Maneno hayo ameyasema Mh. Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu aliposhiriki Uzinduzi wa Mkakati wa Utekelezaji wa Makubaliano ya Mkataba wa Soko Huru la Bara la Afrika , uliofanyika katika Hotel ya Four Season, Dar Es salaam, ulioandaliwa na Wizara ya Viwanda na Buashara.

Katika hotuba yake , Waziri Kikwete aliipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kazi Nzuri wanayoifanya na kuwakumbusha umuhimu wa kutoa elimu ili iwafikie watanzania walio wengi na kuwezesha kuwatambulisha fursa na njia sahihi za kufikia malengo pangwa na serikali. Katika maelezo yake alionyesha nia ya kuwasaidia Watanzania kubadili fikra juu ya ufanyaji wa Biashara katika eneo huru la Biashara la Afrika.

Katika shughuli hiyo ambayo mgeni wa heshima alikuwa Dr. Selemani JAffo, Waziri wa Viwanda na Biashara aliwashukuru Mawaziri waliohudhuria na kuwaahidi kuendelea kushirikiana nao kuhakikisha wanafikia malengo kama ilivyoelekezwa na serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika hatua nyengine Dr. Jaffo ameitangaza tarehe 24 Mwezi Julai ya kila Mwaka kuwa siku maalum ambayo Wadau watakutana ili kujadili mafanikio na changamoto za utekelezaji wa mkataba huu.








Share To:

Post A Comment: