Zaidi ya shilingi milioni 450 zimepelekwa katika Jimbo la Longido Mkoani Arusha kwa ajili ya kumalizia miradi ya afya katika Jimbo hilo ili kuwaondolea usumbufu wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya matibabu.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido,Dkt Steven Kiruswa katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika Tarafa ya Longido kata ya Kimokowa na Namanga na kusema kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inawajali na kuwathamini wananchi wa Longido.
Dkt Kiruswa alisema fedha hizo ni fedha maalumu ambazo zimetolewa na serikali nje ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 na zimelenga pekee yake katika sekta ya afya kumalizia ujenzi wa zahanati na vituo vya afya katika baadhi ya kata wilayani Longido.
Alisema kuna kata vituo vya afya vilianza kujengwa kwa michango ya wananchi na mchango wake binafsi Mbunge lakini miradi hiyo haikuweza kukamilika kutokana na juhudi za Mbunge kuomba fedha serikali na serikali imeona umuhimu wa kutoa fedha hizo ili kumalizia miradi hiyo na kuondoa adha kwa wananchi kufuata huduma umbali mrefu bila sababu za msingi.
Mbunge Kiruswa alisema katika Kata ya Mundarara zilipelekwa shilingi milioni 250 kwa ajili ya kumalizia Zahanati ya kisasa iliyojengwa katika kata hiyo yenye msongamano mkubwa wa watu kwa kuwa kata ya Mundarara imebarikiwa kuwa na madini ya ruby hivyo kuna wananchi wengi kutoka maeneo mbali mbali ya nje ya wilaya ya Longido hivyo kuwa na uhitaji mkubwa wa zahanati.
Alisema katika Tarafa ya Ketumbeine Kijiji cha Losuruway zanahati ya kisasa imejengwa na imekamilika lakini ilikuwa haina nyumba ya daktari hivyo serikali ilitoa shilingi milioni 45 kumalizia ujenzi wa nyumba hiyo sambamba na kata ya Loirienyito kituo cha afya kimepelekwa fedha shilingi milioni 45 kumalizia ujenzi wa kituo hicho cha afya.
Naibu Waziri Kiruswa alisema kata ya Kimokowa Tarafa ya Longido zimepelekwa shilingi milioni 45 kuendeleza na kumalizia zanahati iliyojengwa katika kata hiyo sambamba za shilingi milioni 30 zilizopelekwa kata ya Noondoto Kijiji cha Ngusero kumalizia ujenzi za Kituo cha afya,shilingi milioni 30 kupelekwa Kijiji cha Naadale kumazilia ujenzi wa kituo cha afya.
Alisema katika fedha hizo pia shilingi milioni 30 zimepelekwa katika Kijiji cha Wosiwosi kilichopo Tarafa ya Ketumbeini kumalizia ujenzi wa kituo cha afya ambapo awali wananchi na mbunge walianzisha ujenzi wa kituo hicho na serikali imewakumbuka na kutoa fedha kwa ajili ya umaliziaji wa kituo hicho.
Dkt Kiruswa alisema kuwa wananchi wa Jimbo hilo wanamshukuru sana Rais kwa uamuzi wake wa kutoa fedha kwa ajili ya umaziaji wa zahanati na vituo vya afya katika baadhi8 ya kata na kusema kuwa huo ni uamuzi ulioshukuruliwa kwa akiasi kikubwa na wananchi wa Jimbo la Longido.
Mbunge huyo yuko katika ziara ya siku nne katika Jimbo la Longido kueleza miradi iliyotelekezwa na serikali na mchango wake kama mbunge kwa wananchi wa Jimbo hilo na kueleza ahadi alizoahidi ambazo amezitekeleza kwa asilimia mia moja.
Post A Comment: