Wananchi wameamua kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha wanamlinda, kumtetea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa gharama yeyote Ile.

Hayo yamejidhirisha kwenye uzinduzi wa ofisi ya kwanza na ya kihistoria nchini ya TK Movement uliotokana na nguvu za Wananchi ambapo uzinduzi huo wa ofisi umefanywa na Afisa Tarafa Lisekese Emmanuel Shilatu kwenye Kijiji cha Miwale kilichopo Kata ya Msikisi.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Msikisi, Shilatu aliwasihi Wananchi kuongeza Utaifa, Uzalendo kwa Taifa lao la Tanzania kwa kujivunia Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kujivunia Serikali yao, kujivunia na kuyasema maendeleo yaliyopatikana nchini.

"Nawapongeza Wananchi wote kuhakikisha upatikanaji wa ofisi ya kwanza ya TK Movement. Ndugu zangu, akitokea Mtu akikwambia Tanzania tuna nini mwambie tuna amani, tuna maendeleo na tuna Rais Samia Mzalendo, Mchapa kazi, hodari, mtekelezaji na mfuatiliaji. Akikuuliza maendeleo yapi mpeleke muonyeshe miradi ya maendeleo ambayo ipo Kila sehemu kwenye sekta za afya, elimu, maji, miundombinu nk. Waonyesheni pembejeo za kilimo mnazopewa bure na Rais Samia. Hakikisheni mnawaeleza Watu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi CCM unaofanywa na Serikali" Alisema Shilatu.

"Tunapoelekea kwenye uchaguzi Mkuu huu wa kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais hakikisheni mnadumisha amani na utulivu lakini pia mjiepushe na vitendo vya rushwa." Alisisitiza Gavana Shilatu.

Nae Mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Rauphu Said amesema Wananchi wanajivunia Serikali yao napo tayari kuitetea na kumtetea Mhe. Rais Samia.

"Mimi kama kijana na Vijana wenzangu tunayaona maendeleo yanayoendelea kupatikana na kukua nchini yanayotupelekea kuamua kuitetea Serikali iliyopo Madarakani na kumlinda Rais Samia kwa wivu mkubwa." Alisema Rauphu.

TK Movement ni mtandao unaofanya kazi ya kuhamasisha Vijana na Wanawake katika ushiriki wao wa shughuli za maendeleo nchini ili kuchochea Kasi ya maendeleo katika Taifa letu.






Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo. Mgombea huyo wa NLD aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Chausiku Khatib Mohamed (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 10,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima(Picha na INEC).

 


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo. Mgombea huyo wa NLD aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Chausiku Khatib Mohamed (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 10, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu.

 


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Makini (MAKINI), Mhe. Coster Jimmy Kibonde. Mgombea huyo wa MAKINI aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Aziza Haji Suleiman (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 10, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima.

 


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Makini (MAKINI), Mhe. Coster Jimmy Kibonde. Mgombea huyo wa MAKINI aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Aziza Haji Suleiman (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 10, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu.

 Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewafikia wadau takriban 1,450 kwa utoaji wa elimu ya uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira katika Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane jijini Dodoma na Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya mwaka huu.


Elimu hiyo imetolewa kwa wadau kutoka sekta mbalimbali ikiwa ni sehemu ya juhudi za Baraza hilo kuhamasisha uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Katika banda lake la maonesho, NEMC ilielimisha kuhusu mbinu bora za kilimo hifadhi kinachozingatia mazingira, ufugaji endelevu, uvuvi salama pamoja na kulinda vyanzo vya maji.

Aidha, wananchi na wadau waliotembelea hapo walielimishwa kuhusu umuhimu wa kufanya tathmini ya athari kwa mazingira kabla ya kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo hususani ya kilimo ili kupunguza athari hasi kwa mazingira.

Miongoni mwa masuala yaliyopatiwa kipaumbele ni pamoja na kuwahimiza wawekezaji kusajili miradi NEMC ili kupata vyeti vya mazingira kama kigezo muhimu cha kuendesha shughuli zao kisheria na kwa kuzingatia mazingira.

Katika maonesho hayo, wataalamu wa NEMC pia walieleza athari za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja za shughuli za binadamu kama uchomaji moto hovyo, ukataji miti na utupaji taka kwenye mifumo ya ikolojia, hali inayochangia mabadiliko ya tabianchi, mmomonyoko wa ardhi na upungufu wa rasilimali maji.

“Tunawahimiza wawekezaji kushiriki kikamilifu katika kulinda mazingira. Elimu tunayoitoa ni msingi wa kufanya maamuzi sahihi ya kisera, kiuchumi na kijamii yanayozingatia mustakabali wa mazingira yetu,” alisema Bi. Dalia Kilamlya, Afisa Mazingira NEMC

Kwa ujumla, mwitikio wa wadau mbalimbali katika kupata elimu ya mazingira kutoka NEMC umetajwa kuwa mkubwa na wenye kuleta matumaini ya mabadiliko chanya katika namna jamii inavyoshiriki kwenye kulinda na kuhifadhi mazingira.




 Mgombea urais kupitia Chama Cha Makini, Coaster  Kibonde, amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), huku akiahidi iwapo watanzania watamchagua kila kijana wa Kitanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 21 atapewa ekari  tano za ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo.

Kibonde anakuwa mgombea wa nne kuchukua fomu akitanguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Dkt Emmanuel Nchimbi (CCM)  Kunje Ngombare Mwiru na Chumu Abdallah Juma ,Chama cha Wakulima (AAFP) na Hassan Almas na Ally Hassan (NRA).

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Kibonde ambaye aliambatana na mgombea mwenza wake, Bi. Azza Haji Suleiman, amesema kuwa serikali yake inalenga kuwahamasisha vijana kuingia kwenye kilimo cha kisasa chenye tija, badala ya kutegemea kilimo cha jadi ambacho  hakina manufaa ya kudumu.

 “Tutafanya kilimo cha umwagiliaji ili kuachana kabisa na kilimo cha kutegemea mvua ambacho ni kilimo cha umasikini. Maana ya Chama Makini ni Maarifa,kila kijana tutampatia ekari 5 kwa ajili ya kulima kwa kutumia matrekta,  amesema Kibonde.

Amevitaja vipaumbele vya Chama hicho ni elimu, Kilimo na Afya lengo likiwa ni kuhakikisha wanaondoa umaskini kwa watanzania.

Kibonde alisisitiza kuwa elimu itakuwa kipaumbele cha kwanza katika utawala wake huku akiweka  mkazo mkubwa katika kuhakikisha kila kijana wa Kitanzania anapata elimu ya kiwango cha kimataifa.

 “Ukimnyima Mtanzania elimu ni sawa na kumfunga gerezani maisha. Sisi tutalivalia njuga suala la elimu tutahakikisha elimu inayopatikana duniani kote inamfikia kijana wa Kitanzania,” amesema Mgombea huyo

Kwa upande wa afya, Kibonde amesema serikali yake itaweka mkazo mkubwa katika kuimarisha huduma za afya nchini kwa kujenga hospitali katika kila kata pamoja na kuzipatia vifaa tiba vya kisasa.

“Ukimnyima Mtanzania afya ni sawa na kumhukumu kifo tutahakikisha tunakuwa na wataalamu wa kutosha kwa sababu tutawekeza sana katika elimu ya afya,” alisema.

Alitangaza pia kuwa serikali yake itaanzisha bima ya afya kwa wote itakayojulikana kama MakiniCare, ambayo italenga kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya bila ubaguzi.

Vyama vingine vinavyotarajiwa kuchukua fomu leo ni National League (NLD) na United People Democratic  (UPDP).



 


Naitwa Sonia kutokea Tanga, niliolewa mwaka 2010 huku huku Mombasa nikiwa kama mke wa pili kwa mume wangu ambaye mke wake wa kwanza alikuwa ameshajaliwa naye watoto wawili.

Hii ni ndoa ambayo nilipitia mambo mengi sana kiasi kwamba kamwe siwezi kuja kusahau kabisa maishani mwangu, hiyo ni kutokana sikuweza kubeba ujauzito mapema kama ambavyo mume wangu alitarajia.

Baada ya miaka kama mitatu ndani ya ndoa, mume wangu alianza kupunguza mapenzi aliyokuwa akinipa na kunionyesha kama mke mdogo, mara nyingi alikuwa akikaa zaidi na mke mkubwa. Soma zaidi hapa 


 

Kwa miaka minne ya ndoa yangu, nilikuwa kama mgeni ndani ya nyumba yangu mwenyewe. Mume wangu alikuwa tajiri wa kutupwa anaendesha biashara kadhaa jijini Mwanza, anamiliki magari ya kifahari na hata nyumba kadhaa.

Lakini pamoja na utajiri wake wote, hajawahi kunipa hata shilingi mia moja kwa hiari. Kila mara nilipohitaji hela ya matumizi au hela ya kwenda saluni, ilikuwa lazima niombe kwa unyenyekevu hadi nahisi kama ombaomba. Hata nguo zangu nyingi zilinunuliwa na dada zangu au marafiki walionionea huruma.

Kwa nje tulionekana familia ya kupendeza. Tulivalia vizuri, tuliishi kwenye nyumba nzuri, lakini ndani ya moyo wangu kulikuwa na kilio kisicho na sauti. Nilishindwa kuelewa kwa nini mume tajiri kabisa anaweza kuwa na roho ngumu kiasi cha kuniangalia nikihangaika, wakati pesa iko mezani kwake.

Nilijaribu kila njia kumvutia: kumpikia vizuri, kumjali, kumpa heshima, hata kumletea zawadi ndogo ndogo. Lakini moyo wake ulionekana kuwa na barafu badala ya upendo. Alikua mpole lakini mkavu hakuwa katili, lakini hakuwa pia mtu wa kuonyesha mapenzi au ukarimu. Soma zaidi hapa 

  


Nilikuwa nimekata tamaa kabisa ya maisha. Kila asubuhi ilikuwa mzigo mwingine wa kuamka, na usiku nilijikuta nikilia kimya kimya bila sababu. Watu waliniona kama mtu mwenye huzuni ya kawaida au hata msongo wa mawazo, lakini ndani yangu nilihisi kitu tofauti kabisa. Sikuwa mimi yule niliyekuwa kabla mwenye matumaini, furaha na ndoto nyingi. Hali hii ilianza ghafla, bila tukio kubwa la maisha kuichochea. Nilidhani ni msimu tu wa huzuni, lakini kila siku iligeuka kuwa vita ya kiakili na kimwili.

Nilianza kujitenga na marafiki, nikakosa hamu ya kula, na mara nyingi nilitaka tu kulala au kutoweka. Nilipokwenda hospitali, madaktari walinitaja kuwa na ‘depression ya kiwango cha chini’. Nilijaribu dawa na ushauri nasaha, lakini hakuna kilichonisaidia kabisa. Ndipo nilianza kuhisi labda kuna kitu zaidi ya afya ya akili kitu kisichoonekana kwa macho.

Nilipoanza kuuliza na kuchunguza kwa kina, dada mmoja aliyekuwa rafiki wa karibu alinieleza jinsi hali kama yangu inaweza kuwa matokeo ya nguvu za kiroho hasa uchawi wa kunifanya nijinyime maisha.

Aliniambia pia jinsi watu huweza kuwekewa vitu ili washindwe kuendelea na maisha yao, wakate tamaa, na kujiua hata bila kuelewa kwa nini. Sikuchukua kwa uzito mwanzoni, hadi alinielekeza kwa Kiwanga Doctors ambao husaidia watu waliopitia hali kama yangu. Soma zaidi hapa 

  

Nilikuwa nimekaa mbele ya kioo, nikiangalia pua yangu, ngozi yangu yenye madoa na mdomo wangu uliokuwa mwembamba. Sikuwa najipenda. Kilichoniumiza zaidi ni maneno aliyoniambia mtu niliyempenda kwa moyo wangu wote: “Wewe si mrembo, na huwezi kuwa mrembo bila kufanya upasuaji.” Alikuwa mpenzi wangu wa miaka miwili, lakini siku hiyo alikatiza uhusiano wetu kwa kauli hiyo ya kikatili.

Toka utotoni nilikuwa na matatizo ya kujiamini. Nilichekwa sana shuleni, wenzangu waliniita majina kama “kiatu cha mguu mmoja” na “uso wa ndoo.” Nilijua sina ngozi laini kama ya wenzangu, nilikuwa na chunusi za mara kwa mara na nywele zangu hazikuwa laini wala zenye mvuto.

Nilipokuwa mtu mzima, nilijaribu bidhaa nyingi scrubs, serums, hata vipodozi vya bei ghali vilivyosemekana vinatoka Ulaya lakini hakuna kilichobadilika.

Kipindi nilipoingia kwenye uhusiano huo, nilidhani nimempata mtu wa kunikubali jinsi nilivyo. Kwa muda fulani alionyesha kunijali, lakini baadaye alianza kuniambia nivae makeup nene au nijifunge shungi kuficha uso. Mwisho wa yote, akaniambia ukweli wake: siwezi kuwa mrembo kwa hali yangu ya asili. Alinitaka nifanye upasuaji wa sura. Soma zaidi hapa 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Innocent Bashungwa amesema Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza kimeeleza mpango wa kuanzisha kituo cha umahiri cha utoaji wa mafunzo kwa wafungwa ili kuwapa maarifa, ujuzi na stadi za biashara zitakazowawezesha kujikimu kiuchumi pindi wanapomaliza vifungo vyao na kutoa wito wa kuhakikisha maandalizi ya kituo hicho yanafanyika.

Ameyasema hayo  Agosti 6, 2025 katika hafla ya kutunuku vyeti vya ujasiriamali na stadi za biashara kwa wafungwa, iliyofanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Arusha.

Waziri Bashungwa pia amempongeza Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka kwa namna anavyosimamia chuo, ubunifu alionao, maono ya kutafsiri mahitaji ya jamii na taaluma zinazotolewa chuoni, na mafanikio makubwa aliyoleta katika upande wa michezo. Aidha, Waziri Bashungwa ameishukuru IAA kwa ushirikiano ambao imeutoa kwa Jeshi la Magereza katika programu ya mafunzo ya ujasiriamali na stadi za biashara yaliyotolewa kuanzia Mei 7, 2025 kwa wafungwa takribani 170 wakiwemo wanawake 41 na wanaume 129.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza CGP Jeremiah Katungu amemshukuru Prof. Sedoyeka kwa maono ya ushirikiano katika utoaji wa mafunzo hayo, akisema kuwa tangu mashirikiano na IAA kumekuwa na matokeo chanya ikiwemo mahafali hayo ya kwanza ya wahitimu wa mafunzo ya ujasiriamali na stadi za biashara yaliyotolewa kwa wafungwa.

 Aidha, CGP Katungu amesema mafunzo yatawafanya wahitimu kuwa wema, wenye maarifa na kuwataka kutumia mafunzo kuanzisha shughuli mbalimbali za kuwaingizia kiptao watakapomaliza vifungo vyao.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka amesema mafunzo hayo yameanzishwa kwa kutumia uhalisia wa mazingira, mahitaji ya washiriki, ambayo yalihusisha vipindi vya nadharia na vitendo juu ya stadi za uanzishaji biashara kisheria, ujasiriamali, vyanzo vya mitaji, usimamizi wa fedha pamoja na utafutaji wa masoko na mazingira ya kufanyia biashara; eneo ambalo IAA ina uzoefu mkubwa kitaaluma na kiutendaji ili kuwawezesha wafungwa kupata ujuzi wa kujitegemea mara baada ya kumaliza vifungo vyao.

Aidha, Prof. Sedoyeka ameongeza kuwa IAA kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza nchini wamejipanga kupanua programu hii kwenye magereza mengine, kutoa vifaa vya kuanzisha biashara, kusaidia wahitimu kupata mitaji kupitia mamlaka za serikali za mitaa na kutoa mafunzo endelevu na msaada kwa wafungwa waliohitimu mafunzo. 

Pia, Prof. Sedoyeka ametoa rai kwa wahitimu kutendea haki fursa hii ya mafunzo waliyoyapata.












 


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Innocent Bashungwa amempongeza Mkuu wa Chuo-IAA, pamoja na menejimenti nzima kwa namna anavyosimamia chuo, umahiri na ubunifu wake katika sekta mbalimbali ikiwemo mashirikiano aliyoanzisha na Jeshi la Magereza katika kutoa mafunzo ya ujasiriamali na stadi za biashara kwa wafungwa.

“Kama Mkuu wa Chuo pamoja na timu yako naomba tuwapongeze na tuwashukuru kwa ushirikiano, ambao mnalipa Jeshi la Magereza Katika hii programu ambayo leo hii tunatunuku wahitimu 170” amesema

Waziri Bashungwa ameyasema hayo Agosti 6, 2025 katika hafla ya kutunuku vyeti vya ujasiriamali na stadi za biashara kwa wafungwa waliohitimu mafunzo ya ujasiriamali na stadi za biashara yaliyotolewa na Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza, hafla iliyofanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Arusha

Aidha, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza CGP Jeremiah Katungu amesema ana imani kubwa kuwa wahitimu wa mafunzo hayo wamepata elimu na maarifa muhimu, yatakayowawezesha kuwa wabunifu na wajasiriamali mahiri pindi watakapomaliza vifungo vyao na kwenda kwenye jamii.

“lengo la mafunzo ni kuwaandaa na kuwarejesha kwenye jamii wakiwa raia wema na wenye uwezo wa kuendesha shughuli za kiuchumi” amesema

Naye, Mkuu wa Chuo-IAA Prof. Eliaman Sedoyeka amemshukuru CGP Katungu kwa mashirikiano mazuri na IAA katika urekebishaji wafungwa, kupitia utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali na stadi za biashara na kutoa rai kwa taasisi zingine za elimu, mashirika ya kiraia na taasisi binafsi kushirikiana na IAA katika kuhakikisha wafungwa wanapata ujuzi na maarifa.

Nao, baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo yaliyoanza Mei 7, 2025 wamepongeza  viongozi wote na walimu kutoka IAA kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali na stadi za biashara, wakisema italeta tija kwao kiuchumi baada ya kumaliza vifungo vyao.




NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekutana na kuwapa elimu wafanyabiashara wadogowadogo wanaofanya shughuli zao ndani ya mkuza wa bomba la gesi asilia katika eneo la Kinyerezi Mwisho, Mtaa wa Kanga na Kibaga ili kuweza kuondoka eneo hilo ambalo sio rasmi na salama kwa shughuli zozote za kibinadamu ikiwemo kufanya biashara.



Dodoma, Agosti 7, 2025


Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet R. Lekashingo, ameongoza ujumbe wa Tume kutembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Dkt. Lekashingo ameambatana na Makamishna wa Tume, Mhandisi Theonestina Mwasha na Dkt. Theresia Numbi, pamoja na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo. 

Wakiwa katika banda hilo, wamepata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tume, ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini, taratibu za upatikanaji wa leseni, biashara ya madini, uongezaji thamani madini, pamoja na usimamizi wa mazingira katika shughuli za uchimbaji.

Akizungumza na maafisa wa Tume na wananchi waliotembelea banda hilo, Dkt. Lekashingo amewapongeza watumishi wa Tume kwa kazi nzuri ya kutoa elimu na huduma kwa umma. 


Amesisitiza umuhimu wa kutumia maonesho hayo kama jukwaa la kuelimisha na kuhamasisha Watanzania kushiriki kikamilifu katika Sekta ya Madini, hususan kupitia uongezaji thamani madini na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyopo.

“Ni muhimu wananchi wakapata uelewa mpana kuhusu namna wanavyoweza kunufaika na rasilimali za madini zilizopo nchini iwe ni kupitia uchimbaji, biashara, uongezaji thamani au utoaji wa huduma kwenye migodi. Sekta hii ina mchango mkubwa katika Pato la Taifa na ajira kwa Watanzania,” amesisitiza Dkt. Lekashingo.

Kwa upande wao, Makamishna wa Tume wameeleza kufurahishwa na mwitikio mkubwa wa wananchi kutembelea banda la Tume na kuonesha dhamira ya kujifunza zaidi kuhusu Sekta ya Madini, jambo linalodhihirisha hamasa na mwamko chanya wa Watanzania kushiriki kwenye sekta hiyo muhimu.

Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, amewataka maafisa wa Tume kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kulingana na mahitaji ya wadau waliopo katika maonesho mbalimbali nchini.

“Yapo madini yanayotumika kama mbolea, na pia zipo fursa nyingi za usambazaji wa bidhaa za kilimo kwenye migodi. Ni muhimu wananchi wakafahamu fursa hizi na kushiriki kikamilifu ili Sekta ya Madini iendelee kuwa kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi na mchango wake katika Pato la Taifa uongezeke,” amesema Mhandisi Lwamo.

Tume ya Madini ni miongoni mwa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini zinazoshiriki kikamilifu katika Maonesho ya Nane Nane mwaka huu, ikiwa na lengo la kuelimisha umma kuhusu Sekta ya Madini, kuonesha mafanikio yaliyopatikana, pamoja na kuhamasisha uwekezaji zaidi katika sekta hiyo kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.