Wizara ya Viwanda na Biashara imeendelea kupambana na bidhaa bandia nchini kupitia operesheni maalum zilizofanywa na Tume ya Ushindani (FCC), ambapo hadi Aprili 2026 jumla ya chupa 4,251 za pombe bandia, chupa tupu 286 na katoni tupu 250 zilikamatwa jijini Dar es Salaam.

Katika operesheni hizo, pia vifaa vya uzalishaji na ufungashaji wa bidhaa bandia vilikamatwa ikiwemo mashine za kuchapisha maelezo ya bidhaa, kipima kilevi, mashine za kufunga vifuniko, mizani, ethanoli pamoja na vifaa vya kuchanganyia na kuchujia pombe.

Akiwasilisha Mpango wa bajeti leo Mei 22,2026 bungeni,Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema mbali na pombe bandia, FCC pia imebaini uwepo wa bidhaa nyingine bandia zikiwemo vipuri na vilainishi ambapo watuhumiwa walichukuliwa hatua mbalimbali za kisheria.

Amesema mkakati wa Serikali katika kukabiliana na bidhaa bandia unajikita katika kuimarisha uchunguzi wa taarifa za kiintelijensia, kufanya operesheni za ukaguzi na ukamataji pamoja na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wahusika.
Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: