Kocha Mkuu wa Timu ya Tabora United Denis Laurence amesema kuwa katika kipindi cha siku saba tangu alipojiunga na Timu anaridhishwa na viwango vya wachezaji kutokana na kujituma kwao kwenye mazoezi uwanjani.


Kocha Laurence amesema kuwa ameshangwaza kuona wachezaji kwa kipindi kifupi tangu alipojiunga na Timu hiyo yenye Makazi yake Mkoani Tabora wanamuonesha ushirikiano wakutosha nakusikiliza kila anachowaelekeza kwenye uwanja wa mazoezi na kwamba hajapata changamoto yoyote hadi sasa.


Ameongeza kuwa ushirikiano ambao wachezaji wanampa unatoa  taswira njema kuelekea kwenye michezo tisa ya Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara pamoja na michuano ya Kombe la Azam Sport Federation dhidi ya Singida Fountain Gate kufanya vizuri kwani ndio mkakati uliopo kwa sasa kama Timu.


“Nafurahi kuona wachezaji wananisikiliza vizuri, tunakwenda sawa ,tunazungumza Lugha moja , kwa huumuda mfupi ambao nimekuwa nao hapa kwangu ni maajabu, wanafuata ninachowaambia lakini pia wanafanyia kazi, hii kwangu ni kubwa sana kama kocha, muhimu nazidi kuwasisitiza kila mmoja ananafasi kwenye kikosi changu cha kwanza” amesema Kocha Laurence.


Ukiangalia kila mmoja anauwezo mkubwa, nahii ni kawaida kwa wachezaji wa  Afrika, muhimu ninachokifanya ni kuwaweka kwa pamoja wacheze kitimu ili tuweze kushinda, morali na hari zao zipo juu hivyo ninafurahia sana kuwepo na wachezaji wangu mazoezini na mazingira yote kwa ujumla.


Aidha katika hatua nyingine Kocha Laurence amesema kuwa hadi sasa tayari ameshapata kikosi chake cha kwanza lakini akasisitiza sio ndio kitadumu milele hapana kwani mfumo wake ni kuhitaji kila mmoja aweze kucheza kweye michezo hii iliyosalia kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2023/2024.


Tabora United itakuwa ugenini siku ya Aprili Nne katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza ikiwakabili Singida Fountain Gate kwenye mchezo wa ASFC na badae Aprili 14 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi hapa Mjini Tabora.


Imetolewa leo Machi 28


Na Christina Mwagala


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano


Tabora United

Share To:

Post A Comment: