Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wahitimu wa kozi mbalimbali (hawapo pichani) katika Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.

Sehemu ya wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya 41 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye mahafali hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (mwenye kofia nyekundu) akijumuika katika maandamano ya wahitimu wa kozi mbalimbali (hawapo pichani) katika Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu hao wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahim Mahumi akitoa akitoa neno la utangulizi kwa wahitimu wa kozi mbalimbali (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na wahitimu hao wakati wa Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kulia) akiteta jambo na Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho (kushoto) wakati wa Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.



Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho akiwasilisha taarifa ya utendaji wa chuo kwa mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa mahafali ya 41 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.



Sehemu ya wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya 41 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakifurahi wakati wa maandamano yaliyofanyika nje ya Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (mwenye kofia nyekundu) akiteta jambo na Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Prof. Masoud Muruke (wa kwanza kulia) ambaye amemwakilisha Mwenyekiti wa bodi hiyo wakati wa Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali wa chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho.

Sehemu ya wazazi na walezi wa wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa Mahafali ya 41 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (mwenye kofia nyekundu) akitazama maandamano ya wahitimu wa kozi mbalimbali (hawapo pichani) katika Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu hao wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida. Wengine ni Viongozi wa mkoa huo na Watendaji wa chuo hicho.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakati wa Mahafali ya 41 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.

Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakielekea kwenye Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission wakati walipojumuika kwenye msafara wa wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi huo mkoani Singida.


Na. Veronica Mwafisi-Singida


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewaasa wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kusimamia na kutunza maadili ya taaluma walizosomea kwa ustawi wa taifa.

Mhe. Simbachawene amesema hayo leo tarehe 30 Mei, 2025 kwenye Mahafali ya 41 ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Social Rwoma RC Mission mkoani Singida.

Kuhitimu ngazi za Shahada, Stashahada na Astashahada katika fani mbalimbali sio jambo dogo, elimu mliyoipata ni kubwa, hakikisheni mnasimamia na kutunza maadili ya elimu hiyo kwa manufaa yenu na ustawi wa taifa amesisitiza Mhe. Simbachawene.

Mhe. Simbachawene amewataka wahitimu walioajiriwa katika Utumishi wa Umma na watakaoajiriwa kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na kutunza siri za Serikali na kuepuka rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao na wahitimu ambao hawana ajira kutumia ujuzi walioupata kujiajiri kwa maendeleo ya taifa.

Aidha, ametoa rai kwa wahitimu hao kutunza afya zao pamoja na kuepuka Magonjwa Yasiyoambuza kwa kuwa taifa linawahitaji katika kukuza uchumi wa nchi.

Vilevile, Mhe. Simbachawene ameueleza uongozi wa chuo hicho kuwa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ina matarajio makubwa na Chuo hicho kwa kuwa kimeimarika sana hasa katika kuwajengea uwezo watumishi wa Umma na kutoa wahitimu mahiri na wenye uzalendo wanaoleta chachu ya maendeleo nchini.

Kadhalika, Mhe. Simbachawene amewapongeza Walimu, Wazazi na Walezi wa wahitimu hao kwa jitihada kubwa ambazo kila mmoja kwa nafasi yake amezifanya ili kufanikisha kupata wahitimu hao wa ngazi za Shahada, Stashahada na Astashahada katika fani mbalimbali.

Awali, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Ernest Mabonesho amemshukuru Waziri Simbachawene kwa kukubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo na kumtaarifu kuwa jumla ya wanafunzi 1330 wamehitimu kozi mbalimbali katika chuo hicho wakiwemo wanawake 906 na wanaume 224.

Dkt. Mabonesho ameongeza kuwa pamoja na jitihada nyingine zinazofanywa na chuo hicho, wameendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za ndani ikiwemo Chuo cha Hombolo na vyuo vingine mbalimbali pamoja na vya nje ya nchi kwa lengo la kuboresha ujuzi na kubadilishana uzoefu katika utendajikazi.

“Mhe. Mgeni rasmi tumefanya jitihada mbalimbali ili kuboresha mafunzo yetu kwa kushirikiana na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi hasa vinavyohusika na masuala ya Utumishi wa Umma ikiwemo chuo cha Hombolo pamoja na vyuo vingine ili kuweza kupata fursa ya kujifunza na kuboresha utendajikazi alisema Dkt. Mabonesho.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahim Mahumi amesema taifa limepata wahitimu ambao ni nguvukazi nyingine watakaosaidia utendajikazi katika Utumishi wa Umma na taifa kwa ujumla.

Aidha, SACP. Mahumi amemshukuru na kumpongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene kwa kusimamia miongozo mbalimbali pamoja na taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo ambayo imekisaidia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kuhitimisha wanafunzi wanaoweza kutekeleza majukumu mbalimbali pasipokuwa na changamoto zozote.
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: