Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma 
salamu za pole kwa familia ya Agness Gerald Waya kufuatia kifo cha mtoto
 wao Agness alimaarufu kama Masogange kilichotokea Ijumaa.
Rais
 Magufuli ametuma salamu hizo kupitia kwa Mwenyekiti Jumuiya ya Umoja wa
 Vijana UVCCM Bw. Kheri James na kusema kuwa amesikitishwa sana na kifo 
cha binti huyo kwani kifo chake kinapunguza idadi ya vijana ambao ndiyo 
jeshi na watu ambao wanaweza kufikisha mbali taifa. 
"Kupitia
 jukwaa hili naomba nitoa salamu za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi 
(CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe 
Magufuli ambaye leo amewasili mjini Dodoma lakini ameomba niwasilishe 
kwenu salamu za pole kwa kuondokewa na kijana mwenzetu, 
"Mwenyekiti
 anafahamu nchii hii sisi vijana ndiyo warithi wa taifa hili sisi ndiyo 
tumebebe dira ya kulifikisha taifa ambapo tunadhani linafaa kufika hivyo
 anasikitishwa sana kuona katika jeshi kubwa kama hili la vijana 
tunapungukiwa na vijana wenzetu wanaondoka na kupunguza idadi ya askari 
wetu , naomba mpokee salamu za Mwenyekiti wetu" alisema Kheri James 
Mwili wa Agness Masogange utazikwa jijini Mbeya nyumbani kwa wazazi wake Mbalizi

Post A Comment: