MKUU wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi ametoa siku tatu kwa maofisa Usafirishaji (bodaboda) kutoa milio inayoshtua watu kwenye pikipiki zao

Kenani alitoa agizo hilo jana Jijini Arusha wakati akiongea na waendesha bodaboda na bajaji wa Mkoa wa Arusha na kusisitiza sekta hiyo ni muhimu endapo itatumiwa kwa nidhamu. 

Alisema milio hiyo inaleta kero kwa jamii na kuwasihi waenda bodaboda hao kuacha tabia ya kubeba bangi kupitia vyombo hivyo na kuhatarisha usalama wao 

"Tatu mzuka mnaoiba hela au vitu vya watu acheni na wale wenye pikipiki zenye milio nawapa siku tatu acheni tutachukua hatua za kisheria"

Aliongeza kuwa Arusha haitakuwa sehemu salama kwa watu wenye bodaboda kuiba 

Hakimu Msemo Katibu wa Maofisa Usafirishaji Mkoa wa Arusha, alisema wanatamani kila dereva wa bodaboda awe anatambulika kwenye mfumo wa kidigitali ambapo jumla ya wanachama 8,000 wamesajiliwa na kujulikana kwa haraka endapo amepata changamoto ikiwemo sare

Alisema umoja huo umeimarisha uongozi kwa kata 25 ikiwemo usajili huo kati ya vituo 511 vilivyopo Jijini hapa ambapo mfumo huo unaweza kuwa na wanachama zaidi ya 200,000 lakini pia wanandoto ya kuanzisha ushirika ambapo mpaka sasa wanajumla ya sh, milioni 23 ambazo zipo ndani ya ushirika wao unaotarajia kuanza

Alisema sh, milioni 10 walipewa na Rais Samia Hassan Suluhu, ambapo kwasasa wanaunganisha wanachama na taasisi mbalimbali ikiwemo kushirikiana na jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.

" Wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ofisi katika wilaya mbalimbali ikiwemo vijana wengi kutokuwa na elimu ya usalama barabarani na  wengine kupata ajali kutokana na kukosa leseni"

Waliomba kuongezewa vituo vingi zaidi ili waweze kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuangaliwa maeneo mengine ya kutoa huduma hizo ya Ngusero, Lemara, Kijenge Juu.


















Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: