www.msumbanews.blogspot.com

 

Programu hiyo ni jibu la Google kwa programu nyengine kama ile ya Apple ya Face Time,Skype ya Microsoft na Facebook messanger.

Haina tofauti kubwa na programu nyengine zinazotoa huduma za video,isipokuwa inakupatia uwezo wa ni nani anayepiga simu hivyobasi kumpatia mtumiaji fursa ya kuamua iwapo ataipokea simu hiyo au la.

Google inasema kuwa programu hiyo imetengezwa hali ya kwamba inakubishia hodi kabla simu kuingia.

Programu hiyo mpya iliotangazwa mwezi Mei inazinduliwa kama huduma ya bure kwa simu zinazotumia Android pamoja na simu za Apple za iPhone.

Simu zinalindwa na haziwezi kudukuliwa na video hubadilika kulingana na kasi ya kushika simu inayopigwa.

Kama programu ya FaceTime ,duo inahitaji nambari ya mtu ya simu kuunganishwa.

Huduma nyengine zinahitaji mtumiaji kuingia katika akaunti zao ili kupata fursa ya kupata huduma hiyo.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: