Sitamsahau yule jirani yetu wa apartment ya pili. Alikuwa mrembo kweli, siwezi kukataa. Mchongoo, rangi ya chungwa, sauti ya kupendeza, na alijua kuvaa. Lakini sikuwahi kufikiria kuwa ataingia kwenye ndoa yangu kama mchwa wanaovamia kuni taratibu.
Nilikuwa na mume ambaye tulianza maisha bila chochote. Tulijenga pamoja. Tulihangaika. Lakini baada ya kupata kazi nzuri, maisha yakabadilika na yeye pia akabadilika.
Ilikuwa inaanza kwa kuchelewa kurudi nyumbani. Mara simu imejaa password. Mara ni busy na kazi. Nilijaribu kuuliza kwa utulivu lakini alinijibu kwa ukali.
Akasema mimi ni mtu wa mashaka na sina imani. Siku moja niliamka alfajiri nikamkosa kitandani. Simu yake ilikuwa mezani. Nilipotoka nje, nikaona viatu vyake kwa mlango wa jirani. Sikuamini macho yangu. Nilirudi chumbani nikapiga magoti. Nikalia kimya kimya hadi jua lilipochomoza.
Nilichoka, lakini sikuongea. Nilinyamaza. Nilikuwa na machungu lakini sikuwa na nguvu ya kupigana na mwanamke mwingine. Nilikuwa na hofu ya kuvunja ndoa. Nilianza kupoteza uzito. Nilikuwa kimya lakini moyo wangu ulikuwa unapigwa mapigo ya maumivu. Soma zaidi hapa.
Post A Comment: