NA DENIS MLOWE IRINGA
MKURUGENZI wa Masoko na Uzalishaji wa kampuni ya VunjaBei Fadhili Ngajilo ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Iringa Mjini katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza na wanahabari mjini Iringa, Ngajilo ambaye ni Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Iringa ametangaza nia hiyo kwa kuweka vipaumbele 10 endapo atachaguliwa na wajumbe na kupewa nafasi ya kugombea jimbo la Iringa mjini.
Ngajilo ambaye ameshatia nia kupitia Ccm kwa miaka 3 katika miaka ya 2010, 2025 na sasa 2025 na kuleta upinzani mkubwa ndani ya chama katika kura za maoni katika jimbo la Iringa mjini ametangaza pia kupumzika kwa muda nafasi ya uenyekiti wa wazazi mkoa.
"Nimeandika barua kwa chama changu ya kupisha kwa muda nafasi yangu ya Mwenyekiti wazazi mkoa wa lringa ili kuruhusu vikao vikao vya uchaguzi viendelee kwa sababu mimi nimetia nia ya kugombea ubunge jimbo fa Iringa Mjini na ni matumaini yangu kuwa chama na wanachama wenzangu wa CCM wataniamini kuwa ninaweza kubeba majukumu, lakini pia ni matumaini yangu kuwa wananchi wa jimbo la Iringa mjini watanipokea na kunikubalia kuwa Mbunge wao kwa kipindi cha 2025 hadi 2030."
Aliongeza kuwa Imani huzaa Imani kuamini katika uwezo wa kuongoza kutokana na makuzi na malezi mazuri niliyoyapata ndani ya CCM kwa za zaidi ya miaka ishirini huku akishika nafasi mbalimbali ndani ya CCM na serikalini.
Akitangaza sababu za msingi za kuweka nia ya kugombea ubunge Iringa Mjini kwa mwaka 2025 alizitaja kuwa kutimiza wajibu wa kikatiba wa kugombea na kuchaguliwa kwa kuwa sifa na nia zote anazo na kuwa mwakilishi wa wananchi bungeni.
Alisema lengo la kutia nia ni baada ya kubaini kuwa Iringa mjini inahitaji "voice of the people" (sauti ya watu) ambayo ikisema jambo bungeni au popote basi ijulikane kuwa Iringa imesema jambo na kuongeza kuwa vita vya kiuchumi zinahitaji watetezi na watu wenye uwezo wa kujenga hoja kuvutia miradi na uwekezaji katika sekta za viwanda, biashara,
"Sauti hii inahitajika kuwaunganisha wana Iringa kwa rika, jinsia na imani zao yaani watoto, vijana, wazee, wanaume na wanawake mimi Ngajilo nimejipima nimeona hili naliweza na kama mjuavyo wote kuwa sisi wakazi wa lringa Mjini tuna shughuli za mbalimbali zikiwemo kilimo, biashara/ ujasiriamali tunahitaji sauti ya mtu atakayewaunganisha wakulima na kutimiza ndoto zao, vivyo hivyo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kama wauzaji masokoni, machinga, mama na baba lishe, maafisa usafirishaji kama bodaboda, bajaji, daladala na mawakala katika stendi zetu za mabasi, bila kuwasahau mafundi mbalimbali wa nguo, vifaa vya mbao,vipuri vya magari,. Alisema
Aliongeza kuwa Iringa mjini inahitaji kiongozi mbunifu, msikivu, mwenye upendo wa dhati na wana Iringa mzalendo na anayeweza kukaa na wana Iringa wakabuni na kupanga mikakati mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali hivyo nimejipanga vilivyo kuwatumikia wananchi kwa moyo wa dhati, moyo wa utumishi na kuwa mtumishi wa watu (servus populi) endapo nitapewa ridhaa.
lringa Mjini imesheheni Vyuo vikuu ni mji wa vyuo vikuu inahitaji mbunge aliyejaa uelewa wa mahitaji ya vyuo vikuu na elimu. mbunge anayeweza kuwaunganisha wana vyuo kuweza kuwa na mchango wa kiuchumi na kijamii kwenye mkoa wetu wa Iringa kwa kuwa ujuzi wa kuishi na kustawisha vyuo vikuu.
Ngajilo aliongeza kuwa lringa Mjini inahitaji mtu anayeamini katika kuweka mifumo ya usalama wa wananchi wote
wakiwemo watoto, wanawake, wazee na vijana kuna matukio ya unyanyasaji Kuvunja haki za wengine aidha kuna maeneo vibaka na wezi wameshamiri hivyo kwa umoja na jamii uwezo ninao na kuweza kuwaaunganisha wana Iringa kuzuia unyanyasaji na uhalifu kwa vitendo.
Vile vile alisema kuwq jimbo la Iringa mjini linahitaji kiongozi anayetambua maana ya kuweka mifumo ya burudani na michezo kwani kwa kipindi cha miaka 15 nimewaunganisha wadau wa sekta hiyo kwa kuendesha kombe la NGAJILO CUP (Vunjabei Cup) kupitia taasisi ya NGAJILO Foundation.
Alisema Iringa tunahitaji timu ya Ligi kuu hivyo nimejipanga na nina mikakati madhubuti ya kurudisha heshima ya Iringa katika medani ya michezo na kutambua uwepo wa makundi mengine ya burudani kama mabondia, madansa, wasanii.
Kigezo kingine ni Iringa Mjini bado tuna changamoto za miundombinu ya barabara hasa kata za pembezoni mwa manispaa yetu hivyo anahitajika mtu jasiri wa kusukuma agenda ya miundombinu ambapo yupo tayari kulipambania hili ili libakie kuwa historia.
Akizungumzia Agenda ya utalii kwa Iringa ni muhimu sana kwa kuwa imezungukwa na vivutio vya utalii vingi kama Ruaha NP, Isimila S.A.S, Kalenga H.S, nk. Uwanja wa ndege mzuri, Hali ya hewa, makampuni ya utalii, ukarimu wa wana lringa ni vigezo tosha kuvutia watalii wa kitaifa na kimataifa kuja lringa kukumbusha kuwa Iringa mjini kuwa katikati ya mikoa na vijiji vingi fursa inayohitaji mtu mbunifu kuitumia ili kuwanufaisha wana lringa Mjini
Alimalizia katika huduma za afya na elimu, pamoja na kuendelea kuimarika kimiundombinu lakini changamoto ni nyingi kwenye utoaji wa huduma zinahitaji msukumo mpya kuhakikisha wana lringa Miini wanapata huduma bora kwa kuona hilo amejipima na kuona hii changamoto ipo ndani ya uwezo wangu.
Post A Comment: