Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amefika kwenye milima ya Kilimarondo Nachingwea kukagua na kufuatilia Utekelezaji wa Kazi ya Uchimbaji visima inayofanywa na Magari ya Mitambo ya Uchimbaji iliotolewa kwa mikoa yote nchi nzima na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
Akiwa Nachingwe Waziri Aweso ameshuhudia Gari maalumu ya Mkoa wa Lindi ikifanya kazi baada ya kuwa imepaki muda mrefu mpaka kupeleka Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa kufika na kutoa maelekezo mahususi.
1000543598
Katika hatua nyingine, Waziri Aweso baada ya kushiriki zoezi la uchimbaji ametoa maelekezo mahususi nchi nzima yatakayosimamiwa na Meneja wa Uchimbaji Visima na ujenzi wa Mabwawa Mhandisi Ndele Mengo aliemteua hivi karibuni.
Aidha, Amesisitiza kuwa atafanya kazi ya kusimamia na kufuatilia kwa ukaribu utendaji kazi na ufanisi wa mitambo hiyo na kutoa maagizo magari yote ya uchimbaji kutoondolewa na kubaki kwenye mikoa yaliopo kabidhiwa.
Mwisho Wananchi wa Kijiji cha Kilimarondo wametoa shukrani zao za dhati kwa kupata Maji baada ya kuteseka kwa muda mrefu kutokana na changamoto hiyo sababu kubwa ikiwa ni umbali wa eneo lao uliopelekea baadhi ya huduma za kijamii kuchelewa.
Share To:

Post A Comment: