Serikali ya India imeshatumia Dola za Kimarekani milioni 600 sawa na fedha za kitanzania Bilioni 1.4 katika kuwekeza miradi ya maendeleo hapa nchini ikiwa ni jitihada za kuiunga mkono serikali katika kuwaletea maendelea wananchi wake.
Fedha hizo ni kutoka na serikali ya India kutenga katika bajeti yake ya mwaka 2026/27 dola Bilioni 1.1 sawa na fedha za kitanzania shilingi Trioni 2.7 kwa ajili ya miradi yote ya maendeleo hapa nchini.
Fedha hizo Dola milioni 600 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo Afya,elimu,maji na barabara ikiwa ni njia mojawapo ya kuunga mkono utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha uongozi wake.
Hayo yalisemwa na Balozi wa India hapa nchini ,Bishwadip Dey katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama toka chanzo cha chemchem ya tono,Kijiji cha Losirwa kata ya Iloirienito Tarafa ya Ketumbeine Wilayani Longido Mkoani Arusha ambapo serikali ya India ilitoa shilingi milioni 125 katika mradi huo na watu zaidi ya 2000 kunufaika.
Balozi Dey alisema yeye hakwenda Longido kama mtalii bali ameenda Longido kama mwanafamilia kwa kwenda kuangalia miradi iliyoanzishwa na kumalizwa na nchi ya India kupitia wawekezaji wa nchi hiyo.
Alisema serikali ya India inaunga mkono jitihada za serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi wake maendeleo katika sekta zote na kwa kutambua hilo ndio maana serikali ya India imetenga fedha hizo ikiwa ni njia mojawapo ya kumuunga mkono kazi ya Rais kwa kupeleka fedha katika miradi sehemu mbalimbali kote nchini.
‘’Serikali ya India imepitisha bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo kote nchini na tayari dola milioni 600 zimeshatumika katika miradi hiyo ikiwemo miradi iliyopo Longido hiyo ni kumsaidia Rais kwa kazi nzuri anayoifanya kwa wananchi wake’’ alisema Balozi Dey
Aidha ameishukuru kampuni ya Dar Solution inayomilikiwa na mwekezaji kutoka nchini India kwa kuchangia vifaa vya Tehama vyenye thamani ya shilingi milioni 15 na kuwezesha ukamilishaji wa majengo ya shule shikizi katika kata ya Engikaret,Noondoto na Ketumbeine vyneye thamani ya shilingi milioni 30 na kusema kuwa hayo yote ni matunda ya serikali yao katika kuwahimiza wawekezaji kushirikiana na serikali ya Tanzania.
Balozi alisema na kuwaeleza wananchi wa kata ya Iloirienito juu ya mahitajitaji ya shule ya katika Kata hiyo na kusema kuwa watakwenda kuyafanyia kazi ili kata hiyo iwe na shule ya karibu kuondoa usumbufu kwa watoto kwenda umbali mrefu kusaka elimu huku wakikutwa na vikwazo vingi.
Naye Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido ,Dkt Steven Kiruswa alisema mradi wa maji uliozinduliwa na Balozi Dey umewezeshwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na yeye pamoja na wahisani toka kampuni ya kihindi ya Dar Solution ambayo ndio iliyonunuwa mabomba yote na matanki yaliyotumika kukusanya na kusambaza maji ya chemchem ya tono katika vitongoji vya Kisambi na Olomuki.
Kiruswa alisema na kuishukuru serikali ya India kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa serikali na wananchi wa Longido na kusema kuwa wao kama serikali ya Tanzania na wananchi wa Longido watashirikiana kwa hali na mali katika kufanikisha miradi ya manedeleo katika Jimbo hilo iliyoanzishwa na nchi hiyo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Longido,Salumu Kally pamoja na kumshukuru Balozi Dey pia aliwaomba wananchi wa Longido kutunza miradi hiyo ili iwajengee heshima kwa wahisani wawqeze kuendelea kusaidia miradi mingine wilayani huo.
Post A Comment: