Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Isack Joseph Copriano amesimamisha uuzaji wa ardhi katika kata ya Esilale huku akita maeneo yote ya malisho kuhakikiwa upya na idara ya ardhi wilaya ya Monduli.

Yote hayo yanajiri mara baada kundi la wamama zaidi 200 kutoka majumbani kwao na kwenda kukaa eneo la Losirwa lililouzwa  kinyemela na kupaza sauti zao kuiomba  serikali kuingilia kati na ili kurejeshewa eneo lao muhimu la malisho.

Mhe.Isack amesisitiza kuwa amefanya hivyo kwasababu yeye ni mwakilishi wa wananchi nani mtu namba moja anayetetea  maslahi ya wananchi wake wa jimbo la Monduli.

“Ili kujiridhisha eneo hili ni mali ya wanakijiji kesho nendeni na wekeni Vibao vitakavyo onyesha eneo hili ni eneo  la Malisho na ogopa matapeli eneo hili haliuzwi!.

Nae Mwenyekiti wa sasa wa  kijiji hicho Bwana Yamat amesema anatambuq kuwa eneo hilo kama eneo la malisho na  kuwataka wananchi kijiji hicho kuwachukia watu waliouza eneo hilo la Malisho.

Hata hivyo wanachi hao walifikisha kero yao kwa Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Isack Joseph Copriano na  kumuomba awasaidie kurejesha eneo lililouzwa na watu wasio julikana.

Katika ziara hiyo Mbunge wa jimbo la Monduli amembatana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Mhe. Kisioki Moitiko.






Share To:

Post A Comment: