BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mkoani Geita, limewafuta kazi watumishi 3 wa Halmashauri hiyo kwa mujibu wa Kanuni za Kiutumishi .

Akitoa Taarifa hiyo katika kikao Maalumu kilichoketi mara baada ya kukamilika kwa Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Butobela, Charles Kazungu amesema watumishi hao wamefutwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwemo makosa ya Utoro kazini.

“Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kauli moja limekwenda kuwafuta kazi watumishi watatu kwasababu ya kanuni zetu za kiutumishi ,” Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Kazungu.

Kazungu amewataja watumishi hao kuwa ni Aden Benard ambaye ni Afisa Mtendaji katika Kijiji cha Nzera, John Misango Afisa Mtendaji Kijiji na Walter Innocent ambaye pia alikuwa ni Mteknolojia Maabara, pia Baraza linaendelea kuwachungunza watumishi wawili akiwemo Mussa Alfredy ambaye ni Afisa Tabibu Msaidizi pamoja na Elisha Makaja ambaye pia ni Mteknolojia wa Dawa.

Share To:

Post A Comment: