Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Kenani Kihongosi ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha amekabidhi rasmi ofisi kwa mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anamringi Macha.
Tukio la makabidhiano ya Ofisi limefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliyoko katika Mji wa Kiserikali Nyaumata Wilayani Bariadi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi Ofisi hiyo Mhe.Kihongosi amewashukuru Viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoani Simiyu kwa ushirikiano mkubwa waliompatia katika kipindi chote alichohudumu kama Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Aidha Mhe.Kihongosi amemshukuru Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Kayombo pamoja na Sekretarieti yake kwa ushirikiano mkubwa waliompatia kipindi chote akiwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Amemhakikishia Mkuu wa mkoa mpya Mhe.Anamringi Macha kuwa Mkoa uko katika hali ya utulivu na kwamba viongozi na Watendaji wa Mkoa ni wachapa kazi wazuri.
Amewahimiza Viongozi na watendaji wa Serikali Mkoani humo kumpatia ushirikiano wa kutosha Mhe.Macha ili mkoa uweze kupiga hatua zaidi kimaendeleo.
Kwa upande wake Mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anamringi Macha amewapongeza watumishi kwa kushirikiana vyema na aliyekuwa mkuu wa Mkoa huo ambapo amewataka kumpatia ushirikiano zaidi ili kuendeleza kazi nzuri zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Makabidhiano ya ofisi kwa wakuu hao wawili yanafuatiwa na mabadiliko ya uongozi yaliyofanywa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo katika mabadiliko hayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Laban Kihongosi amehamishiwa Mkoani Arusha na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuhamishiwa Mkoani Simiyu.
Post A Comment: