Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imeendelea na yake ziara Mkoani Kilimanjaro.

Maafisa wa Mamlaka walipata fursa ya kutembelea Mahabusu ya watoto iliyopo katika Manispaa na Moshi na kutoa Elimu juu ya Madhara ya matumizi ya Dawa za kulevya katika kituo hicho.

Pamoja na hilo Maafisa kutoka Mamlaka Kanda ya Kaskazini imetembelea Asasi za kiraia zinazofanya Kazi na Vijana, hii ni katika kuziibua ili ziweze kutoa Elimu juu ya Tatizo la dawa za kulevya kwa kundi hilo.

Sambamba na Hilo Maafisa walitembelea Nyumba za Upataji nafuu na kukagua taratibu na kuishi na Waraibu kama zinatekelezwa pamoja na kuongea na Waraibu wanaopata huduma kwenye nyumba hizo.

Aidha, Maafisa Waliungana na Afisa kutoka TAKUKURU kwenda kutoa Elimu katika Chuo cha Mwenye Catholic University ili kuhamasisha Klabu za Rushwa na Dawa za Kulevya zinapata mwamko na wanafunzi kujiunga pamoja.

Pamoja na Hilo Maafisa walipata fursa ya kutembelea Ofisi za TAKUKURU KILIMANJARO na kukutana na Mkuu wa TAKUKURU Kilimanjaro ambae amesisitiza kushirikiana zaidi katika kutoa Elimu kwa jamii.

Share To:

Post A Comment: