✅YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI KWA SAUDI ARABIA


Shirika la Madini la Taifa( STAMICO) limefanya mazungumzo na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Serikali ya Saudi Arabia kuelezea fursa za uwekezaji zilizopo katika mnyororo wa rasilimali madini kwa manufaa ya watanzania.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse katika Mkutano uliofanyika Agosti 18 2026 jijini Dar es Salam

Dkt Mwasse, amesema STAMICO inaendelea kufungua milango kwa wawekezaji kulingana na Sheria na taratibu za Serikali ili kuhakikisha inaleta manufaa kwa wote.

Amesema Shirika linazingatia misingi ya kujiendesha kibiashara na kwa uwazi ili kuzuia mianya ya urasimu na kuhakikisha inatoa matokeo yenye tija kwa haraka.

STAMICO, ni Shirika sahihi kuingia nalo ubia kwa kuwa lina wataalam wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha, ushirika mzuri na jamii inayozunguka miradi na uwezo wa kushirikiana na taasisi zingine.

Naye, Abdulrahman Al Thobaity Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyabiashara wa Saudia Tanzania, ameshukuru kwa taarifa za fursa za uwekezaji na ushirikiano waliopata kutoka STAMICO.

Kwa upande wa wataalam meneja wa Utafiti Bw Frederick Mangasini Ametumia nafasi hiyo kuonesha fursa za uwekezaji katika miradi mbalimbali ikiwemo ya dhahabu, makaa ya mawe, shaba (copper) na uendelezaji wa wachimbaji wadogo

STAMICO inaendelea kujiimarisha na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa maslahi ya taifa.










Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: