Kampuni
kadhaa nchini China zimetangaza kuwafuta kazi wafanyakazi wake
watakaoingia madukani kununua simu mpya za kampuni ya Apple ambazo ni
Iphone 7.
Baadhi
ya kampuni hizo zimedai kuwa zimeamua kuchukua maamuzi hayo kutokana na
sababu za kizalendo huku nyingine zikisema zinataka kuwafundisha
wafanyakazi wake kutopenda sana raha na anasa za dunia.
Mtandao
mmoja umemnukuu msemaji wa kampuni ya Nanyang Yongkang Medicine, Liu
akisema lengo la agizo hilo ni kuwahamasisha pia wafanyakazi kuangalia
zaidi familia na kuachana na vitu vya starehe ambavyo si vya lazima.
Hata
hivyo baadhi ya watu wamesema kuwa maamuzi ya makampuni hayo huenda
kukawadhuru wachina wenyewe kwa kuwa uzalishaji wa simu za Apple
hufanywa katika viwanda vya kampuni ya Foxconn nchini Uchina.
Simu hizo zinauzwa kwa kiasi cha $1,047 kwa nchi ya China.
Post A Comment: