Dickson Mnzava, same.

Fainali za Mathayo Cup ngazi ya tarafa zimehitimishwa rasmi na washindi wa kila tarafa kujinyakulia zawadi yake.

 

Katika tarafa ya mwembe mbaga mchezo wa fainali ilikuwa Kisiwani united vs Mshewa FC na Mshewa FC kuibuka Mabingwa wa tarafa hiyo kwakuchapa bila huruma Kisiwani united goli 2-0 matokeo ambayo yamewaduwaza wengi kwani watu wengi waliamini Kisiwani united ndio Mabingwa kwani mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa Kisiwani.

 

Mchezo wa fainali ya pili ngazi ya tarafa ulichezwa kwenye katika uwanja wa Makanya ambapo Makanya united walikuwa wakipepetana na kirua FC toka Hedaru mchezo uliomalizika kwa makanya kushinda goli 1-0 na makanya united kuwa Mabingwa wa tarafa ya chome suji.

 

Kilele cha fainali hizo ngazi ya tarafa kilihitimishwa tarehe 28/01/2024 katika tarafa ya Same ambapo vigogo wa soka mjini Same Chato FC Kutoka kavambughu mjini Same waliivaa Green forest ya mjini Same mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Same sekondari na Chato FC kuibuka Mabingwa wa tarafa hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya penaliti 7-6.kwani dakika 90 timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1.

 

Mabingwa hao ngazi ya tarafa wamejinyakulia kila mmoja kombe na pesa tasilim milioni 2 seti ya jezi na mipira huku mshindi wa pili kila mmoja amejinyakuli pesa tasilimu milioni 1.2 jezi na mipira na mshindi wa tatu kujinyakulia kitita cha milioni 1 jezi na mipira.

 

Akizungumzia mashindano hayo mwenyekiti wa chama cha soka wilayani SADFA Raphael Senkoro amesema sasa wapo kwenye mchakato wa kupanga droo ya nane bora kuelekea kwenye fainali za jumla ngazi ya Jimbo ambayo inatarajiwa kuchezwa mapema mwezi February.

“Tumehitimisha fainali za tarafa leo na sasa tunaenda kukaa kupanga droo ya nane bora kuelekea kwenye fainali za jumla ngazi ya Jimbo kwenye mashindano yetu ya mheshimiwa Mbunge Mathayo Cup timu zote zimefanya vizuriii kumekuwa na ushindani mkubwa sana kwenye mashindano haya wenyewe wanahabari mmejionea ni mashindano makubwa mno kuwahi kutokea kwenye Jimbo letu hivyo tunaendelea kuwasihi vijana kuendelea kujifua zaidi kwani sasa ndio tunaanza”

“Alisema Rafael mwenyekiti SADFA na mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo”.

 

Mashindano hayo yalianza November mwaka jana yakiwa na jumla ya timu 53 Kutoka kwenye tarafa 3 ambazo zipo kwenye Jimbo la Same magharibi ambazo ni tarafa za mwembe mbaga, Chome suji na tarafa ya Same na yanatarajia kufungwa rasmi mwezi February tarehe 24.

Share To:

Post A Comment: