Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makalla amesema kuwa Julai 26 2025 ndiyo siku ambayo Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itafanya kikao chake cha kawaida, badala ya jana au leo kama ilivyotarajiwa hapo awali. 

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama cha Mapinduzi CCM.

"Wagombea ni wengi sana, kwa hiyo kazi ya kuchambua ni kubwa na sisi tunataka tutende haki na tuifanye kwa umakini. Kwa hiyo uteuzi wa mwisho utafanyika tarehe 28 na baada ya hapo kwenda kwenye kura za maoni." Alisema

Aidha, amesema kikao hicho cha kawaida kitatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kitakachofanyika siku hiyo hiyo ya Julai 26, 2025. 

Makalla amesema kuwa, baada ya vikao hivyo kitafanyika kikao kingine cha Kamati Kuu ya CCM Taifa Julai 28, 2025 ambacho ni mahususi kwa ajili ya uteuzi wa wagombea wa chama hicho ngazi ya ubunge na udiwani watakaopeperusha bendera ya CCM.

Share To:

Post A Comment: