Mbio za Mwenge wa Uhuru, zimeendelea kukimbizwa Mkoani Njombe ambapo katika Wilaya ya Makete Miradi 8 yenye thamani ya Shilingi Bilioni  1.453,205,190)=  imetembelewa na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru.

Akizungumza kwa nyakati tofauti Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ndg. Godfrey Eliakim Mnzava, amesema kuwa lengo la Serikalini ni kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi.

" Mwenge huleta Matumaini pasipo na Tumaini, hivyo basi niwapongeze Halmashauri ya Wilaya ya Makete, kwa kusogeza huduma za kijamii kwa Wananchi" Alisema Ndg. Mzanva.

Aidha, Ndg. Mnzava amewataka viongozi Wilayani humo kuendelea na Kampeni ya Kupinga rushwa , ikiwa ni pamoja kuwa na Klabu za Rushwa katika kila Shule Wilayani humo.

Sambamba na hayo, Mwenge wa Uhuru Wilayani humo, umekagua Vikundi mbalimbali vya kijasilimali ambavyo vimekuwa vikipewa Fedha za mikopo  ya asilimia 10 kama vile, Kikundi cha Bodaboda cha Ujuni kilichopo Kata ya Kitulo.

Ikumbukwe kuwa, Mwenge wa Uhuru, umekagua na Kutembelea Miradi 8, ya Shamba la Miti 203, ya Matunda ya Parachichi na Kushiriki kupanda Miti 15, Umzindua mradi wa Maji katika kijiji Cha Tandala, Umetembelea mradi wa Uhifadhi wa Mazingira katika Shamba Darasa la Msitu wa Kanisa la Roman Katholic Kisinga.

Miradi mingine ni kama vile, Kutembelea Uendelevu wa Kituo cha Mafuta cha BEM, Kikundi cha Bodaboda Ujuni, Kupokea taarifa ya Hasama za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Kupokea taarifa ya Lishe na kugawa viini Lishe Kwa Watoto na Mama Wajawazito.

Pia, Mwenge wa Uhuru, umetembelea Kazi iliyofanywa na asilimia 5 ya  Fedha za michango ya Wananchi, Umepokea Taarifa ya mradi na kuweka Jiwe la Msingi katika Madarasa 12, na Matundu 20 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Mount Chafukwe, Umezindua Klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Mount Chafukwe na Chama Cha Skauti, pamoja na Kuweka Jiwe la Msingi katika Kituo cha Afya Mfumbi pamoja na Kupokea taarifa za VVU/Ukimwi pamoja na Ugonjwa wa Malaria.Share To:

Post A Comment: