changamoto badala ya kuwaachia wageni kutoka nje.

"Hii dhana haileti taswira nzuri Jamani tumekuwa tukiwaachia wageni tu kuchangia kuanzia masomo , chakula,na mengineyo kwanini hatujishughulishi na hawa watoto wakati ni watanzania "alihoji dkt.Ng'ondi

Hata hivyo aliitaka kamati ya ulinzi kwa watoto mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa inaendelea kutoa elimu Juu ya ukatili kwa mtoto kwa kuwa takwimu zinaonesha kuwa vitendo hivyo vimekidhiri katika mkoa wa Arusha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Amani na  Makazi Salama Cha kuokoa watoto wa mitaani  Mendert Schaap alisema kuwa kituo hicho kinalea watoto zaidi ya 300 na kuwapatia elimu na kuwakutanisha na wazazi wao.

Bw.Schaap alisema kuwa mbali na kuwawezesha  watoto wanaoishi mitanii makazi hayo Salama,yatawawezesha watoto kupatiea misaada Mbali Mbali na kujiendekeza kiuchumi na kielimu.

Mmoja wa watoto aliyeokolewa mtaani anayefahamika kwa jina la Marry Christopher (19) alisema kuwa aliingia mtaani akiwa na miaka kumi tu na aliweza kuishi ndani ya miaka miwili mtaani Kama mtoto wa kiume ili aweze kukwepa vitendo vya ukatili.

Marry alisema kuwa kituo cha Amani kimeweza kumpatia elimu na Sasa ni mwalimu ambaye anafundisha kuchomelea vitu Mbali Mbali na kuwataka  watoto wa mitaani pindi wanapokolewa kutumia vyema nafasi ya elimu na  kupata ujuzi .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: