Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Denis Londo, amesema ubora wa bidhaa ni nguzo muhimu katika kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania kwenye soko la kimataifa na kufanikisha azma ya nchi ya kujenga uchumi wenye thamani ya dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050.
Kariakoo, 31 Julai, 2026

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Kariakoo imeendelea kuimarisha ushirikiano na walipakodi kupitia mikutano ya ana kwa ana (Outreach) inayolenga kusikiliza, kutatua changamoto na kutoa elimu ya kodi ili kuwawezesha walipakodi kutekeleza wajibu wao kwa hiari.
Kuingia kwenye ndoa ni matumaini ya kila mwanamke kwamba atapata mume atakayempenda, kumheshimu, na kuilinda familia yao. Hata hivyo, mara tu baada ya harusi yetu, ndoa yangu iligeuka kuwa uwanja wa maumivu na dharau kubwa.

Mume wangu alibadilika ghafla na kuanza kuendesha nyumba yetu kwa maelekezo ya mama yake mzazi pekee. Kila uamuzi uliotakiwa kufanywa kuanzia matumizi ya fedha, chakula kinachopikwa, hadi malezi ya watoto ulipaswa kupitishwa na mama mkwe wangu kwanza.

​Kila nilipojaribu kutoa maoni yangu au kushauri kama mke wa ndani, mume wangu alinisukuma pembeni, kunitusi, na kuniambia kuwa mimi ni mgeni tu aliyetoka mbali ambaye sina haki ya kupinga kauli ya mama yake.

Mama mkwe alitumia fursa hiyo kunidharau waziwazi na kunifanyia vitimbi vya kila aina ili nionekane sifai. Nilibaki nikiwa sina sauti wala thamani kwenye nyumba yangu mwenyewe, nikilia usiku kucha kwa uchungu wa kuonekana kama mjakazi na sio mke halali.SOMA ZAIDI.

 

Kwa zaidi ya miaka minne, nilikuwa nikimiliki duka kubwa la vifaa vya ujenzi na bidhaa za nyumbani katika mji wetu. Biashara hii ilikuwa ndiyo tegemeo langu kuu na chanzo cha rizki kwa familia na wafanyikazi wangu sita.

Niliwekeza mamilioni ya fedha na mtaji wangu wote ili kuhakikisha duka langu linakuwa na kila aina ya bidhaa zenye ubora wa hali ya juu. Hata hivyo, kuanzia katikati ya mwaka jana, mambo yalianza kubadilika ghafla kwa njia ya kutatanisha sana.

​Duka langu lilikuwa katikati ya mji ambapo watu wengi wanapita, lakini ajabu ni kwamba wateja walikuwa wakipita mlangoni na kuingia kwenye maduka ya jirani yaliyokuwa na bidhaa chache kuliko zangu.

Siku zilipita bila kuuza hata bidhaa moja ya maana. Akiba yangu ya benki ilisha kabisa, madeni ya wauzaji wa jumla yalianza kunilundikia, na wafanyikazi wangu walishindwa kupata mshahara kwa miezi mitatu mfululizo.

Nilibaki nikiketi dukani kuanzia asubuhi hadi jioni nikiwa na msongo mkubwa wa mawazo, nikitazama biashara yangu ya mamilioni ikiporomoka kuelekea kufilisika kabisa. SOMA ZAIDI.

 

Jina langu ni Baraka. Kuna siku moja katika maisha yangu ambayo sitaisahau kamwe.

Ilikuwa siku ambayo kosa dogo la kutuma pesa lilibadilisha maisha ya familia yangu.

Mama yangu alikuwa amelazwa hospitalini katika hali mbaya sana. Madaktari walihitaji malipo ya haraka ili kuendelea na matibabu yake.

Nyumbani kulikuwa na hofu kubwa. Kila mtu alikuwa akipiga simu kutafuta msaada. Ndugu walichangia walichoweza.

Baada ya kuhangaika kwa muda, hatimaye nilifanikiwa kupata TSh 1,850,000. Kwangu mimi, hiyo haikuwa pesa tu.

Ilikuwa matumaini. Ilikuwa nafasi ya kumuokoa mama yangu. SOMA ZAIDI.

Takribani wakulima wadogo 1,000 kutoka mikoa ya Morogoro, Dodoma na Arusha wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya kuondokana na matumizi ya viuatilifu hatarishi katika shughuli zao za kulimo. Idadi hiyo ya wakulima itawagusa moja kwa moja wakulima wa mbogamboga, vitunguu, mbogamboga na pamba waliopo kwenye wilaya za Karatu, Chamwino, Mvomero na Meru. Hatua hiyo inayolenga kuwahamasisha wakulima kuachana na matumizi ya viuatilifu hatarishi ili kupunguza madhara ya kiafya yanayosababishwa na kemikali hizo kuanzia kwa mkulima mpaka kwa mlaji.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Asasi Isiyo ya Kiserikali ya AGENDA For Environment and Responsible Development, Dorah Swai, mkoani Morogoro wakati wa warsha ya siku mbili ya wadau wa kilimo bora na mazingira kutoka katika taasisi za serikali na binafsi. Bi. Swai amesema kuwa mradi huo uliofadhiliwa na mfuko wa Global Frame Work (GFC) unahusisha nchi tatu za ukanda wa Mahariki mwa Afrika ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia na kila nchi imejiwekea malengo ya kufikia angalau wakulima 1000. Amesema dhamira kuu ya mradi huo wa kuondoa viuatilifu hatarishi ukanda wa Mashariki mwa Afrika una lengo la kuangalia namna bora ya kuwawezesha wakulima wadogo 3,000 watakaokuwa vinara wa mabadiliko katika matumizi ya viuatilifu mbadala kwa wenzao.

Katika warsha hiyo, Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Joseph Kiwango, amesema serikali iko tayari kushiriukiana na wadau wote wenye nia ya kuwainua Watanzania kupitia sekta ya kilimo kinachozingatia utunzaji wa mazingira na afya za binadamu. Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Asasi ya Mwavuli wa Kilimo Hai Tanzania (TOAM), Bakari Mongo, pamoja na Afisa Programu Mkuu wa Agenda, Silvani Mng’anya, kila mmoja kwa nyakati tofauti amesema suala la kupambana na viuatilifu hatarishi halipaswa kuwa la mtu mmoja au kikundi Fulani, kwani madhara ya viuatilifu hatarishi hayaishii kwa mtu mmoja. “Jukumu la kuondoa viuatilifu hatarishi halipaswa kuwa la mtu mmoja, ni jukumu letu sote katika kuhakikisha mlaji wa mwisho analindwa dhidi ya madhara yatokanayo na viuatilifu hatarishi.”amesema Mongo.

 

 

Na. Mtemi Sona

Dodoma. Mwenyekiti wa Ujenzi Sports Club, Arch. Ibrahim Chatila, amesema uongozi mpya umejipanga kuijenga timu hiyo kuwa ya kisasa, imara na yenye ushindani mkubwa katika mashindano yote itakayoshiriki.

Akizungumza kuhusu mikakati ya kuiboresha klabu hiyo iliyo chini ya Wizara ya Ujenzi, Chatila amesema lengo kuu ni kuunda kikosi chenye ubora wa hali ya juu kitakachokuwa na uwezo wa kushindana na timu mbalimbali nchini.

Amesema hatua za awali zitahusisha usajili wa wachezaji bora pamoja na kuimarisha benchi la ufundi kwa kuwashirikisha makocha wenye uwezo na sifa zinazohitajika ili kuongeza ushindani wa timu.

"Tunataka kuunda timu yenye wachezaji watakaoweza kuleta ushindi na ambao watazingatia weledi, nidhamu na taaluma katika kila mashindano tutakayoshiriki," amesema Chatila.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa uongozi mpya uliochaguliwa umeazimia kuijenga upya Ujenzi Sports Club kwa misingi ya umoja, utawala bora na uwajibikaji kuanzia kwa viongozi, benchi la ufundi, wachezaji hadi wanachama.

Kwa mujibu wa Chatila, mafanikio ya timu hayatategemea ubora wa kikosi pekee, bali pia uimara wa mifumo ya uendeshaji wa klabu.

Mbali na masuala ya kiufundi, amesema uongozi wake umeweka mkazo katika kuimarisha uchumi wa klabu kwa kutafuta wadhamini na wadau mbalimbali watakaosaidia kuiendesha timu kwa kiwango cha kisasa.

"Lengo letu ni kuwa na klabu inayojitegemea kiuchumi, yenye uwezo wa kujiendesha na kushiriki mashindano kwa ushindani mkubwa," amesema.

Arch. Ibrahim Chatila ni Mbunifu Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambayo ni moja ya taasisi zinazounda Ujenzi Sports Club. Pia ni kocha mwenye leseni ya CAF na amewahi kuwa mjumbe wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida kwa kipindi cha miaka minne.

Yeye ni miongoni mwa viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni kuiongoza Ujenzi Sports Club, klabu inayoundwa na taasisi 10 zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi.

Klabu hiyo hushiriki michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, netiboli, riadha, kuvuta kamba na michezo mingine ya ushindani.