Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesimama kwenye Jukwaa la Kampeni za Uchaguzi mkuu kwa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan akisema kazi kubwa imefanyika ndani ya miaka minne ya Uongozi wa Rais Samia, akisema Lindi Mjini ni kioo cha mafanikio makubwa yaliyotekelezwa Mkoani Lindi.
"Ndugu wana Lindi, Mgombea wetu leo yupo mbele yenu kuja kuomba kura za Chama Cha Mapinduzi na sisi tunakuja kusherehesha na kueleza sababu za yeye kupigiwa kura za ndio na ninyi Watanzania wenzangu ni mashahidi, nchi yetu imefanya vizuri sana, serikali imefanikiwa kuwahudumia watanzania katika mambo muhimu ya kila siku ikiwemo elimu, afya, maji, umeme, uwezeshaji na kila ambacho kinamgusa mwananchi."amesisitiza Mhe. Majaliwa.
Mhe. Majaliwa katika Mkutano huo wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini ameeleza kuwa Watanzania wanazo sababu nyingi za kukichagua Chama Cha Mapinduzi CCM ili kuleta muunganiko wa pamoja katika kuwahudumia watanzania, akizungumzia pia mradi wa gesi Mkoani humo huku akifurahishwa na waliohamia CCM hii leo kwakusema kuwa ni kweli kwamba Tanzania hakuna Chama cha Upinzani cha kuweza kupambana na Chama Cha Mapinduzi CCM.

Post A Comment: