Jina lake halisi ni Salim H Njwete au Samjet. Unaweza ukawa umewahi kumuona sehemu. Mwaka 2012, alikuwa mshindi wa shindano la Dume Challenge lililowakutanisha vijana 20 wababe wa mazoezi na kazi ngumu. Salim alijinyakulia kitita cha shilingi milioni 20. 

 Salim Njwete aka Scorpion (Kushoto) akikabidhiwa mfano wa hundi kufuatia kutangazwa mshindi wa shindano la Dume Challenge, December 2012

Ni mwalimu wa karate na mbabe wa mapigano na ndio maana pindi anamshambulia Said hakuna aliyethubutu kumsaidia kwasababu kila mtu maeneo ya Buguruni anamhofia.

Ni muigizaji wa filamu pia na kwa mujibu wa Walter, aliyekuwa mshiriki mwenzake kwenye Dume Challenge, baada ya mashindano hayo Salim alitoa filamu moja.

Alivyokuwa Mdogo Alikataa Kusoma Mama Yake Mzazi Alishafariki Siku Nyingi Na Alikuwa Akilelewa Na Mama Yake Mdogo Maeneo Ya Yombo Buza.

Alishawahi Kufungwa Jela Japo Haijajulikana Alikosa Nini, Na Jina Lake Kamili Ni Salum Njwope Na Jina Hilo Nila Babu Yake. Yeye Ni Mwenyeji Wa Mkoa Wa Shinyanga. Kwa Mujibu Wa Mama Yake Mdogo Anasema Scorpion Alipokua Akitoka Nyumbani Usiku Saa Mbili Anamuaga Mama Yake Mdogo Huyo Kuwa Anakwenda Kwenye Kazi Ya Ubaunsa Katika Club Kumbe Mwenzie Alikuwa Anaenda Buguruni Kuibia Watu Mpaka Asubuhi Ndio Anarudi Nyumbani.

Pia Scorpion Ashawahi Kushiriki Katika Shindano Lililojulikana Kama Dume Challenge Kama Miaka Mitatu Iliyopita Na Aliibuka Mshindi. Napia Alianza Mafunzo Ya Kucheza Caret Tangu Akiwa Mdogo Sana Napia Ni Mtu Mwenye Nguvu Za Kuzaliwa Nazo.

Kuna Kipindi Aliondoka Nyumbani Kwao Kwa Muda Mrefu Mama Yake Mdogo Anadai Alikuwa Hajui Yuko Wapi Mpaka Baadae Aliporudi Mwenyewe Nyumbani.Amekamatwa Na Polisi Baada Ya Kutuhumiwa Kumjeruhi Mkazi Mmoja Wa Dar Es Salaam Eneo La Buguruni Kwa Kumng’oa Macho Katika Kitendo Kilichoelezwa Kuwa Ni Wizi Wa Fedha.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: