Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiongozana na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde imetembelea Kituo cha  Jemolojia Tanzania (TGC) kinachotoa Mafunzo ya Uongezaji Thamani Madini  kwa ajili ya kukagua mradi wa ujenzi wa jengo  la kituo hicho ambalo litakuwa mahsusi kwa utoaji wa mafunzo ya kuongeza thamani,minada ya madini ya vito na maonesho ya madini.


Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt. David Mathayo amepongeza serikali kwa jitihada za kuboresha mafunzo katika eneo la uongezaji thamani madini ya vito na kutoa maagizo ya uharakishwaji wa taratibu za kuanza ujenzi wa mradi mapema ili manufaa yake kwa watanzania yaonekane.


Akizungumza katika Ziara hiyo Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kwamba jengo hilo pacha(_twin tower_) lenye thamani ya Tsh Bilioni 35 litakuwa na miundombinu mbalimbali ikiwemo madarasa, karakana (viwanda) vya uongezaji thamani madini, maabara za madini ya vito na bidhaa za usonara, mineral gallery, ofisi, mabweni ya wanafunzi, kantini na maduka. 


Mh Mavunde aliongeza pia kwamba Jengo hilo litafungamanisha mafunzo ya uongezaji thamani madini pamoja na viwanda vya uchakataji na biashara ya madini nchini kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo ili kuimarisha umahiri. Mradi huu pia, uhahusisha utolewaji wa mafunzo kwa watumishi kwa lengo la kuwaongezea uwezo (capacity building) pamoja na ununuzi wa vitendea kazi.


 Akitoa taarifa ya Mradi huo Kaimu Mratibu wa Kituo cha Jemolojia Tanzania(TGC) Mhandisi Ally Maganga ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mageuzi makubwa ya sekta ya madini na hasa kupitia uongezaji thamani wa madini ya vito ambao utekelezaji wake utachangiwa na kukamilika kwa mradi huu mkubwa na kutumia fursa hiyo pia kuiahidi kamati ya Bunge juu ya usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa mradi  huu kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa.Share To:

Post A Comment: