Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais -TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume ameitaka Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya(CHMT) kuhakikisha vifaa na vifaa tiba vyote vilivyopelekwa Hospitali ya Wilaya ya Morogoro Vijijini kufungwa kutumika kwa kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt. Mfaume akizungumza na timu hiyo na watumishi wa afya alipokuwa akikagua ujenzi na huduma zinazotolewa hospitalini hapo,

Mkurugenzi huyo amesema hospitali imeanza kufanya lakini baadhi ya vifaa na vifaa tiba vilivyopelekwa havijafungwa ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

“Serikali imenunua vifaa tiba ili kuwaondolea adha wananchi wake katika bajeti ya mwaka 2022/23 jumla ya Sh.Milioni 550 zilitengwa kununua vifaa na vifaa tiba katika hospitali hii na mpaka sasa fedha hizo zimekwishapokelewa na kwa upande wa ununuzi wa vifaa na vifaa tiba vimenununuliwa vyenye thamani ya sh.milioni 247 hivyo ni jukumu la watumishi kushirikiana na kuhakikisha wanavifunga, wanavitumia na kuvitunza,”amesema.

Aidha, amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu akieleza takwimu kuonesha wilaya hiyo ina changamoto ya viashiria vya upotevu mkubwa wa bidhaa za afya.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Robert Manyerere amesema hospitali hiyo ni msaada kwa wakazi 387,736 wa Halmashauri hiyo.

Share To:

Post A Comment: