Articles by "KIHONGOSI"
Showing posts with label KIHONGOSI. Show all posts

 


Wananchi wa Mkoa wa Arusha leo Jumamosi Agosti 23, 2025 wamejumuika pamoja kushiriki kwenye Mbio za Jogging pamoja na mazoezi ya Viungo, ikiwa ni siku ya  Kilele cha Tukio la Tanzania Samia Connect, linalofanyika Mkoani Arusha kuelezea mafanikio yaliyopatikana Mkoani Arusha katika Kipindi cha Miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Jogging hiyo ilianzia kwenye uwanja wa Mgambo, Uzunguni Jijini Arusha Tukio hilo limeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenani Laban Kihongosi, huku pia wananchi wakiendelea kupata huduma mbalimbali ikiwemo matibabu bure na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa na Vitambulisho vya Taifa.











MKUU wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi ametoa siku tatu kwa maofisa Usafirishaji (bodaboda) kutoa milio inayoshtua watu kwenye pikipiki zao

Kenani alitoa agizo hilo jana Jijini Arusha wakati akiongea na waendesha bodaboda na bajaji wa Mkoa wa Arusha na kusisitiza sekta hiyo ni muhimu endapo itatumiwa kwa nidhamu. 

Alisema milio hiyo inaleta kero kwa jamii na kuwasihi waenda bodaboda hao kuacha tabia ya kubeba bangi kupitia vyombo hivyo na kuhatarisha usalama wao 

"Tatu mzuka mnaoiba hela au vitu vya watu acheni na wale wenye pikipiki zenye milio nawapa siku tatu acheni tutachukua hatua za kisheria"

Aliongeza kuwa Arusha haitakuwa sehemu salama kwa watu wenye bodaboda kuiba 

Hakimu Msemo Katibu wa Maofisa Usafirishaji Mkoa wa Arusha, alisema wanatamani kila dereva wa bodaboda awe anatambulika kwenye mfumo wa kidigitali ambapo jumla ya wanachama 8,000 wamesajiliwa na kujulikana kwa haraka endapo amepata changamoto ikiwemo sare

Alisema umoja huo umeimarisha uongozi kwa kata 25 ikiwemo usajili huo kati ya vituo 511 vilivyopo Jijini hapa ambapo mfumo huo unaweza kuwa na wanachama zaidi ya 200,000 lakini pia wanandoto ya kuanzisha ushirika ambapo mpaka sasa wanajumla ya sh, milioni 23 ambazo zipo ndani ya ushirika wao unaotarajia kuanza

Alisema sh, milioni 10 walipewa na Rais Samia Hassan Suluhu, ambapo kwasasa wanaunganisha wanachama na taasisi mbalimbali ikiwemo kushirikiana na jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.

" Wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ofisi katika wilaya mbalimbali ikiwemo vijana wengi kutokuwa na elimu ya usalama barabarani na  wengine kupata ajali kutokana na kukosa leseni"

Waliomba kuongezewa vituo vingi zaidi ili waweze kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuangaliwa maeneo mengine ya kutoa huduma hizo ya Ngusero, Lemara, Kijenge Juu.



















MKUU wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi amepiga marufuku "faini ya funguo"utozwaji ya sh, 30,000 inayotozwa baada ya mmiliki wa eneo husika kushindwa kulipa kodi mbalimbali ikiwemo kodi ya leseni na kodi ya huduma, zinazotozwa  na halmashauri ya Jiji la Arusha kutokana na wafanyabiashara hao, kushindwa kulipa kodi hizo kwa wakati. 

Rc Kihongosi amepiga marufuku hiyo wakati akizungumza na wamiliki,wafanyakazi na watumishi Jiji hilo ili kubaini changamoto zao na kutafuta majibu sahihi ikiwemo utunzaji wa amani ikiwemo usafi wa maeneo wanayofanyia kazi. 

Amesema watakaothibitika kuchukua sh, 30,000 za faini za funguo kwa watumishi wa idara ya biashara kumi na moja waliopo Jiji la Arusha watachukuliwa hatua za kisheria kwani huo ni ukandamizaji kwa wananchi hao ambao wanaendesha maisha kupitia saluni wanazofanya kazi. 

"Hii faini ya funguo haikubaliki sasa ukifunga saluni na kudai hela hizo kwa mwezi ni shilingi ngapi tutachukua hatua na lakini naagiza Jiji la Arusha kutenga maeneo ya wafanyakazi wa saluni ili kuhakikisha kila mmoja anapata riziki badala ya kugombana"

Alisema watu wa saluni ni kada nzuri yenye wateja wengi hivyo wanapoona kunahabari tofauti za wateja wao watoe taarifa kwa serikali ili hatua ziweze kuchukuliwa na kusisitiza kulinda amani kwa kutoa viashiria ambavyo havijakaa sawa kwani amani ya nchi ni tunu pekee. 

Alisisitiza waajiri wa saluni kutoa mikataba ya ajira huku akisema Jiji la Arusha lina shilingi bilioni 5.5 kwaajili ya utoaji mikopo ya asilimia kumi inayotolewa serikali kwa vijana, wanawake na makundi maalum kwaajili ya kupata mikopo hiyo ili wajikwamue kiuchumi ambapo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, John Kayombo alisisitiza elimi hiyo kuendelea kutolewa ili watu mbalimbali waweze kupata mikopo

Awali baadhi ya wafanyakazi na wamiliki wa saluni akiwemo  Rose John mwenye kibanda namba 133 eneo la stendi ndogo aliweza kupewa umiliki halali wa kibanda chake baada ya awali kuzunguushwa na aliyekuwa mmiliki wa eneo hilo na kumpa notisi ya kuhama ilhali alikuwa akilipa kodi halali ya eneo alilopangishwa kwa mmiliki wake. 

Pia Thedy Mchome aliomba suala la upimaji afya kwa wafanyakazi lichukuliwe kwa uzito wake na wanapotaka kulipa fedha za wafanyakazi kwaajili ya upimaji wapewe controo namba kwa wakati ili waondokane na usumbufu na kuomba kodi wanazotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuhakikisha zinaendana na uhalisia wa biashara zao wanazofanya







 Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kufanikiwa kupunguza vifo vya mama wajawazito na vifo vya mama na mtoto hali iliyochagizwa na kuanzishwa kwa Mfumo wa Rufaa wa M-Mama, uliosaidia wakinamama kujifungulia kwenye Vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kenani Kihongosi akizungumza na Watanzania kupitia mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika mkoa huo leo Julai 20, 2025 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dodoma.

“Vifo vya kinamama wajawazito vimepungua kwa asilimia 78 kutoka vifo 50 (2021) hadi vifo 11 (2025). Vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 859 (2021) hadi 117 (2025),” alieleza.

RC Kihongosi amesema Vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka vituo 249 hadi vituo 350, sawa na asilimia 71.14.

Aidha, Hospitali mpya nane zimejengwa na kufanya jumla ya Hospitali kuwa 21 zikiwa na majengo ya kutolea huduma za dharura na vituo vipya vya afya 8 vimejengwa na kuufanya mkoa kuwa na vituo 66 na Zahanati mpya 38 zimejengwa na kuufanya mkoa kuwa na jumla ya Zahanati 350.

Kihongosi amesema, “kumekuwepo na upatikanaji wa huduma za kibingwa mpya 11 zilizoanzishwa ikiwemo; upasuaji, pua, koo na masikio, mifupa, magonjwa ya figo, magonjwa ya ngozi, uchunguzi wa magonjwa ya saratani, magonjwa ya uzazi na mtoto, magonjwa ya afya ya kisayansi, magonjwa ya ndani, watoto na mfumo wa mkojo.”

Aidha hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi imeongezeka kufikia asilimia 93 (2025) kutoka asilimia 65 (2021). Vile vile, mashine za kisasa zimesimikwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mount Meru, ikiwemo: CT-Scan, ECHO, ECG na MAMOGRAPHY.

Ameongeza kusema jumla ya watumishi 1,403 wameajiriwa na kufanya idadi ya watumishi wa afya kufikia watumishi 3,542 sawa na ongezeko la asilimia 66. Nyumba 105 za watumishi wa sekta ya afya zimeongezeka na kufikia nyumba 423, sawa ongezeko la asilimia 33.

RC Kihongosi amesema. “magari 14 ya huduma za dharura, magari tisa kwa ajili Timu za Uendeshaji Mkoa (RHMT) na Halmashauri (CHMT) pamoja na gari moja la huduma M-mkoba yamenunuliwa kwa ajili ya shughuli za usimamizi wa huduma za afya.”


Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Kenani Kihongosi ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha amekabidhi rasmi ofisi kwa mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anamringi Macha.

Tukio la makabidhiano  ya Ofisi limefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliyoko katika Mji wa Kiserikali Nyaumata Wilayani Bariadi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi Ofisi hiyo Mhe.Kihongosi amewashukuru Viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoani Simiyu kwa ushirikiano mkubwa waliompatia katika kipindi chote alichohudumu kama Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Aidha Mhe.Kihongosi amemshukuru Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu  Bi.Prisca Kayombo pamoja na Sekretarieti yake kwa ushirikiano mkubwa waliompatia kipindi chote akiwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Amemhakikishia Mkuu wa mkoa mpya Mhe.Anamringi Macha kuwa Mkoa uko katika hali ya utulivu na kwamba viongozi na Watendaji wa Mkoa ni wachapa kazi wazuri.

Amewahimiza Viongozi na watendaji wa Serikali Mkoani humo kumpatia ushirikiano wa kutosha Mhe.Macha ili mkoa uweze kupiga hatua zaidi kimaendeleo.

Kwa upande wake Mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anamringi Macha amewapongeza watumishi kwa kushirikiana vyema na aliyekuwa mkuu wa Mkoa huo ambapo amewataka kumpatia ushirikiano zaidi ili kuendeleza kazi nzuri zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Makabidhiano ya ofisi kwa wakuu hao wawili yanafuatiwa na mabadiliko ya uongozi yaliyofanywa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo katika mabadiliko hayo  aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Laban Kihongosi amehamishiwa Mkoani Arusha na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuhamishiwa Mkoani Simiyu.







Oparesheni maalumu ya kuwadhibiti wanyamapori wakali na waharibifu aina ya fisi waliokuwa wanaleta taharuki na madhara Kwa jamii inayoendelea Mkoani Simiyu imeonesha mafanikio makubwa baada ya fisi 16 kuvunwa ikiwa ni hatua muhimu iliyochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuhakikisha usalama na utulivu Kwa wananchi vinarejea.

Hayo yamesemwa leo Februari 19, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi alipokuwa akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

Mhe. Kihongosi amesema kufuatia changamoto hiyo,  Serikali ilichukua jukumu kubwa la kuhakikisha inalinda wananchi wake ikiwemo kuanzisha oparesheni maalumu inayohusisha Jeshi la Uhifadhi Kwa Taasisi za TAWA, TANAPA na TFS Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na wananchi, oparesheni inayotajwa kuanza  Januari 25, 2025.

"Tarehe 20/12/2024 baada ya fisi kuvamia wananchi Serikali ilichukua hatua kubwa ya kushirikisha vyombo vyake (TAWA na Jeshi la Polisi) na kuanza Oparesheni, lakini ilipofika tarehe 25/01/2025 oparesheni ya mkoa mzima ilifanyika Kwa ukubwa kuhakikisha inakabiliana na fisi wote waliokuwa wanasumbua wananchi" amesema Mhe. Kihongosi 

"Na Kwa taarifa njema ni kwamba tangu kuanza Kwa oparesheni hii vyombo vyetu vimeweza kudhibiti na kuua fisi 16 na ndio maana kwasasa mnaweza kuona hali imetulia" ameongeza Mkuu huyo wa mkoa wa Simiyu.

Aidha Mhe. Kihongosi ameendelea kuwatoa hofu wananchi wa mkoa huo akisisitiza kuwa hali ni shwari na kuwataka waendelee na shughuli zao kama kawaida huku akikemea vikali imani za kishirikina kuhusiana na mnyamapori aina ya fisi kwa baadhi ya wakazi wa Simiyu na kuwataka wote wanaofuga wanyamapori pori hao kuacha mara moja kwani ni kosa kisheria kumiliki nyara za Serikali bila Kibali.

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja amewaomba wananchi wa Mkoa wa Simiyu hususani wilaya ya Itilima kuacha tabia ya kutembea  nyakati za usiku na alfajiri kwani ni nyakati ambazo wanyama fisi huwa katika mawindo yao.

Vilevile amewasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Maofisa wa Jeshi la Uhifadhi waliopo uwandani ili kuongeza ufanisi wa zoezi hilo huku akiwahakikishia  kuwa Serikali imedhamiria kulinda wananchi wake na kwamba Askari wapo uwandani wanafanya Kazi usiku na mchana kuwahakikishia usalama wao.

Kwa upande wao wananchi wa Simiyu hususani wilaya ya Itilima wameshukuru Kwa juhudi zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo, wakisema kuwa hatua hiyo imeweza kuwarejeshea matumaini, utulivu na amani.

"Kwakweli tulikuwa tunasumbuliwa sana na haya mafisi ambayo yalikuwa yanauma watu, baada ya Serikali kusikia ikaweka ulinzi, kwakweli imetufanyia vizuri sana mpaka leo hatujawasikia tena tangu Askari waanze kuwashambulia hao fisi, mpaka leo hii tuna utulivu sana kwakweli tunashukuru sana"   amesema Mozo Mabula  mkazi wa Kijiji cha Mwamunhu kilichopo wilaya ya Itilima.

 MKUU wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi ameshiriki katika matembezi ya kuunga mkono azimio la Chama cha Mapinduzi (CCM) ambalo limemteua Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.


Akizungumza mara baada ya matembezi hayo yaliyofanyika Mjini Bariadi Kihongosi amesema wao kama Simiyu wanaunga mkono azimio hilo lililompitisha Dkt Samia na mgombea mwenza wake Dkt Emanuel Nchimbi ili wakaendelee na kazi walioianza.

Akifafanua Mkuu huyo wa Mkoa amesema, maendeleo yaliyopatikana sasa hayafanani na yale ya miaka minne iliyopita ikiwemo ukamilishwaji wa mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere unaogharimu Trilioini 6.5.

“Kabla Rais Samia hajaingia madarakani reli ya kisasa ya SGR inayogharimu trilioni 7.2 ilikuwa haijakamilika na sasa imeanza kazi kwa kipoande cha Dar es Salaam hadi Dodoma, huko mkoani Mwanza ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi maarufu Daraja la Magufuli unaogharimu Sh.bilioni 700 umefikia asilimia 96,” amesema Kihongosi.

Amebainisha hakuna sababu za MwanaCCM yeyote kuogopa wala kuhofia kwa sababu utekelezaji wa Ilani ya umekamilika kwa asilimia kubwa ikiwemo ujenzi wa Shule ya Wasichana Bariadi Kusini, kujengwa kwa shule ya Wavulana Simiyu Boys, na kwa kuwa mkutano mkuu umeshaamua mtu yeyote mwenye nia ya kuwania urais shughuli imeisha na atakayemtweza Daktari Samia Suluhu Hassan CCM itashughulika nae.




 MKUU wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi amewaeleza wananchi katika ziara yake ya kijiji kwa kijiji kuwa Mkoa huo unaendelea kupokea fedha kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa awamu katika kutekeleza mradi mkubwa wa maji unaogharimu Shilingi Bilioni 440 kutoka Serikali kuu.


Utakapokamilika mradi ambao utamaliza changamoto ya maji katika mkoa Mzima wa Simiyu na hivyo wananchi kuwa na uhakika wa maji safi na salama.

Mkuu wa Mkoa Kihongosi ameyasema hayo akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kijiji kwa kijiji ili kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi zinazowakabili.

Akieleza zaidi Kihongosi amesema tayari utekelezaji wa mradi huo wa maji umeanza kwa kasi kubwa na chanzo cha maji hayo kimejengwa Wilaya ya Busega na matanki mengine yanajengwa Wilaya za Bariadi na Itilima ambayo mengine yameshakamilika.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa ili azma hiyo ikamilike amewataka wananchi wa mkoa huo kudumisha amani, upendo na mshikamano kwani kama jamii italinda amani basi imelinda taifa na atakayechochea vurugu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

 MKUU wa Mkoa wa Simiyu Mkuu Kenani Kihongosi amesema Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi wote kwenda kuwatumikia wananchi katika maeneo ambayo wamekabidhiwa dhamana hiyo.


Akizungumza leo Januari 9,2025 wakati anaanza ziara katika vijiji vya Nyamikoma, Mwandama, Sapiwi, Igegu Magharibi,Igegu Mashariki, Igegu, Isenge, Mwamabu, Igagalulwa, Sengerema na Majengo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kihongosi amesema yeye yuko tayari kwenda katika vijiji kusikiliza changamoto za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi.

“Sasa mimi niko tayari kuanzia leo kuja katika vijiji vyenu kusikiliza changamoto zinazowakabili maana kupitia nyie Wananzengo ndipo tunapoibua matatizo mbalimbali, kero zinazowakabili huku ikisaidia pia kujua wapi pana shida ikiwemo ukosefu wa huduma muhimu kama umeme, maji, afya, elimu, ukosefu wa pembejeo na hata miundombinu korofi ya barabara.”

Amesisitiza kwamba maendeleo ya watu katika mikoa, wilaya, Vijiji na hata vitongoji, yanachagizwa na viongozi kwenda katika maeneo mbalimbali kuzungumza na wananchi na kwa kuliona hilo ndio maana ameanza ziara ya siku 30 kwenda kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi katika vijiji vyote vya mkoa wa Simiyu.