Articles by "LONGIDO"
Showing posts with label LONGIDO. Show all posts


KAMPUNI ya Kimataifa ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Barrick Gold kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Kiseriani kata ya Engikaret wilyani Longido Mkoani Arusha,Mbunge wa Jimbo hilo,Dkt Steven Kiruswa na serikali wamefanikiwa kujenga shule shikizi kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 230.

Akizungumza katika uzinduzi wa shule hiyo Kijiji hapo ,Meneja Mkazi wa Barrick{Country Manager} Tanzania ,Melkiory Ngido alisema uamuzi wa kampuni hiyo kuchangia msaada ni kufuatia maombi ya Kiruswa ambaye ni Naibu Waziri wa Madini na kujionea wenyewe hali ya changamoto za wanafunzi kutembea km 32 kwenda na kurudi shule  hali inayoleta hatari kwa wanafunzi hao kwa wanyama wakali.

Ngido aliwaahidi wananchi Kiseriani na Longido kwa ujumloa kuwa Barrick Gold itashirikiana na wananchi katika kujenga miundombinu ya elimu kwa kuwa wananchi wameonyesha nia ya dhati na ushirikiano na uadilifu mkubwa katika ujenzi wa madarasa mawili na 0fisi ya mwalimu kwani kampuni hiyo imechangia zaidi ya shilingi milioni 180 na zimetumika kama ilivyokusudiwa.

Alisema elimu ni msingi wa maisha na wananchi wa Kijiji cha Kiseriani ambao wengi wao ni wa jamii ya kifugaji ya Kimasai kuamua wenye kujitoa na kujenga madarasa mawili na ofisi ya mwalimu ni uamuzi unaopaswa kuungwa mkono kwa kuwa jamii hiyo imeamua kujitoa na kuwajali wanafunzi wa jamii hiyo na kujali elimu zaidi na sio vinginevyo.

‘’Barrick Gold Mining imeaamua kujitoa zaidi Longido kuhakikisha elimu inasogezwa zaidi katika maeneo ya makazi ya watu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha miundombinu ya elimu ikiwemo madarasa,ofisi na nyumba za walimu zinajengwa kwa maslahi ya watoto wa jamii hiyo’’alisema Ngido

Naye Kiruswa aliishukuru kampuni hiyo kwa uamuzi wa ujenzi wa madarasa na ofisi ya mwalimu na kuahidi ushirikiano zaidi na kusema kuwa uamuzi huo unapaswa kupongezwa na wananchi wote wa Longido na kusema kuwa uadilifu ni jambo muhimu katika kuwashawishi wafadhili wengine kujitoa katika kutoa misaada ya miundombinu ya elimu,maji na barabara.

Alisema uamuzi wa ujenzi wa madarasa mengine mawili ulioazwa na wananchi kwa kusomba mawe,mchanga na kokote ni uamuzi wenye busara kubwa na yeye ataunga mkono kwa hilo kwa kutoa mifuko 100 ya simenti na kumalizia upauaji.

Waziri Kiruswa alisema na kuwaomba wana Kiseriani na Longido kwa ujumla kujitoa katika shughuli za kijamii ikiwemo ujenzi wa miundoimbinu ya elimu na kusema kuwa yeye kwa hilo atakuwa mstrari wa mbele katika kuchangia na kusaka wafadhili zaidi .

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} wilaya ya Longido ,Papa Nakuta amempongeza Kiruswa kwa jinsi anavyojitoa kwa maendeleo ya wananchi wa longido na kuwataka wananchi kumuunga mkono mbunge huyo ambaye ameenda bungeni kufanya kazi na sio kulala kwani kila mradi mchango wake upo kama sio yeye basi analeta marafiki zake na kufanya ushawishi kwa serikali kuendelea kupeleka fedha za miradi Jimbo hapo.
















JUHUDI za wananchi wa kitongoji cha Lailupa katika Kijiji cha Meirugoi Kata ya Gelai-Meirugoi wilayani Longido Mkoani Arusha za kujitoa na kujenga darasa la shule ya awali {chekechea} kwa gharama ya shilingi milioni 12 kumemuibua Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Steven Kiruswa kuamua kumalizia ujenzi wa darasa hilo kwa gharama zake binafsi za kiasi cha shilingi milioni 6.

Akizungumza nasi ,Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nailupa Ndung’anak  Mepukor alisema wananchi wa Kitongoji hicho walimsimamisha Kiruswa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini aliyekuwa akielekea kata nyingine kukagua miradi ya maendeleo kutembelea darasa hilo na kujionea mwenye watoto wakipata elimu chini ya mti bila kujali jua wala mvua.

Mepukor alisema jitihada za ushawishi wa akina mama ,vijana ,viongozi wa Milla maarufu kwa jina la Laigwanani ulimfanya Mbunge kwenda kutembelea darasa hilo ambalo bado lilikuwa halijakamilika kwa kukosekana mlango mmoja,madirisha sita ,bati 60 ,madawati 20,mbao,madawati 20 na umaliziaji wa kupiga Plasta hatua iliyomfanya mbunge kubeba gharama hiyo kwa gharama ya kiasi hicho cha fedha cha shilingi milioni 6

Mwenyekiti alisema ujenzi wa darasa hilo uliofanywa na wananchi hao umetokana na michango ya kila kaya kwa fedha taslimu na uuzwaji wa mifugo kwa kila kaya na kujitoa kwa uchimbaji wa msingi na ujenzi wa darasa sambamba na ubebaji wa matofali kwa kila mwananchi wa kitongoji hicho ili watoto waweze kusoma ndani ya darasa hilo wakiwa wameketi kwenye madawati.    

‘’Tulijitahidi hadi kufikia hatua hiyo na Mbunge Kiruswa kukubali tu kufika kuona hali halisi ya watoto kusomea chini ya mti na kuona jitihada za wananchi katika ujenzi wa darasa hilo ameamua kumalizia kila kitu kwa gharama zake’’alisema Mepukor

Akizungumza katika mara baada ya kuahidi kumalizia hatua iliyobaki ,Kiruswa alisema kwa kuwashukuru wananchi hao kwa kujitoa na kufanikisha ujenzi wa darasa hilo na kusema kuwa hatua hiyo imempa faraja kubwa sana na yeye kuamua kuchangia na kumamilisha ujenzi wa darasa ili watoto waweze kusoma karibu na makazi na kuondoka na kutembea umbalim mrefu kufuata elimu.

Kiruswa alisema jukumu la kutaka watoto kusoma na kupata elimu bora ni la kila mwananchi wa Jimbo la Longido na sehemu kubwa inayofanywa na serikali inapaswa kuungwa mkono na wananchi na kilichofanyika katika kitongoji cha Lailupa ni kitendo kinachopaswa kupongezwa na kuungwa mkono na yeye na Halmashauri ya wilaya ya Longido.

Alisema jukumu lake la pili ni kuhakikisha shule hiyo ya awali inasajiliwa na kupata mwalimu mwenye sifa tofauti na sasa mwalimu anayewafundisha ni wa kujitolea na asiyekuwa na sifa na jukumu hilo linabebwa na yeye na hadi mwakani januari kila kitu kinapaswa kukamilika ili watoto wasomeshwe na mwalimu mwenye sifa shule kutambuliwa na serikali.

Naye Diwani wa Kata ya Gelai Meirugoi,Daniel Nasinda alisema kuwa watoto wa Kitongoji cha Lailupa hutembea umbali wa zaidi ya km 10 kwenda na kurudi kusaka elimu hatua ambayo ni hatari kwao kwa kuwa na eneo hilo lina wanyama wakali na ndio maana wazazi walijitoa kujenga darasa ili iwe salama kwa watoto wao kwenda shule.














 


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Bw. Nassoro Shemzigwa, amefungua mafunzo ya siku moja kwa ajili ya waandishi wasaidizi na waendeshaji wa mashine za BVR, yatakayofanyika katika kata zote 18 za wilaya hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya awamu ya pili ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa J.K.Nyerere uliopo makao makuu ya halmashauri hiyo, Bw. Shemzigwa aliwapongeza washiriki kwa kuaminiwa na kuteuliwa tena kushiriki katika utekelezaji wa jukumu hilo muhimu la kitaifa.

Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura linatarajiwa kuanza rasmi Mei 16 hadi 22, 2025 katika kata zote 18 za Wilaya ya Longido.

“Mnatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, kutunza vifaa mlivyopewa, kuepuka vitendo vya uzembe au visivyofaa vinavyoweza kuhatarisha mchakato huu muhimu. Fanyeni kazi kwa weredi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,” alisisitiza Mkurugenzi.

Amesema lengo ni kuhakikisha kila mwananchi mwenye sifa anapata haki yake ya msingi ya kupiga kura na kuchagua viongozi anaowataka katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Serikali Kuu.

Kwa upande wake, Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Longido, Bw. Nevviling Lymo,alisema viongozi wa jimbo na kata kwa pamoja  watahakikisha wanasimamia kwa karibu utekelezaji wa zoezi hilo ili lifanikishwe kwa viwango vya juu na kwa wakati uliopangwa.

“Ni wajibu wa kila afisa mwandikishaji kuhakikisha taarifa zote muhimu zinawasilishwa kwa wakati na mahali sahihi, na kushirikiana kikamilifu na watendaji walioko vituoni ili kufanikisha kazi hii,” alisema Bw. Lymo.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo, Mwenyekiti wa Mafunzo, Bw. Ernest Lotakajack Zakayo, alisema wako tayari kuhakikisha zoezi linafanyika kwa ufanisi mkubwa na kuleta matokeo chanya katika jimbo hilo.
















Zaidi ya shilingi milioni 450 zimepelekwa katika Jimbo la Longido Mkoani Arusha kwa ajili ya kumalizia miradi ya afya katika Jimbo hilo ili kuwaondolea usumbufu wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya matibabu.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido,Dkt Steven Kiruswa katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika  Tarafa ya Longido kata ya Kimokowa na Namanga na kusema kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inawajali na kuwathamini wananchi wa Longido.

Dkt Kiruswa alisema fedha hizo ni fedha maalumu ambazo zimetolewa na serikali nje ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 na zimelenga pekee yake katika sekta ya afya kumalizia ujenzi wa zahanati na vituo vya afya katika baadhi ya kata wilayani Longido.

Alisema kuna kata vituo vya afya vilianza kujengwa kwa michango ya wananchi na mchango wake binafsi Mbunge lakini miradi hiyo haikuweza kukamilika kutokana na juhudi za Mbunge kuomba fedha serikali na serikali imeona umuhimu wa kutoa fedha hizo ili kumalizia miradi hiyo na kuondoa adha kwa wananchi kufuata huduma umbali mrefu bila sababu za msingi.

Mbunge Kiruswa alisema katika Kata ya Mundarara zilipelekwa shilingi milioni 250 kwa ajili ya kumalizia Zahanati ya kisasa iliyojengwa katika kata hiyo yenye msongamano mkubwa wa watu kwa kuwa kata ya Mundarara imebarikiwa kuwa na madini ya ruby hivyo kuna wananchi wengi kutoka maeneo mbali mbali ya nje ya wilaya ya Longido hivyo kuwa na uhitaji mkubwa wa zahanati.

Alisema katika Tarafa ya Ketumbeine Kijiji cha Losuruway zanahati ya kisasa imejengwa na imekamilika lakini ilikuwa haina nyumba ya daktari hivyo serikali ilitoa shilingi milioni 45 kumalizia ujenzi wa nyumba hiyo sambamba na kata ya Loirienyito kituo cha afya kimepelekwa fedha shilingi milioni 45 kumalizia ujenzi wa kituo hicho cha afya.

Naibu Waziri Kiruswa alisema kata ya Kimokowa Tarafa ya Longido zimepelekwa shilingi milioni 45 kuendeleza na kumalizia zanahati iliyojengwa katika kata hiyo sambamba za shilingi milioni 30 zilizopelekwa kata ya Noondoto Kijiji cha Ngusero kumalizia ujenzi za Kituo cha afya,shilingi milioni 30 kupelekwa Kijiji cha Naadale kumazilia ujenzi wa kituo cha afya.

Alisema katika fedha hizo pia shilingi milioni 30 zimepelekwa katika Kijiji cha Wosiwosi kilichopo Tarafa ya Ketumbeini kumalizia ujenzi wa kituo cha afya ambapo awali wananchi na mbunge walianzisha ujenzi wa kituo hicho na serikali imewakumbuka na kutoa fedha kwa ajili ya umaliziaji wa kituo hicho.

Dkt Kiruswa alisema kuwa wananchi wa Jimbo hilo wanamshukuru sana Rais kwa uamuzi wake wa kutoa fedha kwa ajili ya umaziaji wa zahanati na vituo vya afya katika baadhi8 ya kata na kusema kuwa huo ni uamuzi ulioshukuruliwa kwa akiasi kikubwa na wananchi wa Jimbo la Longido.

Mbunge huyo yuko katika ziara ya siku nne katika Jimbo la Longido kueleza miradi iliyotelekezwa na serikali na mchango wake kama mbunge kwa wananchi wa Jimbo hilo na kueleza ahadi alizoahidi ambazo amezitekeleza kwa asilimia mia moja.


 


    

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mheshimiwa Salum Kalli, ameitembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana Lekule mnamo Mei 7, 2025, ambapo alipata fursa ya kujionea maendeleo ya shule hiyo pamoja na kuzungumza na wanafunzi.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Kalli aliwahimiza wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwa na nidhamu wawapo shuleni, akisisitiza kuwa elimu ndiyo njia pekee ya kufikia mafanikio ya maisha. Aliwataka kuepuka kabisa vitendo vya mimba za utotoni ambavyo vinaweza kuwa kikwazo kikubwa katika safari yao ya kielimu na kuwakatisha ndoto zao za baadae.

Aidha, kama sehemu ya kuwatia moyo, Mkuu huyo wa Wilaya aliwazawadia wanafunzi hao nyama ya ng’ombe kwa ajili ya chakula, jambo lililopokelewa kwa shangwe na furaha kubwa.

Akizungumza kwa niaba ya shule hiyo, Mkuu wa Shule Mwalimu Anna Wenseslausi alimshukuru sana Mkuu huyo wa Wilaya kwa ujio wake na zawadi aliyoitoa.