Articles by "MWENGE2024"
Showing posts with label MWENGE2024. Show all posts

 

Na Imma Msumba : Kibaha

MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amesema kuwa maandalizi ya uzinduzi wa kuwasha Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka utawashwa Mkoani hapa umefikia asilimia 96.

RC Kunenge amesema hayo leo tarehe 25 Machi 2025 kama jinsi mnavyoona Uwanja umependeza tumeotesha majani na kutengeneza majukwaa manne ikiwa ni pamoja na jukwaa la VIP katika

Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha Pwani.
RC Kunenge amesema kuwa mambo yanazidi kwenda kama vile yalivyopangwa.

"Tumetengeneza miundombinu ya maji , umeme na pia tumeweka taa ambazo zitatumika hata baada ya sherehe za kuzindua kuwasha Mwenge wa Uhuru uwanja utatumika kwa shughuli mbalimbali.

Wakati huohuo ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani na Mikoa jirani wajitokeze kushiriki katika uzinduzi huo ambapo wanatarajia watu 16,000kuhudhuria.

Uzinduzi huo umepangwa kufanyika tarehe 2 Aprili 2025.

"Kauli mbiu ya Mwenge wa uhuru mwaka huu inasema "Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu 2025 kwa amani na utulivu" amesema Kunenge.





Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru 2024 Ndugu Godfrey Mnzava amezitaka Halmashauri zote hapa nchini kuhakikisha vikundi vya vijana vinavyofanya vizuri kwenye miradi ikiwemo ya ufugaji vipewe vipaumbele kupitia mikopo ya asilimia kumi inayotolewa halmashauri.

Akizungumza wakati alipotembelea mradi wa uwezeshaji vijana kikundi cha Iloonyok kata ya Engikaret Wilayani Longido,Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Godfrey Mnzava aliagiza halmshauri zote nchini kuwapa kipaumbele kwenye mikopo ya asilimia kumi  vijana wanaofanya vizuri katika miradi mbalimbali waliyobuni.

"Vijana wanaofanya vizuri kwenye miradi wapewe vipaumbele vya kupata mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri kwani wanaonyesha bidii katika urejeshwaji wake"

Alisisitiza vijana hao kuendelea kukopeshana kama faida ya mikopo kutokana na aina ya ufugaji wa mifugo wanayonenepesha na kuuza kisha faida wanayopata wakitumia kukopeshana bati kwaaajili ya ujenzi wa nyumba za kisasa

Naye Katibu wa Kikundi hicho,Looyani Kiliani akisoma taarifa ya kikundi hicho alisema  lengo lao ni kukuza mtaji na kuimarisha uchumi kwa makundi ya vijana kwani mradi huo ulianza na sh,milioni 4 zilizotokana na fedha za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwaaajili ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Alisema awali walianza kununua mbuzi 10,kondoo 20 ,ndama mmoja pamoja na chakula na madawa kwa lengo la kunenepesha na kuuza kwa faida  ambao mradi huo uliwawezesha kukuza mtaji kwa kuongeza idadi ya mifugo kutoka mbuzi na kondoo 30 hadi kufikia 40 ikiwemo kurejesha marejesho ya mkopo

Alisema kikundi hicho kinatarajia kuimarisha hali ya makazi kwa wanachama wake kwa kutenga kiasi cha sh ,30,000 kwa kila wanachama kwaaajili ya ununuzi wa bati za ujenzi kutokana na faida wanayoipata baada ya uuzaji wa mifugo mwaka huu

Aliishukuru serikali chini ya uongozi wa Rais,Samia Hassan Suluhu kwa utoaji wa mikopo ya asilimia kumi inayowasaidia kuwa na mradi huo unaowasaidia kuboresha uchumi.

Mwenge huo ukiwa wilayani Longido  ulipitia miradi nane yenye thamani ya sh,bilioni 6.4 ambapo mradi moja iliwekwa jiwe la msingi,miradi mitano ilitembelewa huku miradi miwili ikizinduliwa

Awali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Emmanuela Kaganda  akikabidhi mwenge huo wilayani Longido ulitokea wilayani Arumeru,alishukuru kamati ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana naye pamoja na watumishi  wengine akiwemo Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Arusha Vijijini, Suleiman Msumi ambao kwa pamoja waliwezesha miradi hiyo kuzinduliwa na mingine kuwekwa mawe ya msingi na kiongozi huyo wa mbio za mwenge.








Wananchi zaidi ya 41,168 wa vijiji sita kata ya Akheri Wilayani Arumeru Mkoani Arusha wameanza kunufaika na mradi wa maji safi baada ya wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kusambaza huduma hiyo.

Akisoma taarifa mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Godfrey Mnzava, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Arumeru, Injinia Shabir Waziri amesema mradi huo umegharimu sh. bilioni 1.563 .

Injinia Shabir amesema wananchi hao watanufaika na mradi huo wa maji uliofikia asilimia 95 ya utekelezaji wake na kuongeza kuwa ujenzi  ulianza Aprili 16,2022 na unatarajiwa kukamilika Septemba 30,2024.

Amesema kazi za mradi huo zilizotekelezeka ni ujenzi wa vyanzo vya maji vya mto Malala, ujenzi wa matenki matatu yenye mita za ujazo 500,135 na 50, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa mabomba umbali wa mita 48,172 na ujenzi wa ofisi.

Kwa upande wake Mnzava amewaomba wananchi hao kulinda vyanzo vya maji na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu zinazosababisha uharibufu badala yake miundombinu ya maji hayo itunzwe

“Lindeni vyanzo vya maji kwani Rais Dkt Samia Hassan Suluhu amedhamiria kutua akinamama ndoo kichwani hivyo miundombinu hii itunzwe kwa manufaa yenu,” amesema Mnzava.

Wakati huo huo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, John Palangyo ameishukuru serikali kupeleka maji kwa wananchi hao ambao awali walikuwa wakikabiliwa na adha kubwa ya maji.

Kwa mujibu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini utekelezaji wa miradi Mwaka wa Fedha 2023/2024 katika mwaka wa fedha 2023/2024, Wakala ulipanga kutekeleza jumla ya Miradi 1,546 katika mikoa 25 nchini, inayogharimu Tshs 500,342,398,033.25.

Miradi hiyo inategemewa kuhudumia watu wapatao 2,274,193 katika vijiji 844.

Katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2023/2024, hadi kufikia Desemba 31, 2023 jumla ya miradi 374 iliyogharimu  Tshs 128,177,655,882 ilikuwa imekamilika.

RUWASA inaendelea na utekelezaji wa miradi 1,172 iliyobakia ili kutimiza adhma ya serikali ya kutoa huduma ya uhakika ya Maji Safi na Salama vijijini.


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 Godfrey Eliakimu Mnzava amezitaka Taasisi za serikali pamoja na mashirika ya umma kutumia mfumo wa  kieletroniki wa  NeST kwaajili ya manunuzi ili kudhibiti mianya ya  rushwa  pamoja na kuondoa upendeleo katika zabuni zinazotolewa ili kuhakikisha miradi inayojengwa inazingatia ubora.

Mnzava ametoa agizo hilo wakati wa ukaguzi wa barabara ya boksi kalavati Mbuguni,Shambarai Burka iliyojengwa kwa gharama  ya sh,milioni 99.499 na  Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA).

Alisema endapo mfuko huo ukitumiwa  vema utapunguza masuala ya rushwa ikiwemo upendeleo wa zabuni na kazi  zinazotolewa hususan za ujenzi ikiwemo upendeleo kwenye miradi kwa Watu wasio na sifa za ujenzi.

"Tumieni mfumo wa NeST kwaajili ya manunuzi lakini pia mfumo huo utadhibiti rushwa haswa katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo"

Awali Mhandisi wa TARURA wilaya ya Arumeru,Julius Kaaya alisema kalavati hilo lenye urefu wa kimolita 7.9 linunganisha kata hizo kwaajili ya kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji wa mazao kutoka shambani hadi sokoni.

Alisema kazi zilizofanyika ni Kuta za Daraja pamoja na masikio yake,deku ya Daraja na sehemu ya relief za vizuizi na Daraja hili limejengwa na makandarasi wa kampuni ya Lenana Holding Company Limited 

Wakati huo huo,baadhi ya wananchi wa Shambarai Burka akiwemo ,Mariam Zakaria alishukuru daraja hilo kujengwa kwani Awali wananchi hao walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya barabara kujaa maji kutokana na ukosefu wa daraja na kuomba barabara hiyo kutengenezwa zaidi ili kuondoa changamoto ya vumbi.

"Ujenzi wa daraja hili utarahisisha bidhaa zetu kutoka shambani kwenda soko la Mbuguni na masoko mengivkwa haraka zaidi ikiwemo kijikwamua kiuchumi, tunamshukuru sana Rais Samia Hassan Suluhu kwa kwa barabara hii "

Mwenge wa uhuru umewasili rasmi  Mkoani Arusha ulitokea Mkoani Manyara  ambapo utakimbia  kilomita 1182.9 na kukagua miradi 65 yenye thamani ya sh,bilioni 61.6

Awali  mwenge huo wa uhuru ulipokelewa  katika kijiji cha Migungani kata ya Mbuguni Wilayani Arumeru na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Nurdin Babu  ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro amesema mwenge huo utazindua miradi hiyo Mkoani Arusha 

Mwenge huo wenye wenye kauli mbiu ya " Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu"
























Mwenge wa uhuru umezindua mradi wa maji wa mamlaka ya wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) uliopo kijiji cha Magara Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara wenye thamani ya shilingi Milioni 801.

Akisoma taarifa ya Mradi huo, Meneja wa RUWASA wilaya ya Babati, Mhandisi Felix Mollel amesema utahudumia watu wapatao 5,137.

Chanzo cha mradi huo wa maji ni mto Magara ambapo mtandao wa mabomba ni kilomita 20.7.

Mkuu wa wilaya ya Babati, Lazaro Twange ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili mradi huo mkubwa.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2024, Godfrey Mnzava  amewapongeza RUWASA kwa kutimiza adhma ya serikaki ya kumpunguzia mwananchi adha ya kutembea umbali mrefu kufuata maji.

Hata hivyo baada ya Mwenge wa uhuru kuridhia kuzindua mradi huo wa maji wa kijiji cha Magara ameagiza kibao cha uzinduzi  kihamishwe kiwekwe kwenye tenki mlimani badala ya kwenye kituo cha kuchotea maji.

Nao Wananchi wa kijiji cha Magara wamemshukuru serikali kwa kuwapatia mradi huo wa maji kwani umekuwa mkombozi kwao. 

Kaulimbiu ya Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2024  "Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu".



Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake mkoani Singida ambapo utatembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo 47 yenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni 100. 

Kati ya fedha hizo wananchi wamechangia zaidi ya Milioni 287, Wahisani Bilioni Moja na Serikali Kuu imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 30. Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Chikuyu wilayani Manyoni kati ya Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rozimary Senyamule. 

Rc Dendego amesema kwa mkoa wa Singida Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kilomita 800 kwenye Wilaya Tano na Halmashauri Saba za Mkoa huo Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida amewasisitiza wananchi wa mkoa wa Singida kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuushangilia Mwenge wa Uhuru pamoja na kusikiliza ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru wa Mwaka huu pindi utakapopita kwenye maeneo yao. 

Kwa upande wake, Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava, amewaagiza Viongozi wa mkoa wa Singida wahakikishe taarifa zote za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuwepo kwenye maeneo ya miradi yote ili kujua ubora na thamani halisi ya fedha zilizotumika kwenye miradi hiyo ili kujua ubora kuhusu miradi hiyo. 

Mnzava pia amesisitiza nyaraka zote zinazohusiana na miradi kuwepo eneo la miradi pamoja na Wataalamu wote waliosimamia utekelezaji wa miradi itakayopitiwa na Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kuwepo kwenye miradi hiyo ili waweze kutoa ufafanuzi kwa maswali watakaoulizwa na wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa lengo likiwa ni kujua kama miradi hiyo imetekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya fedha. 

Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Manyoni umetembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo Saba yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2. 

Kauli mbinu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.


Na Imma Msumba : Makambako 

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava ameitaka Halmashauri ya mji Makambako kuendelee kuwasimamia wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF ili kuhakikisha wanazalisha kile wanachowezeshwa na serikali.

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea mradi wa parachichi kwa wanufaika wa TASAF katika Halmashauri ya mji Makambako,ambao walipewa miche kumi ya Parachichi kila mmoja ili kuwajengea uchumi endelevu.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo Mtendaji wa kata ya Lyamkena Giveni Kyando,amesema kuwa miche hiyo ya Parachichi walipoewa wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF imeendelea kukua vizuri na lengo kuu la mradi ni kupata kipato kwa wanufaika kwa kuuza matunda na kuyatumia kwa kula ili kuboresha afya ya familia.

Miongoni mwa wanufaika hao Bi.Evelina Nyali mkazi wa mtaa wa Lyamkena, licha ya kuishukuru serikali kwa kuweka mpango huu, ameiomba serikali iendelee kuwasaidia walengwa wengine ambapo wapo kwenye hali ngumu ya kimaisha na wanahitaji msaada.

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria tukio hilo akiwemo Siza Katawa na Scola Mbwanji, wamewasisitiza wanufaika wa TASAFU wawe wanatumia vyema misaada wanayopewa na serikali, ili wajikwamue kiuchumi na wasiwe tegemezi tena kwenye jamii.

Mwenge wa uhuru wa kwa Halmashauri ya mji Makambako umezindua na kutembelea miradi minne yenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 308.

Ikumbukwe Mauli mbiu ya Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu inasema "Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu"