Monday, 14 October 2019

LIVE: Kilele Cha Mbio Za Mwenge Wa Uhuru, Kumbukumbu Ya Baba Wa Taifa Mwalimu JK Nyerere Mkoani Lindi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli anahudhuria maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Wiki ya Vijana Kitaifa katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA KIJIJI CHA NYUKI KISAKI MKOANI SINGIDA


 Mwalimu wa Chuo cha Ufugaji Nyuki cha International Beekeeping Open School & IPPE, Salvatory Millinga (wa pili kushoto) akiwaelekeza wanafunzi wa chuo hicho namna ya kulina asali kutoka kwenye mzinga wakiwa katika mavazi maalumu wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika Kijiji cha Nyuki cha Kisaki mkoani Singida juzi.
 Rais wa Umoja wa Vijana Wajasiriamali na Wataalamu wa Miradi Mkoa wa Singida (SYECCOS) Philemon Kiemi akuzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliotembelea Kijiji cha Nyuki cha Kisaki kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida.
 Kiwanda cha kuchakata asali kilichopo katika kijiji hicho cha nyuki.
 Mafundi wakichimba shimo la maji taka yanayotoka katika kiwanda hicho.
 Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakipanga chupa zenye asali kabla ya kupelekwa sokoni.
 Rais wa Umoja wa Vijana  Wajasiriamali na Wataalamu wa Miradi Mkoa wa Singida (SYECCOS) Philemon Kiemi akiweka asali iliyochakatwa kwenye chupa ya nusu lita tayari kwa kuwekwa lebo na kupelekwa sokoni.
 Kiemi akiwaonesha waandishi mashine ya kuchakata asali jinsi inavyofanya kazi.
 Kiemi akizungumza na mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika chuo cha ufugaji nyuki kilichopo kwenye kijiji hicho cha nyuki aliyetokea mkoani Ruvuma.
 Fundi mkuu wa kutengeneza mizinga ya nyuki akionesha moja ya mizinga ya kisasa ya nyuki ambayo inatengenezwa katika kijiji hicho.
 Moja ya bweni la kulala wanafunzi 12 linaloendelea kujengwa katika kijiji hicho cha nyuki.
 Mizinga ya nyuki ikiwa katika kijiji hicho cha nyuki.
 Baadhi ya magari yanayotoa huduma ya usafiri katika kijiji hicho.
 Jengo la ofisi kuu ya kijiji hicho likiendelea kujengwa.
 Kiemi akiwaonesha wanahabari shamba la kijiji hicho.
 Kiemi akionesha namna ya mizinga ya nyuki inavyotakiwa kuwekwa kwa mpangilio.
 Hapa Kiemi akitoka kukagua moja ya ofisi inayojengwa kwenye kijiji hicho.
 Mzinga ukiwa umening'inizwa kwenye mti.
 Madaraja ya reli ni moja ya kivutio cha utalii kwenye kijiji hicho cha nyuki.
 Muonekano wa jengo la Utawala katika kijiji hicho.
Wanafunzi na Mwalimu wa chuo cha ufugaji nyuki katika kijiji hicho  Salvatory Millinga (wa pili kushoto) wakionesha uvaaji wa vazi maalumu la kulinia asali.

Na Dotto Mwaibale, Singida

WAFUGAJI wa nyuki nchini wametakiwa kuacha dhana ya kuelewa kuwa nyuki wanamazao mawili  tu za asali na nta wakati wanamengine matano yenye thamani kubwa.

Hayo yalisema juzi na Rais wa Umoja wa Vijana wa Wajasiriamali na Wataalamu wa Miradi Mkoa wa Singida (SYECCOS), Philemon Kiemi wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Kijiji cha Nyuki cha Kisaki kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida.

" Pengine kutokana na uelewa mdogo wa wakufunzi wa ufugaji nyuki ndio uliosababisha wafugaji wa nyuki hapa nchini kubaki na dhana ya kuwa mazao ya asali na nta ndiyo yenye thamani kubwa katika ufugaji wa nyuki" alisema Kiemi.

Kiemi alisema nyuki wana mazao mengine matano ukiondoa nta na asali yaliyozoeleka na wananchi na wafugaji ambayo yanathamani ndogo sana.

Aliyataja mazao hayo mengine yatokayo na nyuki na bei zake kuwa ni Gundi ambayo bei yake kwa kilo ni sh.150,000, maziwa sh.milioni 4 kwa lita, chamvua sh.300, 000 kwa kilo,supu ya nyuki sh.50,000 kwa lita na sumu ya nyuki sh.400,000 kwa gramu.

Alisema mkulima aliyedhamiria kufuga nyuki kiukweli hawezi kutamani kufanya biashara nyingine kutokana na kipato kikubwa anachoweza kukipata ambapo hata akiuza gunia moja tu la mahindi haliwezi kufikia thamani ya kilo moja ya zao la gundi litokanalo na nyuki.

" Ufugaji nyuki hauhitaji madawa mvua wala gharama yoyote zaidi ya kuwa na mizinga yako lakini kilimo cha mahindi, alizeti na mazao mengine kinahitaji mahitaji mengi kama mbolea, madawa, mvua na mambo mengine yanayo mgharimu mkulima tofauti na ufugaji wa nyuki" alisema Kiemi.

Akifafanua zaidi Kiemi alisema ana ndoto ya kuwabadilisha asilimia 70 ya wakulima hapa nchini ili wawe wafugaji wa nyuki kwa sababu ufugaji wa nyuki unatunza mazingira, unatoa ajira nyingi na soko lake ni kubwa ndani na nje ya nchi akitolea mfano wa bei ya gunia moja la mahindi na mbuzi mmoja ni sawa na lita moja ya asali ya nyuki wadogo.

Kiemi ambaye ana vijiji  vitatu vya nyuki mkoani Singida vyote vikiwa na ekari 7000 ni mfugaji wa nyuki wa kwanza Barani Afrika kwa kuwa na mizinga zaidi ya 13,000 akizidiwa na raia mmoja wa Mexico aitwaye Miel Carlota ambaye wanakampuni ya watu watatu wenye mizinga makundi 50,000 na anamashamba 318 ambapo alisema mpaka ifikapo mwaka 2021 anataka kuwa na mizinga 20,000 na kuwa mfugaji wa nyuki namba moja duniani.

WASTAAFU WASHAURIWA KUFUGA SAMAKI


 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi (kulia) akizungumza alipotembelea banda la ufugaji wa samaki katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Singida. Wa pili kulia ni Mzee Juma Ibrahim Mkhofoi mfugaji mkubwa wa samaki mkoani Singida.
 Wafanyakazi wa Mzee Juma Mkhofoi wakiyafanyia usafi mabwawa ya ufugaji wa samaki yanayomilikiwa na mzee huyo.


Mzee Mkhofoi (kulia) akiwa katika banda la kufugia samaki kwenye maonesho hayo. Samaki hao wametoka katika moja ya mabwawa yake.
Mfugaji Mzee Mkhofoi akiangalia kibao cha tarehe aliyopandikiza vifaranga vya samaki katika bwawa hilo.
Mzee Juma Ibrahim Mkhofoi (wa pili kulia) akielekeza wananchi jinsi ya ufugaji samaki katika maonesho hayo.

 Hapa akiwapa samaki chakula.
 Mzee Mkhofoi akitoka kwenye ofisi ya mda iliyopo kwenye mabwawa yake ya samaki.
 Usafi kwenye mabwawa hayo ukiendelea.
 Usafi kwenye mabwawa hayo ukiendelea.Na Dotto Mwaibale, Singida

WASTAAFU wameshauriwa kufuga samaki ili waweze kupata chakula chenye lishe bora na kuinuka kiuchumi badala ya kutegemea fedha za kiinua mgongo pekee.

Wito huo umetolewa na Juma  Ikhofoi mfugaji mkubwa wa samani  mkoani Singida wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika Uwanja wa Bombadia mjini hapa.

" Niwaombe wastaafu wenzangu wasikae bure na kutegemea kiinua mgongo pekee kuendesha maisha yao bali wafuge samaki kwani watapata kitoweo chenye lishe bora na fedha za kujikimu  " alisema Mkhofoi.

Mkhofoi alisema gharama za ufugaji wa samaki ni ndogo  na soko lake ni kubwa tofauti na kilimo ambacho kinahitaji mambo mengi.

Aliongeza kuwa mabwawa ya samaki yanaweza kuchimbwa eneo lolote na chakula chao ni pumba ya mpunga na mahindi ambayo haizidi sh. 5000 kwa gunia na udavi ni sh.250,000 ambapo 
samaki kwa bwawa moja kwa siku wanakula kilo moja tu.

Alisema yeye baada ya kustaafu Wizara ya Maji na Umwagiliaji aliamua kuchimba mabwawa 67 kwa ajili ya kufuga samaki ambapo kila bwawa alitumia sh. milioni moja na sasa anafurahia 
ufugaji huo.

Alisema mabwawa hayo aliyachimba mwaka jana na sasa ameanza kupata matunda ya ufugaji huo kwani kuanzia mwaka jana mwishoni hadi mwaka huu mwanzoni ameweza kupata zaidi ya 
sh.milioni sita baada ya kuvua samaki  na kuwauza.

" Nimeanza kupata pesa kwa kuwauza samaki aina ya sato ninaowafuga pamoja na kitoweo chenye lishe ambacho kinakubalika kwa afya tofauti na nyama zingine " alisema Mkhofoi.

Mkhofoi alisema lengo lake ni kuwa na mabwawa zaidi ya 80 na kila wiki awe ana zalisha kilo kuanzia 1000 hadi 2000 na kuwa soko lake kubwa litakuwa hapa hapa mkoani Singida na 
hapendi kuwauzia wafanyabiashara kwa kuwa wanaenda kuwalangua walaji ambao watashindwa kupata chakula chenye lishe bora.

Mkhofoi ametumia fursa hiyo ya maonesho hayo kuwaomba wananchi wa mkoa wa Singida ambao watahitaji kupata mbegu ya samaki hao kwa ajili ya kufuga na kwa  kitoweo  kwa ajili ya 
matumizi ya nyumbani wawasiliane naye kwa namba ya simu 0755 735441 na 0655 735441.

WAZIRI MPINA ASHIRIKI ZOEZI LA KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KIJIJINI ISANGIJO WILAYANI MEATU MKOANI SIMIYU NA KUSISITIZA UMUHIMU WA UCHAGUZI

 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akijiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. Kulia ni Afisa Mwandikishaji Sospeter Mseya.(13. 10.2019)
 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akiwa kwenye mstari kwa ajili ya kuingia kwenye kituo cha kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. .(13. 10.2019)
 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akisalimiana na Waasisi wa Chama cha TANU muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. .(13. 10.2019
 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. Kushoto ni Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Maswa, Constantine Sement Shillingi  (13. 10.2019)
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akisisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi bora watakaoweza kusimamia mipango ya Serikali kwenye vitongoji na vijiji muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu (13. 10.2019)


Magazeti ya leo Jumatatu Oktoba 14 2019


                 
 

Sunday, 13 October 2019

TFFT YANOGESHA TUZO ZA WALIMU ARUSHANa Ferdinand Shayo,Arusha.

Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation For Tomorrow limefadhili tuzo za walimu jiji la Arusha ambazo zilizotelewa kwa kutambua na kuthamini mchango wa walimu wanaofaulisha wanafunzi vizuri kwa alama za juu katika shule za msingi na sekondari za jiji la Arusha.

TFFT imekua na utamaduni wa kutoa tuzo za walimu kila mwaka jijini Arusha ambapo mwaka huu imeamua kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo jiji la Arusha na shule binafsi katika kuhakikisha kuwa tuzo za walimu mwaka huu zinafanikiwa .

Meneja wa Programu ya Mafunzo kwa walimu katika shirika hilo Noah Kayanda amesema kuwa wamedhamini kipengele cha Tuzo ya Mwalimu Mahiri ikiwa ni moja kati ya njia ya kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya elimu na taifa kwa ujumla.

Noah amesema kuwa TFFT itaendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi ili waweze kuboresha mbinu za ufundishaji na ubunifu na kukuza ubora wa elimu.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro  aliyefika kutoa tuzo za Walimu amewapongeza wadau mbalimbali wa;liojitokeza kufanikisha tuzo za walimu wakiwemo TFFT ,Shule ya Lucky Vicent pamoja na wadau wengine kwani tuzo hizo zinalenga kuwatia moyo walimu.

DC Arusha Atoa Tuzo kwa Walimu Bora


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro ametoa tuzo kwa walimu bora wa shule za msingi na sekondari wa Wilaya ya Arusha mjini kwa kuweza kufaulisha wanafunzi katika alama za juu za ufaulu wa masomo mbalimbali hivyo kulifanya jiji hilo kufanya vyema katika matokeo ya kimkoa na taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Walimu  iliyofanyika katika viwanja vya Nane nane jijini Arusha na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Jiji la Arusha,shirika la The Foundation For Tomorrow ,Shule ya Lucy Vicent .ambapo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka walimu kuboresha mbinu za ufundishaji na kuwa wabunifu badala ya kufundisha kimazoea.

Gabriel amewataka walimu kujivunia kufaulisha wanafunzi katika alama za juu ikiwa ni pamoja na kujenga nidhamu miongoni mwa wanafunzi na walimu ambao ni walezi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr.Maulid Madeni amesema kuwa serikali inatambua mchango mkubwa wa walimu katika ujenzi wa taifa kwani walimu ni kada muhimu ambayo inashiriki katika kujenga taifa kwa kuzalisha wataalamu katika sekta mbalimbali.

Dokta Madeni ameeleza kushangazwa na risala ya walimu ambayo haikugusia mchango wa Mwalimu Nyerere katika kada ya Ualimu kwani alikua mwalimu na alifanya kada hiyo kuheshimika katika jamii ya Watanzania na ulimwenguni.

“Ndugu zangu Walimu katika awamu ya Tano Raisi John Pombe Magufuli amefanya mambo makubwa katika elimu ikiwemo kutoa elimu bure kwa watoto wa wa Tanzania na kuboresha miundombinu na mazingira bora ya kutoa elimu lakini hotuba ya walimu haijagusia hilo ni vyema kutambua mchango wa Raisi katika elimu” Alisema madeni

Katibu wa Chama cha Walimu jiji la Arusha (CWT) Abraham Kamwela akisoma risala ya Walimu amesema kuwa licha ya mafanikio waliyonayo bado wana changamoto mbalimbali ikiwemo madeni  ya mishahara,fedha za likizo pamoja na changamoto ya kukosa makazi ambapo wameliomba jiji la Arusha kuwapatia walimu viwanja kwa bei nafuu ili kuwawezesha walimu kujenga makazi yao na kujimudu kimaisha.

Polisi Arusha Yaimarisha Ulinzi siku 3 za Nyongeza za Kujiandikisha Daftari la Wapiga Kura.Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewaondoa wasiwasi wakazi wa jiji la Arusha na kuwataka wajitokeze kwa wingi kuijiandikisha katika daftari la wapigara kura la uchaguzi mdogo wa serikali za mtaa katika siku tatu ambazo serikali imeongeza hadi kufikia tarehe 17 octoba mwaka huu kwani jeshi hilo limeimarisha ulinzi na usalama wa kutosha kwa wananchi wote.

Akizungumza na wanahabari Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan  Shana amesema kuwa kufutia serikali kuongeza siku za kujiandikisha jukumu lao ni kuhakikisha usalama kwa wananchi wote kwani jeshi litafanya kazi bila kupendelea chama chochote cha siasa.

Shana amesema kuwa serikali inawajali wananchi wake na kuamua kuwaongezea siku za kujiandikisha ili waweze kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Kamanda huyo amesema kuwa jeshi hilo linafanya kazi kwa kuzingatia kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali katika kutekeleza wajibu wake wa msingi.

“Tunawaomba wakazi wa Arusha wajitokeze kwa wingi katika siku hizi zilizoongewa wajiandikishe kwa wingi na pia wajitokeze kupiga kura” Alisema Kamanda

ASILIMIA 15 YA MAPATO YA KOROGWE MINI MARATHON KUTUMIKA KUSAIDIA WAATHIRI WA MAFURIKO WILAYANI KOROGWE

MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Kisa Gwakisa katikati kikimbia pamoja na Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia wakikimbia mbio za kilomita 5 za Korogwe Mini Marathon zilizofanyika leo mjini Korogwe 
Wakimbiaji wa Baiskeli wakiwa wameanza mbio zao kwenye Mashindano ya Korogwe Mini Marathon 


Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kulia akikimbia kilomita 5 wakati wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon leo mjini Korogwe
Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akivalishwa medali na Mratibu wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon Juma Mwajasho mara baada ya kumaliza mbio za kilomita 5
Mratibu wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon Juma Mwajasho 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon kwa upande wa wanaume aliyekimbia kilomita 10 Jumanne Ndege kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Michael John ambaye ni Afisa Tarafa ya Korogwe
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akiendelea kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali mara baada ya kumalizika mashindano hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akiendelea kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali mara baada ya kumalizika mashindano hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Michael John ambaye ni Afisa Tarafa ya Korogwe 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon 
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza wakati wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon

 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kushoto akimpongeza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi 
 Sehemu ya wananchi wakifuatilia mbio hizo
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa katikati akiwa pamoja na washiriki wengine waliojitokeza kushiriki mashindano ya Korogwe Mini Marathon kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Timotheo Mzava
NA MWANDISHI WETU, KOROGWE

ASILIMIA 15 ya mapato yanayotokana na mashindano ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanatarajiwa kutumika kwenye kuwasaidia waathirika wa mafuriko wilayani Korogwe ambao wamekumbwa na majanga mbalimbali.

Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa wakati wa mashindano ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yaliyofanyika mjini Korogwe na kuhudhuriwa na washiriki kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Alisema maafa hayo ni makubwa kutokana na wamewaacha baadhi ya wananchi wakikosa makazi huku wengine wakipoteza maisha hivyo wameona watumie nafasi hiyo kuwafariji wananchi hao kwa kuwapatia kiasi hicho. 


“Ndugu zangu Korogwe tumekumbwa na maafa wenzetu wamepoteza maisha maji yamekata barabara kwa kutumia Mashindano hayo ya Korogwe Mini Marathon tutatoa asilimia 15 kuwasaidia ndugu zetu waliopata maafa na mvua hizo kuwapa mkono wa Pole kwa kuwa ni watanzania wenzetu”Alisema DC Kissa. 

Aidha alisema kwamba lengo kuu la mashindano hayo ni kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ikiwa leo ni mwaka 2019 anafikisha miaka 20 wao wana Korogwe tunatumia siku hii kwa kuenzi kwa kufanyika mashindano hayo”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba Korogwe wameungana na dunia nzima kumuenzi baba wa Taifa ambayo aliwaachia watanzania demokrasia ya vyama vingi kitu ambacho kinaendeleza kwa vitendo na Rais Dkt John Magufuli.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba lengo la pili ni kuchangia miundombinu ya elimu kupitia kampeni ya Nivushe kuhakikisha wanasukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sekta hiyo. 

“Lakini pia tunawashukuru Tanapa wametuchangia milioni 30, tunawashuiru marathon hii isingekamilika kama sio wadau hawa wameweza kudhamini huku mdhamini wa kwanza akiwa Tanapa, wa pili ni Gomba, wa cyclyn ...Lakini Tunawashuku pia NMB na CRDB tunategema kipindi kijacho tutakuwa na ongezeko la wadhamini “Alisema.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume waliokimbia kilomita 10 alikuwa ni Jumanne Ndege kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mkoani Arusha ambaye alikimbia dakika 30 na sekunde 7 ambaye alizawadiwa medali na kitita cha laki mbili.

Nafasi ya mshindi wa pili ilikwenda kwa Jackson Makombe ambaye alikimbia dakika 31 na sekunde 04 ambaye pia akitokea JKT Mkoani Arusha aliyepata kitita cha 140,000 huku mshindi wa tatu ikienda kwa Charles Sule ambaye alikimbia umbali wa dakika 32 na sekunde 07 ambaye pia alitokea JKt mkoani Arusha alizawadiwa kitita cha sh.80,000.

Kwa upande wa wanawake kilomita mshindi wa kwanza ilichukuliwa na Grace Jackson kutoka klabu ya JKT Mkoani Arusha ambaye alikimbia kwa kutumia dakika 35 na sekunde 51 ambaye alipata kitita cha sh.200,000,nafasi ya pili ikichukuliwa na Banuelia Bryson kutoka mkoani Kilimanjaro ambaye alikimbia dakika 41 na sekunde 16 aliyepata kitita cha sh.140,000,huku mshindi wa tatu ikichukuliwa na Pendo Pamba kutoka Klabu ya JKT ya Mkoani Arusha akikimbia kwa dakika 42 na sekunde 18 akizawadiwa kitita cha 80,000.

Hata hivyo kwa upande wa mbio za Baiskeli kilomita 30 wanaume mshindi wa kwanza aliibuka Boniface Saimoni kutoka mkoani Simiyu ambaye alikimbia dakika 49 na sekunde 59 na kupata kitita cha sh.200,000,huku mshindi wa pili ikichukuliwa na Mussa Makala aliyepata kitita cha sh.160,000,na mshindi wa tatu ikichukuliwa na Rashid Ally akizawadiwa kitita cha sh.120,000.

Kwa upande wa mbio baiskeli wanawake kilomita 20 mshindi wa kwanza ilichukuliwa na mshindi wa pili ni Anna Pimax huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo mgeni rasmi wa mashindano hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi alimpongeza Mkuu huyo wa wilaya kwa kubuni na kuanzisha mashindano hayo ambayo yamekuwa na tija kubwa. 

Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto ya mvua lakini mashindano hayo yamefana na kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi na wana michezo ambao walijotokeza kushuhudia mashindano hayo. “Lakini pia nipongeze kamati ya maandalizi kwa kufanikisha dhumuni hili kubwa ikiwa ni kumuenzi baba wa Taifa ambapo kesho ni kumbukizi yake lakini pia kutumia fursa hiyo kuhamamsisha wananchi kuajiandikisha”Alisema

Mwisho.

Waandishi wa Habari wahihitimu kozi fupi ya Habari za Mtandaoni.


Mwenyekiti wa TATO Willy Chambulo ambaye ndiye mgeni rasmi ,akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Habari Maalum kilichopo Ngaramtoni mkoani Arusha .
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani nArusha Cloud Gwandu akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika katika chuo cha Habari Maalum.

Wahitimu wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mwenyekiti wa TATO Willy Chambulo  wa pili kutoka kushoto waliosimama mbele pamoja na viongozi wa chuo cha uandishi wa habari na uongozi cha Habari Maalum Media.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Waandishi wa habari mkoani Arusha chini ya chama cha waandishi wa habari mkoani hapo( APC)Wamehitimu mafunzo ya muda mfupi ya uandaaji na utayarishaji na video na uzalishaji yaliyoandaliwa na chuo cha Habari Maalum Media lengo likiwa ni kuwajengea uwezo katika kuyatimiza majukumu yao ya kila siku.

Mafunzo hayo yamehusisha utayarishaji wa miradi,upigaji picha,uaandaaji wa picha ,kuhariri na uzalishaji wa vipindi mbalimbali vya mtandaoni sambamba na kurusha vipindi mbalimbali katika mitandao ya kijamii.

Astele Reuben Ndaluka ni Kaimu mkuu wa chuo hicho amesema kuwa waandishi wanaoyo nafasi pana katika kuielimisha jamii,kuihabarisha ,sambamba na kuijkosoa pale inapostahili kufanyiwa hivyo bila kuvunja sheria na taratibu za nchi.

Ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali kujitoa kwaajili nya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika nyanja tofauti ili waweze kwenda sambamba na  mabadiliko yaliyopo kwa sasa ya sayansi na teknolojia huku akiwaasa wahitimu hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kiuandishi.

 Willy Chambulo  ni Mwenyekiti wa TATO amewasisitiza  wahitimu wa mafunzo kuwa na matumizi sahihi ya elimu waliyoipata na kuahidi kuendelea kusaidia waandishi wa habari  watakao kuwa na utayari kupata mafunzo zaidi.

Aidha amewataka kuitumia vyema elimu waliyoipata  sambamba na kuigeuza kuwa pesa ili ilete manufaa kwa jamii na kuepuka kuwa tegemezi

Cloud Gwandu ni mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Arusha ,ameishukuru TATO kwa kufadhili mafunzo hayo ya kozi fupi kwa waandishi hao, na kuahidi kuwa mafunzo hayo hayataishia darasani ,bali watayaweka kwenye vitendo zaidi ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Gwandu amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu,ambapo kundi lingine la waandishi wa habari litapata mafunzo hayo baadae mwezi huu ,lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuwa na weledi katika kutaarisha kuandaa habari mbalimbali ya matukio katika jamii kwenye mitandao ya kijamii

Amesema waandishi wa habari wanayo nafasi pana ya kwa kutumia mitandao ya kijamii ,kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya utalii ,haswa kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivituo mbalimbali vilivyo nchini.

Mwisho