Mwenyekiti wa UVCCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewasili mkoani Mtwara leo tarehe 18 Mei 2026 na kupokelewa katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mtwara.
Ndugu Kawaida amepokea taarifa ya CCM mkoa wa Mtwara, taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM ambapo alifanya kikao cha ndani.
Akizungumza na Watendaji wa CCM ngazi ya mkoa wa Mtwara amewasihi kuendelea kuitangaza miradi inayotekelezwa kwa Wananchi na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa CCM.
Ndugu Kawaida amewataka watendaji wote kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na kutumia mitandao ya kijamii kueneza amani ya nchi.
Mwenyekiti Kawaida ataendelea na ziara ya kutembelea wanufaika wa miradi ya mikopo ya asilimia 4, kuzungumza na wananchi na kusikiliza maoni yao.

Post A Comment: