Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Timotheo Mnzava akiwa ameambatana na Mchumba wake Caroline Pallangyo ambaye ni Mtoto wa Mbunge waJimbo la Arumeru Mashariki John D Pallangyo.


Askofu Mkuu Dayosisi ya Meru Elias Nassary mapema hii leo amebariki Send-off ya Mtoto wa Mbunge Caroline John D Pallangyo na Mbunge wa Korogwe Vijijini Timotheo Mnzava na kuwataka wanandoa hao kudumishwa upendo kwani ndoa nyingi za Vijana wa siku hizi zimekuwa ni changamoto.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi {CCM} Dr. John D Pallangyo Amemsihi  Timotheo Mnzava pamoja na mwanaye anayeolewa na Mbunge huyo kwenda kuishi katika Ndoa takatifu yenye upendo wa kujali jamii inayowazunguka na kutambua kwamba maisha ya ndoa hujengwa kwa upendo na kujali jamii. PICHA MBALIMBALI KUTOKA KWENYE HAFLA HIYO.


Askofu Mkuu wa Jimbo la Arumeru Elias Nassary 
Share To:

Post A Comment: