Kulikuwa na siku niligundua kuwa ukimya unaweza kuumiza kuliko maneno. Mimi na mke wangu tulikuwa tunaishi nyumba moja, tunalala kitanda kimoja, lakini mioyo yetu ilikuwa mbali sana.

Hakukuwa na ugomvi mkubwa, wala kelele kulikuwa na kimya kizito kilichokuwa kikinikandamiza kila siku.
Nilijaribu kuanzisha mazungumzo, lakini kila nilipofungua mdomo nilikuta ukuta.

Macho yake yalikuwa na machozi ambayo hayakumwagika, nami nikabaki na maswali yasiyo na majibu. Ndoa yetu ilianza kukosa mwelekeo, na siku hadi siku matumaini yalizidi kupungua.

Siku moja nilichukua ujasiri kuuliza kwa upole kama kuna kitu kinachomsumbua. Hakujibu mara moja. Ilimchukua muda, kisha akaniambia kuna jambo la zamani lililokuwa linamuumiza moyoni jambo ambalo halikuwahi kusemwa kwa miaka mingi.

Ukweli huo ulinishtua, lakini pia ulinifanya nitambue kuwa kimya chetu kilikuwa kimejengwa juu ya maumivu yaliyofichwa. Tulijaribu kujitatulia wenyewe. Tulizungumza, tukasikiliza, tukajaribu kusamehe.

Lakini bado kulikuwa na mzigo ambao ulituzuia kusonga mbele kikamilifu. Nilihisi kama tunazunguka pale pale, bila suluhisho la kudumu.

Ni hapo niliposikia ushauri wa kutafuta msaada wa nje msaada wa watu waliokuwa wamesaidia wanandoa wengine waliokuwa kwenye hali kama yetu.Soma Zaidi.
Share To:

Post A Comment: