Huu ni ugojwa ambao husababishwa na bakteria aitwaye Entamoeba Histolytica ambaye huishi katika kinyesi cha mwanadamu.

NJIA ZA KUPATA

kula matunda bila kuosha
kutokunawa mikono baada ya kutoka chooni
kula chakula bila kuosha mikono
kunywa maji yasiyochemshwa


WATU AMBAO WAPO HATARI KUPATA HAYA MARADHI NI;

Wasafiri
Mashoga
Wanafunzi
wafanya biashara sokoni
Huanza kupata maradhi pale ambapo unakunywa au kula kitu ambambo kimechanganyika na hawa bacteria kisha wanaenda katika utumbo mdogo wanazaliana kuwa mwengi baadaye wanashuka katika utumbo mkubwa na kuanza kushambulia mwili. wakikua huishi katika kinyesi cha binadamu kisha hutolewa kwa njia ya haja kubwa na kuishi katika artdhi kwa muda wa wiki nne.

DALILI ZAKE

Tumbo kuuma kwa chini
kuharisha choo kilichochanganyika na kitu kama kamasi na wakati mwingine damu
kupungua uzito
homa

MATIBABU

Metronidazole, Tinidazole hizi ni ant biotics ambazo hutumika kuuwa hawa wadudu
Kuwekewa drips kama mtu ameharisha sana ili kuhakikisha anapata maji na madini aliyopoteza
Endapo Utapata dalili hizi ni vyema kufika hospitali ili ufanyiwe vipimo vya choo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: