Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwezeshaji wa mitaji ya umma (PIC) imetembelea mradi wa kuboresha huduma ya maji na usafi wa Mazingira ulioanzishwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Maji na usafi wa mazingira AUWSA unaolenga kuondoa changamoto ya ukosefu wa maji katika Jiji la Arusha na maeneo ya jirani.
Mradi huo ambao umegharimu jumla ya shilingi Bilioni 520 huku utekelezaji wake ukianza tangu februari 18 mwaka 2016 na kupelekea kupata mafanikio makubwa ya kutibu maji taka na kuvuna majisafi yanayo changia kuongezeka kwa wingi wa upatikanaji maji baada ya kukamilika kwakwe disemba 2023.
Vuma Augustine ni Mbunge wa Kasulu ambaye ndiye Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji ya mitaji ya Umma Vuma ambapo ameeleza kuwa mradi huo utapunguza na kutatua kabisa changamoto ya ukosefu wa maji kwa wakati katika Jiji la Arusha na kuwapongeza kwa kukamilisha mradi kwa wakati na uaminifu mkubwa.
Sambamba na hilo Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo amewataka AUSWA kuhakikisha wanaendeleza juhudi za kusambaza huduma ya maji kwa wingi katika sehemu mbalimbali zenye ukosefu wa maji katika Jiji la Arusha kutoka na baadhi ya wananchi kuendelea kulalamika kukosa huduma ya maji.
Kama inavyo fahamika jukumu la AUWSA ni kusimamia, kuratibu na kuendeleza Shughuli zote za huduma ya usambazaji wa majisafi na Huduma za usafi wa Mazingira katika Jiji la Arusha na maeneo ya pembezoni hivyo imenzisha utekelezaji wa mradi huo ili kuendana na kasi ya ukuaji wa Jiji hilo.
Post A Comment: