Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir,akizungumza wakati akifunga Mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo Aprili 30,2026 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,akizungumza wakati wa Mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo uliofanyika leo Aprili 29,2029 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakisikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir (hayupo pichani) wakati akifunga Mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo Aprili 30,2026 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir,akiwa katika picha ya pamoja wakati akifunga Mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo Aprili 30,2026 jijini Dodoma.

......
Serikali imewataka watumishi wa sekta ya elimu nchini kuimarisha mshikamano, uwajibikaji na ubunifu ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu bora inayokidhi mahitaji ya karne ya 21.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir wakati akifunga Mkutano wa Pili wa Baraza la 37 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Aprili 30,2026 jijini Dodoma.
Mhe.Ameir amesisitiza kuwa mafanikio ya sekta ya elimu yanategemea kwa kiasi kikubwa ushirikiano kati ya wafanyakazi, menejimenti pamoja na wadau wote wa elimu, akibainisha kuwa mshikamano huo ni chachu ya kuleta mageuzi chanya na endelevu.
Ametoa pongezi kwa uongozi wa Wizara, ukiongozwa na Waziri Adolf Mkenda, kwa kuendelea kusimamia mageuzi ya elimu ikiwemo maboresho ya sera na mitaala inayolenga kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani.
Aidha, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake unaoendelea kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu, hususan katika kukuza ubora wa elimu, ubunifu na tafiti.
" Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha elimu, ikiwemo uzinduzi wa Mkakati wa Kisayansi wa Kuimarisha Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) pamoja na mpango wa kuunganisha taasisi za elimu na waajiri."amesema Mhe.Ameir
Ameeleza kuwa mipango hiyo inalenga kuwajengea wanafunzi ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira na hivyo kuongeza ushindani wao kitaifa na kimataifa.
Hata hivyo amewataka wajumbe wa baraza hilo kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, akisisitiza umuhimu wa kuwa na maadili, nidhamu na uwajibikaji kazini.
Amebainisha kuwa baraza la wafanyakazi limeendelea kuwa jukwaa muhimu la majadiliano, ushauri na maamuzi yanayochangia kuboresha utendaji kazi pamoja na ustawi wa watumishi.
Katika mkutano huo, mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo bajeti ya wizara, usimamizi wa rasilimali watu, maadili ya utumishi wa umma na afya ya akili mahali pa kazi.
Ameir amesema mada hizo zina mchango mkubwa katika kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza tija kwa watumishi, hivyo kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Aidha Ameir ametoa wito kwa watumishi wote kuendelea kudumisha mshikamano, uzalendo na uadilifu, pamoja na kuwa mabalozi wa kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.Carolyne Nombo, amesema kuwa utekelezaji wa kaulimbiu ya mkutano wa wafanyakazi ya “Ushirikishwaji na Mshikamano wa Wafanyakazi ni Chachu ya Kuimarisha Elimu Inayochochea Ubunifu” ni muhimu katika kufanikisha malengo ya sekta ya elimu nchini.
Prof. Nombo amesisitiza kuwa mshikamano na ushirikiano kazini ni msingi wa kuleta mabadiliko ya kweli katika sekta ya elimu.
Ameeleza kuwa kaulimbiu hiyo inalenga kuwajenga watumishi kuwa na utamaduni wa kufanya kazi kwa pamoja, kwa bidii na kwa uwajibikaji, hali ambayo itachochea mageuzi makubwa yanayohitajika katika kuboresha ubora wa elimu nchini.
“Tunaposhirikiana na kufanya kazi kwa bidii kama timu moja, tunaweka msingi imara wa kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya elimu, yanayoakisi dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2050,” amesema Prof. Nombo.
Ameongeza kuwa juhudi hizo zinapaswa kuendana na utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (toleo la 2023), pamoja na kuzingatia mabadiliko mbalimbali yaliyofanyika katika mitaala iliyoboreshwa.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa watumishi kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya serikali katika kutekeleza majukumu yao, akibainisha kuwa nidhamu na uwajibikaji ni nguzo muhimu za kufanikisha malengo ya wizara.

Post A Comment: