Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Pro. Haruni Mapesa leo ametembelea Banda la Chuo katika Maonesho ya Kimataifa ya biashara maarufu Kama (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukagua bunifu mbalimbali zilipo kwenye Banda Prof. Mapesa amewataka Wadau mbalimbali Kutembelea Banda la Chuo ili waweze kusoma machapisho na vitabu mbalimbali, waone bunifu zilizoandaliwa na Wanafunzi, pamoja na Wanafunzi kufanyiwa udahili katika Banda la Chuo.
Amesema Chuo Pia kinatoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu katika masuala ya Uongozi , Maadili na Utawala hivyo ameeakaribisha Wadau kufika kwenye Banda Hilo la Chuo.
Katika ziara hiyo Prof. Mapesa pia aliambatana na Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
03.07.2025
Post A Comment: