Baraza
la usalama la Umoja wa Mataifa kwa wingi wa kura limemteua aliyekuwa
waziri mkuu wa Ureno Antonio Guterres kuwa katibu mkuu mpya wa umoja
huo.
Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa unatarajiwa kufanyika wiki ijayo kuidhinisha uchaguzi wake kwa muhula wa miaka mitano.
Bwana
Guterres ,mwenye umri wa miaka 67,ambaye aliongoza kitengo cha wakimbizi
katika Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka 10 atachukua mahala pake
Ban Ki-moon mapema mwaka ujao.
Bwana Ban mwenye umri wa miaka 72,alimtaja bwana Guterres kama 'chaguo zuri' la kumrithi.
''Uzoefu
wake kama waziri wa Ureno, ujuzi wake wa maswala tofauti duniani na
ukakamavu wake utamsaidia katika kuliongoza shirika hilo la Umoja wa
Mataifa katika kipindi muhimu'' ,bwana Ban aliwaambia wanahabari
alipozuru mjini Rome.
Post A Comment: