Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Moremi Marwa, Julai 4, 2025, amefanya ziara maalum katika Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (SabaSaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Bw. Marwa alipokelewa na wataalamu waandamizi wa TTCL, ambao walimtembeza katika maeneo mbalimbali ya banda hilo na kumweleza kwa kina kuhusu huduma na teknolojia zinazotolewa na Shirika hilo.

Miongoni mwa huduma zilizowasilishwa ni pamoja na Faiba Mlangoni, inayowezesha upatikanaji wa intaneti ya kasi moja kwa moja majumbani na maofisini, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya TTCL kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za mawasiliano kwa gharama nafuu.

Pia alielezwa kuhusu Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB), ambao tayari umesambazwa katika mikoa yote 26 na wilaya 112 kati ya 139 nchini. Mkongo huo umeunganisha Tanzania na nchi jirani na kuchochea matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Huduma nyingine alizotembelea ni pamoja na Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Taarifa Kimtandao (NIDC), chenye uwezo wa kisasa wa kuhifadhi na kulinda taarifa muhimu za taasisi na kampuni mbalimbali, na hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu alifahamishwa kuhusu huduma ya Call Center ya TTCL inayosaidia mashirika kuwasiliana kitaalamu na wateja wao, pamoja na WiFi ya Umma (Public WiFi) inayowawezesha wananchi kupata huduma ya intaneti kwa urahisi katika maeneo ya wazi.

Katika kuendeleza ushirikiano wa kimkakati, Bw. Marwa pia alitembelea mabanda ya taasisi mbalimbali rafiki, ikiwemo Shirika la Posta Tanzania (TPC), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), pamoja na Banda la Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Katika kila banda, alielezwa kuhusu majukumu na huduma zinazotolewa, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano ili kufanikisha malengo ya pamoja ya kidijitali na kiuchumi kwa maendeleo ya Taifa. 


















NA EMMANUEL MBATILO, PWANI

HIFADHI ya Mazingira Asilia ya Uluguru kutoka mkoani Morogoro imefanya ziara ya mafunzo katika Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Pugu Kazimzumbwi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wadau wa utalii kutoka mkoa huo, sambamba na kuimarisha ushirikiano katika uhifadhi wa mazingira na kukuza utalii wa ikolojia.
Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ametoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mikopo na mifuko mbalimbali ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) Tanzania bi.Hadija Juma Ngasongwa amesema wawekezaji wa ndani ya nchi wanasimamiwa na sheria madhubuti zinazosimamia uwekezaji nchini, kusaidia kuimarisha biashara nchini, kulinda

 


Wananchi wametakiwa kuwa na uelewa kuhusu Sera za Kodi  zinazoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la kumfanya mwananchi kulipa kodi kwa hiari ili kuisaidia Serikali kutoa huduma bora na endelevu katika sekta mbalimbali ikiwemo ya afya, maji, barabara, nishati na kilimo.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na mabanda mengine kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) ambayo yameanza  tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.

Alisema kuwa Bunge limepitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Kiasi cha shilingi trilioni 56.49 ambayo inalenga pamoja na mambo mengine kutekeleza miradi yenye faida ya moja kwa moja kwa mwananchi kama barabara, nishati, maji na kilimo.

Bi. Omolo alisema kuwa jukumu la mwananchi katika kufanikisha hilo ni pamoja na kulipa kodi kwa hiari kwa mazingira rafiki ambayo yanatokana na Sera nzuri za kodi ambazo zimeandaliwa  na Wizara ya Fedha. 

Ametoa rai kwa wananchi wanaotembelea katika Maonesho hayo kufika Banda la Wizara ya Fedha ili kukutana na wataalamu ambao watawapa elimu ya Sera ya Kodi na faida zake kwa jamii.

Bi. Omolo amewahakikishia wananchi kupata huduma bora kutoka Serikalini kupitia Bajeti iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa gharama nafuu.

Aidha, alisema kuwa ndani ya Banda la Wizara ya Fedha inatolewa elimu ya huduma ndogo za fedha kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa wa masuala ya fedha ili kuondokana na kuchukua mikopo isiyo na tija. 

Alisema pia kuwa Banda la Wizara ya Fedha linashirikisha Vyuo vikuu vilivyo chini ya Wizara ambavyo vinatoa elimu kuhusu kozi mbalimbali ambapo alivitaja vyuo hivyo kuwa ni pamoja na, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA). 

Aidha alisema kuwa wataalamu wengine ni kutoka Idara na Vitengo vya Wizara hiyo na Taasisi zake ikiwa ni pamoja na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji Tanzania (UTT AMIS), Mfuko wa Self Microfinance, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).

Taasisi nyingine ni pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT), Benki ya Maendeleo TIB na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Hazina SACCOS, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).









Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umewasihi Watanzania kote nchini kuachana na dhana ya kwamba Nishati Safi ya Kupikia ni gharama ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Pro. Haruni Mapesa leo ametembelea Banda la Chuo katika Maonesho ya Kimataifa ya biashara maarufu Kama (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukagua bunifu mbalimbali zilipo kwenye Banda Prof. Mapesa amewataka Wadau mbalimbali Kutembelea Banda la Chuo ili waweze kusoma machapisho na vitabu mbalimbali,  waone bunifu zilizoandaliwa na Wanafunzi, pamoja na Wanafunzi kufanyiwa udahili  katika Banda la Chuo.


Amesema Chuo Pia kinatoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu katika masuala ya Uongozi , Maadili na Utawala hivyo ameeakaribisha Wadau kufika kwenye Banda Hilo la Chuo.


Katika ziara hiyo Prof. Mapesa pia aliambatana na Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe.


Imetolewa na 

Kitengo cha Mawasiliano na Masoko

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

03.07.2025

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kupitia Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu, kimebuni mashine ya kisasa ya kuuza vinywaji baridi inayojiendesha yenyewe bila kuhitaji uwepo wa mtu kwa ajili ya kutoa huduma kwa mteja.
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) linashiriki katika maonesho ya 49 ya kimataifa ya Biashara katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu na watakuwepo hapo kipindi chote cha maonesho ili kuwawezesha Watanzania.
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya China ya CPP na CPTDC kwaajili ya ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Ntorya hadi Madimba mkoani Mtwara kwa kipindi cha miezi 12.

‎ Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo Serikali itaendelea kulinda na kukuza viwanda vya ndani kwa kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa biashara na uwekezaji ili kuongeza ajira, Pato la Taifa na kukuza uchumi Jumuishi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Waziri Jafo ametoa wito kwa Wazalishaji Kundelea kutumia malighafi za ndani Katika kuzalisha bidhaa mbalimbali kama TCC anavyozalisha bidhaa zake kwa kutumia malighafi kutoka kwa wakulima wa Tanzania

‎ Ameyama hayo Julai 03, 2025 alipotembelea Kampuni ya Sigara Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya JTI (Japan Tobacco International) jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda Bw. Juma Mwambapa kwa lengo la kujifunza shughuli za uzalishaji na kusikiliza changamoto zao.

‎Waziri Jafo pia ameipongeza Kambuni hiyo kwa uzalishaji mzuri unaojumuisha mnyororo wa thamani wa Tumbaku kuanzia kwa Mkulima hadi Kiwandani kwa kutumia malighafi zilizopo nchini hatua inayosaidia kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira nchini.

‎Naye Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Tanzania Sigara Tanzania (TCC), Bi. Patricia Mhondo, amebainisha kuwa shughuli za TCC zinagusa maisha ya watu nchini kupitia mnyororo wa thamani unaowahusisha wakulima, wazalishaji, wauzaji na wasambazaji.

‎“Kwa maana hiyo, kampuni yetu inaleta ajira kwa watu wengi zaidi ya wale waliopo ndani ya TCC moja kwa moja. Hii inachangia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza mapato ya Serikali kupitia ulipaji wa kodi,"

‎Aidha, alitumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa Waziri wa Viwanda na Biashara kwa kutembelea kiwanda hicho na kufanya mazungumzo nao kuhusu mafanikio ya kampuni na changamoto wanazokumbana nazo.

 


Na Mwandishi Wetu - KILIMANJARO


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo  kwa kugharamia mazishi ya  miili  42 ya watu waliofariki dunia kufuatia  ajali iliyotokea  Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Mhe. Nderiananga ametoa shukrani hizo  tarehe 03 Julai, 2025 wakati aliposhiriki tukio la kuaga miili 35 katika viwanja vya Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) akisema miili Saba ilichukuliwa na ndugu zao na miili miwili bado vipimo vya DNA vinafanyiwa kazi ili kutambulika.

Tukio hilo lilioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu ambapo Mhe. Nderiananga alimpongeza kwa kujitoa kwa kiasi kikubwa tangu ilipotokea ajali hiyo akishirikiana na watendaji wake wote.

Amesema Serikali  kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa iliyopo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kilimanjaro kwa juhudi kubwa zilizofanyika kuokoa manusura wa ajali hiyo pamoja na miili ya walioungua kwa moto mara baada ya ajali kutokea.

Vilevile ameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuchukua  sampuli za miili hiyo (DNA)  kuhakikisha ndugu wanatambua miili ya wapendwa wao.

Hata hivyo  Mhe. Nderiananga ameendelea kutoa pole kwa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huo mzito kwa Taifa  huku akiwaomba kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu hadi watakapokamilisha kuwahifadhi wapendwa wao. 



Aidha, ajali hiyo iliyotokea Juni 28 2025 katika Kitongoji Mahuu, Kata ya Same, takribani kilomita nne kutoka Same mjini, ililihusisha basi kubwa la abiria, Mali ya Kampuni ya Chanel One, lenye namba za usajili T 179 CWL na basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster, lenye namba T 199 EFX linalomilikiwa na Kampuni ya Mwami Trans.




Coaster hiyo, ilikuwa ikitokea Same kuelekea Manispaa ya Moshi, wakati basi la Chanel One lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Tanga.