Bodi ya Nishati Vijijini (REB) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu, leo tarehe 8 Mei, 2026 imefanya kikao na Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini katika Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha wanaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili kupata taarifa ya utekelezani wa miradi hiyo.

Mwenyekiti Kingu ambaye alikuwa ameongozana na Wajumbe wa Bodi hiyo, Mhe. Balozi Radhia Msuya na Mhandisi Sophia Mgonja walikutana na Kampuni ya Ceylex Engineering Limited na Derm Group Limited na ambao wanatekeleza miradi kwa Mkoa wa Kilimanjaro na pia walikutana na Kampuni ya Ceylex Engineering Limited na Nakuroi Investment Company Limited ambazo zinatekeleza miradi kwa Mkoa wa Arusha.

Mwenyekiti Balozi Meja Jenerali Mstaafu Kingu, amewatata wakandarasi hao kutekelezea miradi hiyo ndani ya muda wa mkataba waliosaini na kuhakikisha wanazingatia ubora unaotakiwa.

Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu, Meneja Msimamizi wa Miradi kutoka REA, Mhandisi Deogratius Nagu, Meneja wa Teknolojia za Nishati kutoka REA, Mhandisi Michael Kyessi, Mhandisi Miradi kutoka REA, Isaac Sanga pamoja na Mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Alex Sonna

Post A Comment: