Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema Serikali katika mwaka wa fedha 2025/26 imetenga bajeti kwa ajili ya malipo ya fidia yenye thamani ya Sh Bilioni 5.1 kwa wananchi 1, 730 wanaopisha njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 kutoka Masasi hadi Mahumbika.
Mhe. Salome ametoa kauli hiyo leo Aprili 13, 2026 wakati akijibu swali la Mbunge wa Ndanda, Mhe. Faraji Buriani Nandala aliyehoji ni lini Wananchi wa Kata za Chikukwe, Chigugu, Chigundi, Mwena, Ndanda na Nanganga ambao wamepitiwa na Mradi wa Grid ya Taifa watalipwa fidia.







Post A Comment: