Na Imma Msumba : Makambako 

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava ameitaka Halmashauri ya mji Makambako kuendelee kuwasimamia wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF ili kuhakikisha wanazalisha kile wanachowezeshwa na serikali.

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea mradi wa parachichi kwa wanufaika wa TASAF katika Halmashauri ya mji Makambako,ambao walipewa miche kumi ya Parachichi kila mmoja ili kuwajengea uchumi endelevu.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo Mtendaji wa kata ya Lyamkena Giveni Kyando,amesema kuwa miche hiyo ya Parachichi walipoewa wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF imeendelea kukua vizuri na lengo kuu la mradi ni kupata kipato kwa wanufaika kwa kuuza matunda na kuyatumia kwa kula ili kuboresha afya ya familia.

Miongoni mwa wanufaika hao Bi.Evelina Nyali mkazi wa mtaa wa Lyamkena, licha ya kuishukuru serikali kwa kuweka mpango huu, ameiomba serikali iendelee kuwasaidia walengwa wengine ambapo wapo kwenye hali ngumu ya kimaisha na wanahitaji msaada.

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria tukio hilo akiwemo Siza Katawa na Scola Mbwanji, wamewasisitiza wanufaika wa TASAFU wawe wanatumia vyema misaada wanayopewa na serikali, ili wajikwamue kiuchumi na wasiwe tegemezi tena kwenye jamii.

Mwenge wa uhuru wa kwa Halmashauri ya mji Makambako umezindua na kutembelea miradi minne yenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 308.

Ikumbukwe Mauli mbiu ya Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu inasema "Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu"

Share To:

Post A Comment: