Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. PAUL MAKONDA anawatangazia Wawanake wote waliotelekezwa na wanaume zao na hawapatiwi fedha za matunzo ya Mtoto kufika ofisini kwake siku ya Jumatatu ya April 09 kwaajili ya kupatiwa msaada wa kisheria.

Jopo la wataalamu wa Sheria, Maafisa Ustawi wa jamii na Askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia wamejipanga ipasavyo kukuhudumia na kuhakikisha mzazi mwenzio anatoa fedha za matunzo ya Mtoto.

Huduma hii inatolewa Bure chini ya uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya Tano.

EWE MWANAMKE HUU SIO WAKATI WA KULIA WALA KUTESEKA,SERIKALI YAKO ITASIMAMA NA WEWE KUHAKIKISHA UNAPATA HAKI YAKO ULIYOIKOSA KWA MUDA MREFU.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: