Wananchi wa Mkoa wa Arusha leo Jumamosi Agosti 23, 2025 wamejumuika pamoja kushiriki kwenye Mbio za Jogging pamoja na mazoezi ya Viungo, ikiwa ni siku ya Kilele cha Tukio la Tanzania Samia Connect, linalofanyika Mkoani Arusha kuelezea mafanikio yaliyopatikana Mkoani Arusha katika Kipindi cha Miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Jogging hiyo ilianzia kwenye uwanja wa Mgambo, Uzunguni Jijini Arusha Tukio hilo limeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenani Laban Kihongosi, huku pia wananchi wakiendelea kupata huduma mbalimbali ikiwemo matibabu bure na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa na Vitambulisho vya Taifa.
Post A Comment: