Articles by "BREAKING NEWS"
Showing posts with label BREAKING NEWS. Show all posts


Chama cha Mapinduzi, kimepokea kwa mstuko mkubwa taarifa za kifo cha Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, Bi Christina Kibiki aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiyojulikana.


 


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru watuhumiwa wote 24 katika kesi ya jinai inayohusu mauaji ya askari Koplo Ganus Mwita. Tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Orlolosokwani Tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Juni 10, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mahakani hapo leo, Mkurugenzi wa Mashtaka ameiandikia Mahakama kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kesi hiyo inajumuisha viongozi wa chama na serikali na ilianza kusikilizwa Mahakamani hapo Juni 16 kukiwa na watuhumiwa 27. Watuhumiwa watatu waliachiwa huru na kusalia watuhumiwa 24.



Ndege ya Precision Air imepata ajali katika Ziwa Victoria Bukoba, Kagera asubuhi hii ambapo Mashuhuda wanasema ajali hii imetokana na Ndege hiyo kupata hitilafu wakati ikitua,RPC Kagera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na wanaendelea na juhudi za uokozi.


Tunaomba radhi kwa tatizo la kutokuonekana kwa picha kwa Baadhi ya watumiaji wetu wa MsumbaNews Blog

Tatizo hili linatokana na Mifumo ya Google kubadilika na kusababisha Baadhi ya mitandao ya simu kushindwa kutoa Data zinazo weza kuonyesha Picha katika Blog yetu

Kwa watumiaji wa Voda na Tigo hawakukubwa na tatizo hili ila kwa watumiaji wa Halotel na Airtel ndio walikubwa na tatizo hili.

Ila kwa sasa tumeweza kufanikisha kutatua tatizo hilo kwa upande wa mitandao yote na Tatizo hili limekwisha


Kwa Maoni au maswali wasiliana nasisi kupitia namba hizi 0758767077 - 0762561399

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Dkt. Zainab Chaula akipokea kitabu cha Mkurugenzi wa Taasisi ya Azaria Foundation Audax Abeli kinachoelezea maisha yake ya mtaani  chenye lengo la kuisaidia Jamii kuwaondoa watoto katika mazingira hatarishi. Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Amon Mpanju na wajumbe wa Menejimenti ya Wizara mara baada ya kikao cha Menejimenti Jijini Dodoma 

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Dkt. Zainab Chaula akiongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara hiyo na Taasisi ya Azaria Foundation kujadili namna ya kuwaondoa watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani, kilichofanyika Jijini Dodoma 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Azaria Foundation Audax Abeli akieleza jambo wakati wa kikao ha Menejimenti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kujadili namna ya kuwaondoa watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani, kilichofanyika Jijini Dodoma tarehe 22 Agosti, 2022.

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imejipanga kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha inapunguza tatizo la Watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Akizungumza katika kikao naTaasisi ya Azaria Foundation jijini Dodoma Agosti 22, 2022 Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainab Chaula ameitaka jamii kuwa na upendo kati ya familia na kuhakikisha watoto wanatunzwa katika familia ili wapate Malezi na Makuzi Bora katika ukuaji wao.

Dkt. Chaula amesema pamoja na kuwa mwanzilishi wa Taasisi hiyo ni zao la watoto walioishi mazingira magumu baada ya kutelekezwa na familia yake amekuwa msaada kwa watoto wengine ili wasiendelee kuishi maisha hayo.

"Familia inaposhindwa kwa namna yoyote ile, sisi Jamii tuchukue wajibu na tuungane na Wadau hawa kutatua shida hii, Wizara tumejipanga kwa kushirikiana na Wadau kutumia mbinu zote" alisema Dkt Chaula

Naye Mkurugenzi na mwanzilishi wa Taasisi ya Azaria Foundation, Audax Abeli ambaye ameishi maisha ya mtaani amesema familia yake ilikuwa chanzo cha yeye kuitwa Mtoto wa mtaani jina ambalo siyo sahihi hivyo namna bora ya kuwatoa watoto hao mtaani ni kuanzia upendo kwao.

 "Hili tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani linatakiwa kushughulikiwa kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa, tunaweza tukapunguza watoto wa mtaani. Pia changamoto nyingine zinatokana na familia" alisema Audax.

Ameeleza kuwa mpaka sasa Taasisi hiyo inahudumia jumla ya watoto 70 kwa kuwapatia huduma muhimu za Kijamii na kuwapatia mbinu mbadala za kupambana na maisha.
 
Kwa upande wake Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Nandera Mhando amesema Wizara itashirikiana vyema na mdau wa Taasisi hiyo kwa kusaidiana na timu ya wataalamu inayofanya kazi ya kushughulikia watoto wanaoishi mazingira magumu na kuwatoa mtaani.

"Mojawapo ya mradi utakaozinduliwa hivi karibuni  ni mradi wa ujenzi wa kituo cha kupokea watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani na kuwapitisha katika mabadiliko ya tabia na ujuzi ili wanaporudi majumbani waweze kujiajiri" alisema Dkt. Nandera.

  


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo imeahirisha usikillizaji wa ushahidi wa shahidi namba saba upande wa Jamhuri wa kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021 ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili kutokana na Mshtakiwa namba Moja Lengai Ole Sabaya kutokufika mahakamani kutokana na sababu za kiafya.

Akiahirisha shauri Hilo Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo amesema shauri hilo litaendelea kusikilizwa tena hapo kesho Agosti 05 asubuhi kwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa shahidi namba saba Mratibu Msaidizi wa Polisi ASP Gwakisa Minga ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Arusha.

 

 


 

Waziri Mkuu Kaasim Majaliwa ameishukuru Benki ya Afrika (BOA) kwa jitihada zake za kuendelea kuisaidia Tanzania katika Sekta mbalimbali za maendeleo.

 

Ametoa kauli hiyo jana (Jumatano Julai 14, 2021) wakati alipozungumza na Rais wa benki hiyo Othman Benjelloun kwenye hoteli ya Sofitel, Rabat Nchini Morocco.

 

Amesema kuwa uwepo wa Benki hiyo nchini Tanzania umewawezesha wananchi kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo, "kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tunaishukuru Benki ya Afrika kwa jitihada hizi".

 

Aidha, Waziri Mkuu alimshauri Rais Benjelloun kuendelea kupanua wigo wa huduma za benki hiyo nchini ili kuwafikia watanzania wengi zaidi hasa katika sekta  za Elimu, Kilimo, Mifugo na Madini.

 

Waziri Mkuu aliahidi kuwa ataandaa utaratibu wa kuukutanisha uongozi wa Benki hiyo na sekta binafsi nchini Tanzania ili kuona namna watakavyoweza kushirikiana  katika kuwahudumia Watanzania.

 

Kwa upande wake, Rais Benjelloun amesema lengo la benki hiyo ni kuendelea kukuza uwekezaji wake  nchini Tanzania. "Sisi tupo tayari kuwekeza katika maeneo mbayo viongozi wa taifa la Tanzania watatushauri lengo likiwa ni kutoa mchango wetu katika kujenga uchumi". 

 

Naye, Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda alisema kuwa benki hiyo isaidie kukuza mahusiano ya Tanzania na Morocco katika sekta ya kilimo hasa kwenye mazao kama vile  Mchele, Tumbaku, kahawa na mazao mengine.

 

 Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Leila Muhamed Mussa amesema yapo maeneo ya fukwe ambayo hayajawekezwa mpaka sasa hivyo ni fursa kwa wawekezaji kuyatumia na kwamba  Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefungua milango kwa wawekezaji. 

 

Pia aliiomba benki hiyo kuona namna ya kuwawezesha wakulima wa viungo ili waweze kufanya shughuli zao kwa tija.


Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Sambaru wakati akiongoza harambee ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kipompo iliyofanyika Kata ya Mang'onyi wilayani Ikungi mkoani Singida jana.

 Diwani wa Kata ya Mang'onyi itakapojengwa shule hiyo, Innocent Makomero akizungumza kwenye harambee hiyo.
Watoto wa Kijiji cha Sambaru wakimpokea kwa mabango Mbunge Mtaturu wakiomba kujengewa shule katika kitongoji cha Kipompo.

Watoto wa Kijiji cha Sambaru wakimpokea  Mbunge Mtaturu.
Mkazi wa Kijiji cha Sambaru Hussein Dede, akimpokea  Mbunge Mtaturu.
Matofari ya ujenzi wa shule hiyo yakifyatuliwa kwa nguvu za wananchi.
Harambee ikiendelea.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Sambaru Samsoni Mwaigaga akizungumza kwenye harambee hiyo.
Wadau wa maendeleo ya elimu ambao ni wachimbaji wadogo wa madini wakitambulishwa  na Diwani wa Kata ya Mang'onyi itakapojengwa shule hiyo, Innocent Makomero (kulia) kwenye harambee hiyo.
Makofi yakipigwa kwenye harambee hiyo
 



Na Dotto Mwaibale, Singida



ZAIDI ya 23 milioni zimechangwa na wadau mbalimbali mkoani hapa kwa lengo la kupunguza adha ya watoto wa Shule ya Msingi ya Kipompo  iliyopo Kata ya Mang'onyi, Wilaya ya Ikungi  kutembea umbali mrefu wa takribani kilomita 15 kila siku kuwahi masomo.

Akiongoza harambee hiyo, Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ambaye kati ya fedha hizo alichangia 5 milioni alisema fedha zilizopatikana  zitatumika kwa ujenzi wa madarasa manne kwenye shule hiyo inayotarajiwa kuanza kujengwa kwenye kijiji cha Sambaru kwa nguvu ya wananchi. 

Hata hivyo, Mbunge Mtaturu alipongeza juhudi za makusudi katika nyanja mbalimbali za maendeleo hasa eneo la elimu  zinazofanywa na wananchi wa kijiji hicho ambacho kina vitongoji vitatu vya Kipompo, Mbugani na Mkunguu.

"Hapa ninapozungumza tayari wananchi hawa kwa nguvu zao  wamenunua mifuko ya saruji 210 kwa hatua za maandalizi ya ujenzi wa awali bila kusubiri serikali" alisema.

Mbali ya mchango huo zaidi Mtaturu aliwatia moyo wananchi hao kuendelea na mshikamano huo kwa kuhakikisha wanasonga mbele katika kufanikisha shabaha iliyopo ya ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa na nyumba ya mwalimu, huku akiahidi kuwawezesha kumalizia hatua ya kupaua.

Mtaturu alisema wametoka kwenye Bajeti ya Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambayo imelenga kuwaletea wananchi maendeleo. 

"Tunamshukuru sana Rais kwa kuonyesha upendo mkubwa kwa watanzania tumuunge mkono," alisema Mtaturu.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mang'onyi itakapojengwa shule hiyo, Innocent Makomero alisema kukosekana kwa shule kwenye Kijiji cha Kipompo kumeibua changamoto kadhaa ikiwemo kuzorotesha ustawi wa elimu sambamba na kuleta athari za saikolojia kwa watoto kutokana na kutembea umbali mrefu.

Alisema azma iliyopo ni kuhakikisha anaunga mkono juhudi za mbunge na wananchi katika kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa miundombinu hiyo ya elimu.

"Ili kufanikisha jambo hili nimewaalika wadau mbalimbali wa maendeleo ya elimu wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini kuja kutuunga mkono katika harambee yetu hii," alisema Makomero.

Mwanafunzi wa darasa la sita kwenye Shule ya Msingi Sambaru Nuru Ramadhan ambaye ni miongoni wa wahanga wa kutembea umbali mrefu akitokea kitongoji cha kipompo, alisema safari ya kutoka nyumbani alfajiri kwenda shuleni huwachukua kati ya masaa 3 hadi 4 kufika shuleni na hawajawahi kufanikiwa kuwahi vipindi vya asubuhi.

"Tunawashukuru wazazi wetu kwa uamuzi huu sababu kukamilika kwa shule hii kutasaidia  kupandisha ufaulu na kupunguza baadhi ya kero ikiwemo kushinda na njaa, na mafuriko kipindi cha mvua wakati tukiwa njiani kilomita 15 kila siku kwenda shule na kurudi." alisema.

Katika harambee hiyo jumla ya 23 milioni zilipatikana zikijumuisha fedha taslimu, ahadi na michango mingine ya hali na mali.


Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Timotheo Mnzava akiwa ameambatana na Mchumba wake Caroline Pallangyo ambaye ni Mtoto wa Mbunge waJimbo la Arumeru Mashariki John D Pallangyo.


Askofu Mkuu Dayosisi ya Meru Elias Nassary mapema hii leo amebariki Send-off ya Mtoto wa Mbunge Caroline John D Pallangyo na Mbunge wa Korogwe Vijijini Timotheo Mnzava na kuwataka wanandoa hao kudumishwa upendo kwani ndoa nyingi za Vijana wa siku hizi zimekuwa ni changamoto.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi {CCM} Dr. John D Pallangyo Amemsihi  Timotheo Mnzava pamoja na mwanaye anayeolewa na Mbunge huyo kwenda kuishi katika Ndoa takatifu yenye upendo wa kujali jamii inayowazunguka na kutambua kwamba maisha ya ndoa hujengwa kwa upendo na kujali jamii. 



PICHA MBALIMBALI KUTOKA KWENYE HAFLA HIYO.






Askofu Mkuu wa Jimbo la Arumeru Elias Nassary 








 

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amefafanua taarifa ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa hivi karibuni kuhusu kufunguliwa kwa vyombo vya habari vilivyofungiwa.

Msigwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ameelekeza Televisheni za Mtandaoni (Online Tv) tu ndio zifunguliwe na sio vyombo vya habari vingine yakiwemo Magazeti yaliyofungwa kwa mujibu wa Sheria.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.  Selemani Jafo amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta ya elimu na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli ndio siri iliyopelekea shule nane za serikali kuingia kwenye kumi bora katika matokeo ya kidato cha sita 2020.

Ameyasema hayo jana ofisini kwake Jijini Dodoma wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu ufaulu wa Shule za sekondari zinazomilikiwa na Serikali katika matokeo ya kidato ya sita.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano Serikali imeendelea kufanya vizuri katika Sekta ya Elimu ambapo kwenye matokeo yaliyotangazwa leo tarehe 21/08/2020  ufaulu umeongezeka kwa wanafunzi wa kidato cha sita kutoka  asilimia 98 kwa mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 99.51 kwa mwaka.

Amesema kuwa katika matokeo hayo shule za Serikali nane zimeweza kuingia katika  shule kumi bora kwa mara ya kwanza zikiwemo shule za kata 3 ambazo ni Kasimiri, Mwandeti na Dareda.

Amezitaja shule za Serikali zilizoshika nafasi kumi bora kuwa ni Mzumbe, Shule ya wasichana Tabora, shule ya wavulana Tabora, Iiliboru na  Kibaha

“Zamani ufaulu wa shule za Serikali ulikuwa mdogo  kiasi kwamba wazazi walikuwa hawapendi kuwapeleka watoto wao kusoma katika shule hizo wanapochaguliwa kujiunga na shule hizo, lakini sasa shule hizo zimekuwa na ufaulu mkubwa na kuwa tegemeo  kwa wazazi kuwapeleka watoto wao” amesema Waziri Jafo

Waziri Jafo anafafanua kuwa  uwekezaji uliofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli umeleta mabadiliko makubwa katika eneo la taaluma nchini

Aidha. Jafo amewashukuru waalimu, maafisa elimu Mikoa na Wilaya kwa usimamizi uliotukuka wa kuhakikisha  vijana wa kidato cha sita wanafaulu  vizuri na kuliongezea taifa sifa katika suala zima la sekta ya Elimu.

Amewapongeza Wanafunzi wote wa kidato cha Sita kwa kusoma kwa bidi na kupata ufaulu mzuri japokuwa kulikuwa na  changamoto ya ugonjwa wa CORONA nchi ya Tanzania bado waliweka juhudu katika masomo na kufaulu mitihani yao vizuri.

Waziri Jafo anaendelea kusema kuwa Serikali imetumia kiasi cha shilingi trilioni 1.09 katika suala zima la utoaji wa elimu bila malipo ambayo imehamasisha  sekta ya Elimu nchini,pia kiasi cha shilingi milioni 588 kwa ajili ya  ujenzi wa miundombinu  jambo hili limesaidia kuongeza idadi ya ufaulu wa wanafunzi.

Sambamba na hilo amesema kuwa Serikali imeweza kuongeza idadi ya waalimu  kwa lengo la kuongeza rasilimali ambao  watasaidia kupeleka elimu juu zaidi hali ambayo inapelekea kuongeza ufaulu zaidi nchini.

"Matokeo hayo yameonyesha pia wanafunzi waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ni asilimia 97.74, haya ni mafanikio makubwa,malengo yetu yalikuwa kuingiza shule sita za serikali kwenye kumi bora lakini tumeingiza shule nane,huu ni ufaulu uliozidi viwango" amesema Waziri Jafo.
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya Twiga Minerals Corporation umetoa msaada wa vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na kadi 450 za msamaha wa matibabu kwa wazee katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 8. 
Hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo imefanyika leo Jumatano Juni 24,2020 katika kijiji cha Bunango kata ya Bugarama ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha. 
Kaimu Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Senkondo amevitaja vifaa vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kuwa ni Fimbo nyeupe 5 kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa macho,magongo 5 na baiskeli 8 kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa miguu pamoja na kadi 450 za msamaha wa matibabu kwa wazee. 
Alisema kutolewa kwa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya jamii (Corporate social responsibility -CSR) unaotekelezwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu ambapo walikubaliana na Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwamba asilimia 10 ya fedha ya CSR kwa ajili ya makundi maalumu vikiwemo vikundi vya akina mama,vijana,wazee na watu wenye ulemavu. 
“Vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na wazee tulivyotoa vina thamani ya shilingi 8,050,000/= . Tunatoa shukrani kwa ushirikiano mzuri na viongozi wa ngazi zote katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya jamii hususani katika kuhudumia makundi maalumu.Tunaomba tuendelee kushirikiana kwa ajili ya kujenga jamii kwa maendeleo endelevu”,ameongeza Senkondo. 
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa walengwa, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha ameupongeza na kuushukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kufanikisha kupatikana kwa vifaa wezeshi kwa wazee na watu wenye ulemavu katika kata za Bugarama na Bulyanhulu. 
“Mgodi wa Barrick Bulyanhulu mmekuwa sehemu ya familia ya wakazi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala kutokana na ushirikiano ambao mmekuwa mkiutoa kwa jamii. Tunawashukuru kwa kuona umuhimu wa kuyafikia makundi maalumu ambayo kimsingi yanashiriki katika shughuli za maendeleo katika jamii”,amesema Macha. 
“Serikali itaendelea kushirikiana na mgodi wa Bulyanhulu na Taasisi mbalimbali katika kuyahudumia makundi maalumu kwani serikali inaamini kuwa binadamu wote ni sawa bila kujali huyu ana ulemavu au mzee.Tutaendelea kuhakikisha watu wote wanaishi kwa amani”,ameeleza. 
Mkuu huyo wa wilaya amesema vifaa hivyo wezeshi (baiskeli,fimbo nyeupe na magongo) vitawasaidia watu wenye ulemavu kuwapunguzia adha ambayo wamekuwa wakiipata katika utekelezaji wa shughuli zao za kijamii na kwamba kadi za msamaha wa matibabu zitawasaidia wazee hao 450 kupata huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya pindi wanapohitaji huduma za matibabu. 
“Naomba mkavitunze na mvitumie vizuri hivi vifaa. Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hakikisha katika vituo vya afya,zahanati kuna madirisha kwa ajili ya wazee na kama hakuna hayo madirisha basi hakikisheni wazee wanapewa kipaumbele na kupewa dawa na kila mmoja anayefika hospitali akaona kuna mzee awape nafasi kwanza wazee”,ameongeza Macha. 
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Dkt.Ntanwa Kilagwire Amesema mgodi wa Bulyanhulu kwa kushirikiana na halmashauri hiyo wamekuwa wakitekeleza mpango wa uwajibikaji kwa jamiiinayozunguka eneo la mgodi katika kata za Bugarama na Bulyanhulu ili kukuza na kuimarisha ustawi wa makundi mbalimbali ya kijamii yaliyopo katika maeneo hayo. 
“Katika utekelezaji wa Programu hii ya CSR kwa mwaka 2019/2020 kwenye afua ya vijana,wazee na watu wenye ulemavu,uongozi wa kata husika uliweka vipaumbele kwenye bajeti kusaidia makundi ya wazee na walemavu vyenye jumla ya shilingi 20,000,000/= inayotolewa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu”,amefafanua. 
Kwa upande wao, Salome Samweli, Abbas Salum na Praygod Museveni wameushukuru mgodi wa Bulyanhulu kwa kuwapatia watu wenye ulemavu baiskeli,fimbo nyeupe,magongo na kadi za msamaha wa matibabu kwa wazee na kuuomba mgodi huo na wadau wengine kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji katika jamii. 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imetangaza ajira zaidi ya 4,400 kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Akiwasilisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2020/21, Waziri wa wizara hiyo, George Simbachawene, alisema ajira hizo zitakwenda pamoja na mafunzo mbalimbali kwa askari na watumishi mbalimbali.

Alisema kwa mwaka huo, Jeshi la Polisi linatarajia kuajiri askari 2,725, askari Magereza 685, Uhamiaji 495 na Zimamoto 501.

Simbachawene alisema katika mwaka 2020/21 Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi limepanga kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa maafisa, wakaguzi na askari 9,465 pamoja na watumishi raia 25.

Alisema kati ya hao 9,051 watapata mafunzo ndani ya nchi kupitia vyuo vya polisi na 414 nje ya nchi kwa udhamini wa taasisi na nchi mbalimbali.

Aidha, alisema katika kuimarisha kuimarisha utendaji kazi wa watumishi wa Jeshi la Polisi jumla ya maofisa, wakaguzi, askari na watumishi raia 5,470 wamepata mafunzo mbalimbali, kati ya hao 5,461 walipata mafunzo ndani ya nchi na tisa nje ya nchi.

Kwa upande wa Jeshi la Magereza, alisema katika kipindi cha Julai,2019 hadi Machi, 2020 jumla ya maofisa naaskari 1,537 walipata mafunzo ya uongozi wa kijeshi katika Vyuo vya Magereza nawatumishi 951 walihitimu mafunzo ya taaluma mbalimbali katika vyuo vya ndani na nje yaJeshi.

“Jeshi linatarajia kuajiri askari 685 wenye fani mbalimbali watakaopatiwa mafunzo ya awali katika Chuo cha Magereza Kiwira (Mbeya), mafunzo ya uendeshaji wa Magereza na Taaluma ya Urekebishaji kwa Maafisa na Askari 3,270 katika ngazi mbalimbali za uongozi,” alisema.

Waziri Simbachawene alisema kuhusu hali ya ulinzi na usalama magerezani, hadi kufikia mwezi Machi, 2020 kulikuwa na jumla ya wafungwa na mahabusu 32,438 katika magereza yote nchini na kwamba kati ya hao, wafungwa ni 14,464 na mahabusu 17,974 ambapo ni asilimia 9 zaidi ya uwezo uliopo wa kuhifadhi wafungwa na mahabusu 29,902.

Simbachawene alisema mwaka 2020/21Idara ya Uhamiaji inatarajia kuajiri askari 495 na kuwapa mafunzo ya awali, ikiwamo kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa maofisa, askari na watumishi raia ili kuwaongezea ujuzi wa utendaji kazi kwa ufanisi zaidi.

Alisema katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa rasilimaliwatu, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatarajia kuwapandisha vyeo Maoafisa na askari 1,311 na kuajiri askari wapya.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga na Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa wamekutana na waandishi wa habari ili kuzungumza  na umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake  katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameanza kwa kueleza mahitaji na matumizi ya sukari nnchi ‘‘Mahitaji ya sukari ya matumizi ya kawaida Nchini yanakadiriwa kufikia tani 470,000 kwa Mwaka. Kiasi hiki ni kwa wastani wa mahitaji ya kiasi cha tani 38,000 kwa kila Mwezi pamoja na kiasi cha tani 14,000 kwa ajili ya dharura. 
 
Uwezo wa viwanda vyetu vya ndani kwa msimu wa 2019/20 kwa mujibu wa makadirio ya mwanzoni mwa msimu yaani Julai, 2019 ni kuzalisha takribani tani 378,000 za sukari. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 82.9 ya mahitaji halisi ya tani 456,000 ambayo hayajumuishi kiasi cha dharura cha tani 14,000. 
 
Uwezo huu wa uzalishaji wa viwanda vya ndani unaacha pengo la kiasi cha tani 78,000 ili kuweza kutosheleza mahitaji halisi ya tani 456,000 bila kiasi cha dharura cha tani 14,000.
 
Hata hivyo, uwezo huu wa uzalishaji wa viwanda vya ndani ulitarajiwa kufikiwa pale tu panapokuwa na hali nzuri ya hewa na ufanisi mzuri wa viwanda’’

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameendelea kwa changamoto ambazo zimekumba msimu wa uzalishaji sukari wa Mwaka 2019/2020
 
‘‘Kutokana na ukweli kwamba msimu wa uzalishaji sukari wa Mwaka 2019/20 umekumbwa na changamoto kadha wa kadha zikiwemo
      i.         Mvua nyingi kupita kiasi ambayo imepelekea uvunaji wa miwa kuwa mgumu,
    ii.         Mlipuko wa magonjwa ya miwa kama vile viding’ata wa njano n.k,
   iii.         Uharibifu wa mitambo ya baadhi ya viwanda na kuchelewa kupatiwa vipuri.
Sababu hizo zote kwa pamoja zimechangia kwa kiasi kikubwa Viwanda vyetu vya ndani kushindwa kufikia malengo ya kuzalisha tani 378,000 za sukari kwa msimu wa 2019/20.’’

Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa ametoa hali ya uzalishaji wa viwanda vya sukari nchini:
Na.
Jina la Kiwanda
Malengo ya Uzalishaji (tani)
Kiasi kilichozalishwa (tani)
Uzalishaji (%)
1
Kilombero Sugar Co. Ltd
                    120,183
                    103,122
85.8
2
TPC Ltd
                      90,815
                      88,968
98.0
3
Kagera Sugar Ltd
                      95,000
                      79,403
83.6
4
Mtibwa Sugar Estates Ltd
                      33,513
                      20,705
61.8
5
Manyara Sugar Co. Ltd
                       5,785
                        6,750
116.7

JUMLA
                   345,296
                   298,949
86.6

‘­­­‘Kutokana na hali halisi ya uzalishaji wa ndani wa sukari kuwa pungufu ya malengo ya uzalishaji, Serikali ilifanya makadirio ya kiasi cha sukari ya kuziba pengo la uzalishaji (gap sugar) na kutoa vibali kwa wazalishaji ili kuweza kuagiza na kuingiza sukari hiyo Nchini kwa wakati kwa ajili ya kukidhi mahitaji. Hadi hivi sasa tunazungumza na nyinyi, sukari iliyoagizwa kuja kuziba pengo la uzalishaji takribani tani 10,710 imeshaingia nchini na inaendelea  kusambazwa katika Mikoa yote.
 
Mnamo tarehe 24, 28 na 30 Aprili, 2020 tunategemea kupokea jumla ya tani 13,500 za sukari ya kuziba pengo na tutaendelea kupokea kiasi kingine cha sukari Mwanzoni mwa Mwezi Mei, 2020. Kiasi chote cha sukari kilichopo Nchini na tunachoendelea kupokea kinatosheleza kabisa mahitaji ya sukari nchini. Kwa taarifa hii, tuwaombe Wananchi wote kuwa watulivu kwa sababu Nchi yetu inayo sukari ya kutosha.’’

Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa amesema serikali haitakubali kuona wafanyabiashara kupandisha bei kiholela
 
‘‘Tunapenda kuwatangazia Wafanyabiashara wote Nchini wenye tabia hizi za kupandisha bei kiholela waache mara moja kwani Serikali haipo tayari kuona Wananchi wake wanaumia kwa manufaa ya watu wachache.
Serikali itachukua hatua kali kwa Mfanyabiashara yeyote ambaye atabainika kujinufaisha kwa kuuza sukari bei ya juu kulikoni bei ya kawaida ya soko.’’

Aitha, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kabla ya kutangaza bei ya sukari ya reja reja Katika Mikoa yote nchini amesema;
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Sukari  Na. 26 ya Mwaka 2001(Cap. 251) chini ya kifungu cha 11A inampa Mamlaka Waziri mwenye dhamana ya Kilimo kutangaza bei ya ukomo wa juu ya sukari.
 
Kutokana na changamoto ya wafanyabiashara kupandisha kiholela bei ya sukari nchini, Serikali tumeamua kuutangazia Umma wa Watanzania bei Kikomo ya sukari katika Mikoa yote Nchini Tanzania. Bei hizi kikomo zinalenga kukabaliana na changamoto ya kupanda kiholela kwa Bei ya Sukari Nchini ambayo kwa sasa imefikia wastani wa Shilingi 4,000/= hadi 4,500/= kwa kilo. Bei hii kikomo ya sukari imepangwa kwa kuzingatia gharama zote za uagizaji wa sukari ya kuziba pengo zinazotumiwa na wazalishaji kuagiza sukari kutoka nje ya Nchi.
 
Hivyo, kwa niaba ya Serikali tunapenda kuutangazia umma wa Watanzania kuwa bei ya sukari ya reja reja Katika Mikoa yote nchini itakuwa kama ifuatavyo;

KIWANGO CHA JUU CHA BEI YA SUKARI KWA REJA REJA KWA KILA MKOA

NA.
MKOA
BEI YA  KILO (Tsh)




  1.  
IRINGA
2,900

  1.  
MBEYA
3,000

  1.  
RUKWA
3,200

  1.  
KATAVI
3,200

  1.  
RUVUMA
3,200

  1.  
NJOMBE
2,900

  1.  
LINDI
2,800

  1.  
MTWARA
2,800

  1.  
ARUSHA
2,700

  1.  
KILIMANJARO
2,700

  1.  
MANYARA
2,700

  1.  
TANGA
2,700

  1.  
DAR ES SALAAM
2,600

  1.  
PWANI
2,700

  1.  
MOROGORO
2,700

  1.  
KAGERA
3,000

  1.  
MWANZA
2,900

  1.  
SIMIYU
2,900

  1.  
SHINYANGA
2,900

  1.  
GEITA
2,900

  1.  
MARA
3,000

  1.  
KIGOMA
3,200

  1.  
SINGIDA
2,900

  1.  
TABORA
2,900

  1.  
DODOMA
2,900

  1.  
SONGWE
3,000

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amemaliza kwa kusisitiza kuwa;
‘‘Bei hizi za ukomo za sukari zimezingatia umbali wa kila eneo katika Mikoa yote nchini. Niwaombe Wafanyabiashara wote nchini kuzingatia maelekezo haya ya Serikali. Yeyote atakayekiuka maelekezo haya atakuwa ametenda kosa na hivyo atafikishwa katika vyombo vya sheria ili apate adhabu ambayo itahusisha ama kunyang’anywa leseni ya biashara, kulipa faini au adhabu zote kwa pamoja. Tutachukua hatua kali za kisheria kwa mfanyabiashara yeyote ambaye atakiuka masharti haya.’’