MKUU wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi amepiga marufuku "faini ya funguo"utozwaji ya sh, 30,000 inayotozwa baada ya mmiliki wa eneo husika kushindwa kulipa kodi mbalimbali ikiwemo kodi ya leseni na kodi ya huduma, zinazotozwa na halmashauri ya Jiji la Arusha kutokana na wafanyabiashara hao, kushindwa kulipa kodi hizo kwa wakati.
Rc Kihongosi amepiga marufuku hiyo wakati akizungumza na wamiliki,wafanyakazi na watumishi Jiji hilo ili kubaini changamoto zao na kutafuta majibu sahihi ikiwemo utunzaji wa amani ikiwemo usafi wa maeneo wanayofanyia kazi.
Amesema watakaothibitika kuchukua sh, 30,000 za faini za funguo kwa watumishi wa idara ya biashara kumi na moja waliopo Jiji la Arusha watachukuliwa hatua za kisheria kwani huo ni ukandamizaji kwa wananchi hao ambao wanaendesha maisha kupitia saluni wanazofanya kazi.
"Hii faini ya funguo haikubaliki sasa ukifunga saluni na kudai hela hizo kwa mwezi ni shilingi ngapi tutachukua hatua na lakini naagiza Jiji la Arusha kutenga maeneo ya wafanyakazi wa saluni ili kuhakikisha kila mmoja anapata riziki badala ya kugombana"
Alisema watu wa saluni ni kada nzuri yenye wateja wengi hivyo wanapoona kunahabari tofauti za wateja wao watoe taarifa kwa serikali ili hatua ziweze kuchukuliwa na kusisitiza kulinda amani kwa kutoa viashiria ambavyo havijakaa sawa kwani amani ya nchi ni tunu pekee.
Alisisitiza waajiri wa saluni kutoa mikataba ya ajira huku akisema Jiji la Arusha lina shilingi bilioni 5.5 kwaajili ya utoaji mikopo ya asilimia kumi inayotolewa serikali kwa vijana, wanawake na makundi maalum kwaajili ya kupata mikopo hiyo ili wajikwamue kiuchumi ambapo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, John Kayombo alisisitiza elimi hiyo kuendelea kutolewa ili watu mbalimbali waweze kupata mikopo
Awali baadhi ya wafanyakazi na wamiliki wa saluni akiwemo Rose John mwenye kibanda namba 133 eneo la stendi ndogo aliweza kupewa umiliki halali wa kibanda chake baada ya awali kuzunguushwa na aliyekuwa mmiliki wa eneo hilo na kumpa notisi ya kuhama ilhali alikuwa akilipa kodi halali ya eneo alilopangishwa kwa mmiliki wake.
Pia Thedy Mchome aliomba suala la upimaji afya kwa wafanyakazi lichukuliwe kwa uzito wake na wanapotaka kulipa fedha za wafanyakazi kwaajili ya upimaji wapewe controo namba kwa wakati ili waondokane na usumbufu na kuomba kodi wanazotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuhakikisha zinaendana na uhalisia wa biashara zao wanazofanya
Post A Comment: