Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI itafuatilia utendaji kazi wa watumishi wa Mikoa na Halmashauri na kufuatilia changamoto za wananchi katika maeneo yao ili ziweze kutatuliwa.

 
Akieleza hayo Januari 27, 2024 katika kikao cha majumuisho na wataalamu wa afya ngazi ya CHMT, HMT za hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya, RHMT na MSD.
 
Aidha, kikao hicho ni baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa afya, utoaji wa huduma kwa wananchi na kuzungumza na watumishi katika Halmashauri ya Wilaya Morogoro, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na Manispaa ya Morogoro.

1000545406


Akieleza lengo la Serikali katika usimamizi wa miradi kukamilika kwa wakati lakini pia miradi kuendana na thamani ya fedha iliyowekezwa amesisitiza kila mtumishi atekeleze majukumu yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi huku akiwataka kuitumia na kuisimaia vizuri mifumo ya kieletroniki iliyofungwa kwani ukusanyaji wa fedha hizo husaidia kuendelea kuboresha huduma za afya.
 
Dkt. Mfaume amewataka watumishi hao kushirikiana na Wakurugenzi wao kwa sababu zipo baadhi ya Halmashauri ambazo fedha za kumaliza miradi zinapochelewa au kuwa hazitoshi Wakurugenzi wamekuwa wakitoa fedha kumaliza miradi ili huduma zitolewa na hivyo wao ni jukumu lao sasa kuhakikisha wanatoa huduma kwa wananchi kwa wakati.
 
Kwa upande mwingine Dkt. Mfaume amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa kuendelea kusimamia na kuzuia ugonjwa wa kipindupindu ambao kwa sasa upo kwenye baadhi ya mikoa na kuwakumbusha watendaji hao kuendelea kuweka mikakati ya kuzuia ugonjwa huo kwa kutunza vyanzo vya maji visichafuliwe na mifumo ya vyoo na maji taka kuimarishwa ili kuzuia maambukizi.

1000545404


“Natoa wito kwa watendaji wenzangu ni lazima tuchukue tahadhari na hatua za kinga dhidi ya magonjwa ya kuhara” amesisitiza
 Dkt. Mfaume
 
Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kusirye Ukio amesema, watayafanyia kazi yale yote waliyoelezwa kwa kushirikiana na watumishi wote kwa lengo la kutoa na kuboresha huduma kwa wananchi.
Share To:

Post A Comment: